Sunday, May 24, 2015

Ajira Mpya Kwa Walimu 2015........Haya Ni Majina Ya Awamu Ya Pili Pamoja Na Mabadiliko Ya Vituo Vya Kazi


Tarehe 27  na 30  Aprili, 2015,  Ofisi ya Waziri Mkuu  -  TAMISEMI ilitangaza ajira ya wahitimu wa mafunzo ya ualimu na mafundi sanifu  wa maabara  kwa  kuweka  orodha kwenye tovuti ya    www.pmoralg.go.tz.  Iliagizwa kuwa  waajiriwa    wapya walipaswa kuripoti katika Mamlaka za Serikali za Mitaa kuanzia tarehe 01 hadi 09 Mei, 2015.

Napenda  kuchukua nafasi hii kuutaarifu umma  kuwa ofisi yangu  ilipokea  na kuchambua  maombi ya  walimu ambao hawakuajiriwa awali;  na walioomba kubadilishiwa vituo kutokana na    matatizo mbalimbali.

 Vilevile ofisi  imezingatia kuwapanga tena  walimu ambao kwa sababu  za msingi  walishindwa kuripoti kufikia tarehe 09 Mei, 2015.  

Walimu wote waliopo katika orodha ya awamu ya pili wanapaswa kuripoti kuanzia tarehe  01 hadi 05 Juni, 2015  kwenye ofisi za Wakurugenzi wa Halmashauri kwa ajili ya kuajiriwa na kupangiwa vituo vya kazi.

Orodha ya walimu  hao watakaoajiriwa katika halmashauri husika  imegawanywa katika makundi yafuatayo:-

i.  walimu wa cheti (Daraja IIIA) waliokosa ajira kwa awamu ya kwanza;

ii.  walimu wa cheti (Daraja IIIA) waliobadilishiwa vituo;
iii.  walimu  wa  masomo ya sanaa  kwa ajili ya shule za sekondari  ambao hawakupangiwa vituo; 

iv.  walimu waliobadilishiwa vituo wa masomo ya sanaa  kwa ajili ya shule za sekondari; 

v.  walimu wa masomo ya sayansi na hisabati kwa ajili ya shule za sekondari ambao hawakupangiwa vituo; na

vi.  walimu  waliobadilishiwa vituo wa masomo ya sayansi na hisabati kwa ajili ya
shule za sekondari.

Utaratibu wa Ajira ya Walimu Awamu ya Pili
Kila mwajiriwa mpya anatakiwa kuzingatia yafuatayo:-i.  kuwasilisha vyeti halisi vya taaluma ya kuhitimu mafunzo  ya ualimu, elimu ya sekondari, cheti cha kuzaliwa pamoja na nakala zake; na

ii.  atalipwa  posho ya kujikimu kwa muda wa siku saba (7) na nauli ya usafiri wa magari (ground travel), malipo hayo yatatolewa na halmashauri husika.

Angalizo
i.  Walimu ambao wamekwisharipoti na mchakato wao wa ajira umeanza katika  Mamlaka za Serikali za Mitaa hawatahusika na mabadiliko  haya  hivyo waendelee kufanya kazi katika halmashauri husika na hawahusiki na upangaji wa awamu hii.

ii.  Walimu ambao walichelewa kuripoti tarehe 9 Mei, 2015 na majina yao hayajaonekana katika mabadiliko haya wanatakiwa waende kuajiriwa katika halmashauri walizopangwa awali (kwa kuzingatia orodha iliyotolewa kwenye tovuti tarehe 30/4/2015).  Aidha, walimu wa masomo ya sanaa ambao hawakuripoti katika Halmashauri za Wilaya za Meru na Arusha wamebadilishwa vituo.

iii.  Walimu waliopangwa ni wale wa masomo  ya sanaa/biashara na cheti waliohitimu mafunzo kwa mwaka wa masomo 2013/14 na wahitimu  wa miaka ya nyuma wa masomo ya sayansi na hisabati kwa ajili ya kufundisha katika shule za sekondari.

iv.  Kituo cha kazi cha mwalimu ni shule na sio Makao Makuu ya Halmashauri, posho italipwa baada ya mwalimu kuripoti na kuandika  barua kupitia kwa
Mkuu wa Shule.

v.  Mwalimu hatapokelewa na kuaajiriwa kama ikitokea yupo katika orodha na amehitimu shahada au stashahada zisizo za ualimu na wenye shahada za ualimu zisizo na somo au masomo ya kufundishia katika shule za sekondari.

vi.  Ikibainika kuna mwalimu atakayekwenda kuripoti na kuchukua posho na kuondoka, atachukuliwa hatua kwa mujibu wa Sheria.

Ni muhimu kuzingatia maelekezo haya, ikiwa ni pamoja na muda uliowekwa kuripoti kuepuka usumbufu unaoweza kujitokeza.

Limetolewa na
Ndg. Jumanne A. Sagini
KATIBU MKUU
OFISI YA WAZIRI MKUU-TAMISEMI 
______________










Thursday, May 21, 2015

ZIARA YA MBUNGE WA JIMBO LA KWIMBA KWA WANANCHI WAKE

Mbunge wa Kwimba Mansoor amepata mapokezi makubwa jimboni kwake.



Akiwa ameambatana na Katibu wa mkoa wa Mwanza Bw. Miraji Mtaturu, Mbunge huyo amekabidhi kadi 1600, mifuko ya saruji 600 yenye thamani ya shilingi milioni 12 na kuviwezesha vikundi mbalimbali zaidi ya shilingi milioni 5.

wanachama wapya

















MBUNGE MANSOOR, JIMBO LA KWIMBA LIMEBADILIKA NA KUPIGA HATUA YA 
MAENDELEO KWA VITENDO.

MBUNGE wa Jimbo la Kwimba, Shanif Mansoor,ametamba kuwa wananchi wa jimboni humo wajivune kwa kushirikiana nae kuleta maendeleo kwa vitendo na kulibadilisha badala ya kusikiliza uzushi wa baadhi ya wapinzani wake kisiasa wanaoendekeza ukabila.

Pia amekuwa akichangia miradi ya maendeleo ambapo metoa kiasi cha shilingi milioni 17 za kutekeleza ahadi zake za maendeleo na Ilani ya Uchaguzi ya CCM kwa vitendo katika Jimbo lake.

Mansoor alikabidhi saruji mifuko 600 katika Kata za Mhande, Fukalo, Ngudu na Bupamwa kwa ajili ya kusaidia ujenzi kwenye shule za msingi, zahanati na sekondari pamoja na kuchangia fedha na vifaa vya Kompyuta kwenye baadhi ya sekondari    na Chuo cha Afya cha Ngudu mjini.

Mbunge Mansoor akizungumza na mamia ya wananchi waliofurika kwenye mkutano wa hadhara juzi uliofanyika katika viwanja vya stendi mjini Ngudu, alisema kwamba saruji hiyo aliyoitoa katika Kata ya Bupamwa kwenye vijiji vya Dodoma, Kiliwi na itegamatwi kwa ujenzi wa vyumba vya madarasa shule za msingi.

Katika Kata ya Fukalo alitoa saruji katika vijiji vya Sanga, Msongwa, Chibuji kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule za msingi, Kata ya Mhande ni kijiji cha Gurumwa kwa ajili ya kusaidia pia ujenzi wa shule ya msingi na milioni tatu kwa maabara ya sekondari na Kata ya Ngudu mjini alitoa fedha kiasi cha shilingi milioni mbili sekondari ya Bujiku Sakila na shilingi milioni moja Ngudu mjini.

Maeneo mengine aliyochangia ni Chuo cha Afya Ngudu mjini shilingi milioni 2 kwa ajili ya ujenzi wa choo na kutoa Komputa tatu(sh. 1.8 mil), kuchangia saruji mifuko 50 kanisa la Romani (RC) na mifuko 50 kanisa la Afrika Iniland Charch Tanzania (AICT) katika kijiji cha Kilyaboya na kikundi cha ujasilimali Ngudu mjini kilipata shilingi laki tano.

Mansoor aliwaeleza wananchi kuwa katika fedha hizo za kuchangia maendeleo hazihusiani na Mfuko wa Jimbo la Kwimba bali kutokana na nguvu yake kwa lengo la kuwasaidia wananchi ili kupiga hatua ya maendeleo, ambapo al katika Kata ya Ngudu mjini alichangia saruji pia vijiji vya Gudula (shule) na Chamela (jengo la Kiliniki).

“Thamani ya saruji ambayo leo nimeitoa kusaidia wananchi katika vijiji hivyo ni shilingi milioni 12 na jumla ya fedha zilizokabidhiwa ni shilingi milioni tano tasilimu hivyo hapa misaada yote imegharimu kiasi shilingi milioni 17 jambo ambalo ni la kujivunia kwa wananchi kwa kuwa na Mbunge anayetambua maendeleo,”alisema.

Mansoor alitamba kuwa kwa kipindi chake cha uwakilishi kwa wananchi amefanya mambo makubwa kusimamia ikiwemo, usambazaji umeme vijijini katika Kata, kupigania maji safi kutoka chanzo cha Ziwa Victoria cha Ihelele, Shinyanga- Kahama ambayo huduma imefika na barabara ya Hungumalwa, Ngudu-Magu kwa kiwango cha lami ambayo tayari upembuzi yakinifu utaanza hivi karibuni.

Mbunge    huyo alitoa wito kwa wananchi wa Jimbo la Kwimba kumpatia ushirikiano kutekeleza yale aliyoahidi kwao na kutekeleza Ilani ya CCM kwa vitendo na kuwapuuza baadhi ya wanasiasa wachache walioanza kupitapita huku wakimchafua na kuanza kuhamasisha ukabila jambo ambalo alisema wananchi wanapashwa kutafakari na kuwataka wapinzani wake waeleze sela na hoja zitakazowashawishi kuwachagua.

chanzo: gsengo blog.


MTIA NIA MWINGINE JIMBO LA KWIMBA KUELEKEA UCHAGUZI MKUU MWAKA HUU



Heshima kwenu wakubwa,Mimi ni mtanzania mwenye akiri timamu {Aged 26 years old},bila kushurutishwa na mtu yeyote yule nimeamua kutangaza nia mapema kabisa ya kugombea ubunge jimbo la kwimba 2015.Nina degree ya falsafa na Elimu kutoka chuo kikuu cha mtakatifu Agustino Mwanza {SAUT}.Bachelor of philosophy with education.Nimetarajia kufanya mambo yafuatayo.

1. Kununua magari mawili kwa kutumia hera za mfuko wa jimbo ndani ya miaka miwili,Gari moja litabaki ngudu mjini na lingine litakuwa Mwamashimba.Kazi ya magari haya ni kama ifuatavyo:

A-   Kupeleka wagonjwa hospitarini wanaotoka vijiji vya mbali kama vile,Mahiga,Nyamilama,Bugembe, Mwang'haranga,shilaboya,mwadub i,jojiro pamoja na maeneo mengine.Vile vile na gari litakalokuwa Mwamashimba nalo litafanya kazi vilevile.

B-   Kusomba mchanga na mawe pamoja na shughuri zingine ili kutengeneza mfuko kwa ajiri ya kusomesha watoto yatima.

2. Kufanya mkakati wa kutengeneza barabara ya kutoka ngudu mjini kupitia jojiro hadi mabuki kwa kiwango cha lami,barabara ya kutoka mjini kupitia sumve hadi Magu kwa kiwango cha lami,barabara ya kutoka ngudu mjini kupitia mahiga,Nyamilama hadi Hungumalwa kwa kiwango cha lami.Nitashirikiana na atakaye kuwa mbunge wa maswa kufanya mpango wa kuitengeneza barabara ya kutoka Maswa kupitia,Shigumhulo,jojiro hadi mwabuki kwa kiwango cha Lami.

3.  Kufanya mkakati wa kuweka umeme kwenye center zote ambazo zitapitiwa na barabara ya lami kama vile Nyamilama,Lunele,Jojiro,Mwamas himba na maeneo mengine.
3.Kushugurikia suala la maji.Ni mengi sana ila naomba niishie hapo.

UFISADI ULIOFANYWA NA MBUNGE WA SASA WA KWIMBA (KAKA MANSOURI-CCM)

1.Kutumia hera ya mfuko wa jimbo milioni mia mbili na laki moja kwenye miladi yake.
2.Kuhamisha miladi ya barabara mbili za wilaya ya kwimba kwenda Bariadi zilizopaswa kutengenezwa kwa kiwago cha lami.
Haya ni machache tu,mengi yanakuja.

Ndugu wana wa Kwimba na watanzania kwa ujumla popote pale mlipo wenye mapenzi ya dhati kabisa na nchi yetu na mnaochukizwa na matumizi mambaya ya Raslimali zetu,pasipo kubagua dini pamoja na vyama nahitaji sana mchango wenu wa khari na mali ili niweze kufikia malengo yangu ya kuondoa matatizo ya jimbo la kwimba na Tanzania kwa ujumla.Kwa haya yote namtanguliza mwenyezi mungu katika Malengo yangu.Nasema hivi kwa sababu gani,umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu.Napenda sana changamoto pamoja na ushauri.

JINA.MARTIN WILBERT MANDAGO PHILLPO.
MAHARI.ILAMBA NGUDU-KWIMBA
UMRI - MIAKA 26
KABILA. MSUKUMA
CONTACT.PHONE NO.0765183733


Monday, May 11, 2015

Diwani CUF Mbaroni kwa Tuhuma za Kuomba na Kupokea Rushwa ya Sh 150,000 wilaya ya KWIMBA


DIWANI wa Kata ya Ngula wilayani Kwimba, Palu Mashagu (CUF), anashikiliwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kwa tuhuma za kuomba na kupokea rushwa ya Sh 150,000.

Taarifa kutoka Kwimba na kuthibitishwa jana na Kamanda wa Takukuru, Faustine Maijo, ilisema Mashagu alikamatwa Mei 6, mwaka huu mchana katika ofisi ya Mtendaji wa Kata ya Ngula akidaiwa kuomba na kupokea Sh 150,000 kutoka kwa mtumishi wa Halmashauri ya Kwimba, Nyabugumba Jonathan.

Mashagu ambaye pia ni Mwenyekiti wa CUF wilaya ya Kwimba anadaiwa kuomba na kupokea kiasi hicho cha fedha kwa ajili ya kumsaidia mtumishi huyo pamoja na wenzake wanne waliokuwa wakikabiliwa na tuhuma za ubadhirifu wa Sh milioni 72 za mradi wa usafi na mazingira.

Kutokana na tuhuma hizo kufika katika vikao vya Halmashauri ya Kwimba, kikao cha Baraza la Madiwani kiliazimia kufanya uchunguzi wa tuhuma hizo na kuunda kamati ya madiwani watano chini ya uenyekiti wa Diwani wa Nkalalo, Enos Ntwale, kuchunguza wizi wa fedha hizo kabla ya hatua nyingine dhidi ya wahusika kuchukuliwa.

Wajumbe wengine wa kamati hiyo ni Shija Malando (Kata ya Hungumalwa), Peter Msalaba (Kata ya Nyambiti), Tabu Samson (Viti Maalumu) na Mashagu.

Akizungumzia taarifa za diwani wake kutiwa mbaroni kwa kosa la rushwa, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kwimba, Zephania Masangu, alisema amepokea taarifa hizo lakini hajui undani wake na kubainisha alikuwa miongoni mwa wajumbe wa kamati yake aliyounda Aprili 29, mwaka huu.

“Kamati niliyounda ilishakamilisha kazi yake na taarifa kukabidhiwa sasa maelezo zaidi nadhani wanajua waliomkamata mngewauliza wao,”alisema Masangu.

Akizungumzia suala hilo mmoja wa wajumbe wa kamati hiyo aliyekataa jina lake kuandikwa  alidai taarifa walizopokea katika kamati yao zimedai Mashagu aliomba rushwa ya Sh 500,000 kwa Ofisa Afya Msaidizi aliyetoa taarifa Takukuru ndipo ukawekwa mtego na kumnasa akipokea Sh 150,000.


Chanzo:  mpekuzihuru
Previous Page Next Page Home