Mbunge wa jimbo la Sumve, Richard Ndasa akiweka shada la maua |
Bi. Winfrida Senga akiweka shada la maua kwenye Kaburi la Mumewe, wakati wa mazishi yaliyofanyika kwenye Makaburi ya Kijijini kwao, Shushu Kwimba, Jijini Mwanza. |
Senga (58) aliyefariki dunia Julai 27
mwaka huu nchini India, alizikwa nyumbani kwao katika Kijiji cha Shushi
wilayani Kwimba.
Maziko hayo yaliongozwa na Kiongozi wa
Kambi rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe ambaye pia mwenyekiti wa
Chadema. Pia alikuwapo Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Vincent Mashinji
na mamia ya waombolezaji.
Akizungumza katika maziko hayo, Mbowe
alimuelezea Senga kuwa ni shujaa wa mapambano ya kupigania haki na demokrasia
ya kweli nchini.
Alisema kazi za Senga
aliyoiacha hapa duniani ni kielelezo thabiti cha uwajibikaji usioogopa vitisho.
“Senga alikuwa mfanyakazi na mtumishi
mwenzetu. Senga hakuwa baraka kwa wana Kwimba pekee, bali alikuwa mtu wa wote.
Nimefanya kazi naye kwa zaidi ya miaka 16. Tumezunguka naye kila eneo ndani ya
nchi hii. Hakuna operesheni ya Chadema tuliyomuacha Senga,” alisema
Mbowe.
Vilevile, alisimulia mazingira tatanishi
yaliyosababisha kifo cha aliyekuwa mwandishi wa habari wa Kituo cha Channel Ten
mkoani Iringa, Daud Mwangosi.
Mbowe aliyetumia dakika 20
kumzungumzia marehemu Senga, alisema usingekuwa ujasiri wake kupiga picha za
tukio la kifo cha Mwangosi, dunia isingefahamu polisi ndiyo waliohusika
na mauaji hayo.
Senga ameacha mke mmoja na watoto saba,
kati yao wanne wa kike na watatu wa kiume.
Mungu ailaze mahala pema peponi, roho ya
marehemu, Joseph Senga.
Chanzo: MTANZANIA
No comments:
Post a Comment