HALMASHAURI ya Wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza, inahitaji madawati 5,314 sawa na asilimia 15 kukamilisha agizo la Rais Dk John Magufuli ifikapo Julai 30 mwaka huu.
Kauli hiyo imetolewa
jana na Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Pendo Malebeja, wakati wa hafla fupi ya
kupokea msaada wa madawati 60 yenye thamani ya Sh milioni 5 iliyofanyika shule
ya msingi Kakora Kata ya Ngudu Mjini, kutoka kwa uongozi wa Benki ya CRDB tawi
la Nyerere jijini Mwanza ikiwa ni kuunga jitiada za serikali ya awamu ya tano
katika kuboresha miundombinu ya elimu nchini.
Malebeja alisema
kwamba hadi juzi Halmashauri ilikuwa imetengeneza na kukarabati jumla ya
madawati 30,006 sawa na asilimi 85 ambapo mahitaji halisi ni madawati 35,000
hivyo upungufu uliopo ni 5,314 sawa na asilimia 15 baada ya kupokea madawati 60
kutoka kwa wadau Benki ya CRDB upungufu sasa ni 5,254.
Akizungumza wakati wa
kukabidhi msaada huo, Meneja wa CRDB tawi la Nyerere, Naomi Mwamfupe, alisema
kwamba wao wanaunga mkono juhudi za serikali za kuboresha miundombinu ya Elimu,
Afya, Mazingira, pamoja na kusaidi yanapotokea maafa na majanga lengo ikiwa ni kuleta
usitawi wa jamii na kukuza uchumi.
“Tumewezesha wanafunzi
120 kukaa kwenye madawati baada ya wananchi wa Wilayah ii nao kujitokeza na
kuchangia madawati kwa kushirikiana na serikali kwa asilimia 85 hivyo kwa
mafanikio ya miaka 20 ya Benki ya CRDB nchini tunaunga mkono juhudi za Rais Dk
Magufuli kuboresha miundombinu katika Sekta zote za utoaji huduma kuwa rafiki
kwa wananchi,”alisema.
Mwamfupe alimtaka
Mkurugenzi Malebeja na Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Peter Ngassa (CCM),
kufikisha ushauri kwenye Kikao cha Baraza la madiwani ili kuangalia uwezekano
wa kufungua Akaunti katika tawi la benki hiyo lililopo ofisi za Halmashauri
hiyo ili kuwapa fursa wadau mbalimbali na wananchi kujitokeza kwa hiali
kuchangia maendeleo ikiwemo madawati.
Kwa upande wake mgeni
rasmi aliyemuwakirisha Mkuu wa Wilaya hiyo, Katibu Tawala wa Wilaya (DAS),
Andreaw Ng’hwani, alipongeza uongozi wa Benki hiyo tawi la Nyerere kwa
kujitokeza kusaidia madawati ili kuwezesha Halmashauri kufikia lengo kwa
asilimia 100 kama ilivyoagizwa na Rais Dk Magufuli nhini kote.
Chanzo: GSENGO BLOG
Best online baccarat - FEBCasino
ReplyDeleteBest online baccarat. Learn about the rules, rules, strategy, and how kadangpintar to play. 바카라 사이트 Find the most popular หาเงินออนไลน์ games on our site!