Utawala wa Kijiji ni miongoni mwa tawala katika serikali za mitaa za Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania. Huu ni utawala wa chini
kabisa kimuundo ukitanguliwa na utawala wa Kitongoji. Kuwa utawala wa chini haimaanishi kuwa na umuhimu
mdogo, isipokuwa ni kupitia utawala huu ndiko ambako mambo mengi yanayoamuriwa
au kupangwa na tawala za juu kama serikali, hutekelezwa. Utawala wa kijiji
huelekeza wananchi katika kutumia madaraka yao ya kidemokrasia kuamua juu ya
mambo yanayowahusu kama wanakijiji moja kwa moja bila kupitia mlolongo au urasimu mrefu. Mambo yanayohusiana na tawala za serikali za
mitaa yanaratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu.
Mkutano Mkuu wa Kijiji ni chombo cha utawala kinachoundwa na
wajumbe wafuatao:
·
Wakazi
wote wa Kijiji wenye umri usiopungua miaka 18 na wenye akili timamu.
·
Mwenyekiti
wa Kijiji.
·
Wenyeviti
wa Vitongoji vyote kijijini.
·
Wajumbe
wa Halmashauri ya Kijiji ambao ni kati ya 15 na 25.
·
Afsa
Mtendaji wa Kijiji – Katibu.
Kwa mujibu wa kifungu cha 103 (2)
cha sheria namba 7 ya mwaka 1982. Mkutano Mkuu wa Kijiji huitishwa mara mmoja
kila baada ya miezi mitatu.
Kwa mujibu wa kifungu cha 141 cha
sheria namba 7 ya mwaka 1982, Mkutano Mkuu ndiyo Mamlaka yenye madaraka ya juu
kabisa kuhusu maamuzi yote ya sera na maendeleo kijijini na ndiyo yenye wajibu
wa kuwachagua na kuwaondoa madarakani wajumbe wa Halmashauri ya Kijiji ikiwa ni
pamoja na kutekeleza majukumu mbalimbali iliyopewa kwa mujibu wa sheria hii na
nyingine.
Kila baada ya miaka mitano kinakuwa na Mkutano
Mkuu Maalum
wa uchaguzi wa Mwenyekiti na wajumbe wa halmshauri ya
Kijiji.
Mkazi wa kijiji anayegombea nafasi ya uongozi kwenye halmashauri ya kijiji au
uenyekiti wa kijiji lazima awe na umri usiopungua miaka 21. Mwenyekiti wa Mkutano Mkuu
ni Mwenyekiti
wa kijiji akisaidiwa
na Afisa
Mtendaji wa Kijiji(VEO).
Mwenyekiti na Afisa Mtendaji wa Kijiji (VEO) hupanga ratiba za vikao, kuandaa
na kuitisha vikao vya Mkutano Mkuu wa Kijiji.
Muundo wa Halmashauri ya Kijiji
Halmshauri
ya kijiji ni
chombo kikuu cha utendaji katika utawala wa kijiji. Hukutana mara moja kila
mwezi, mikutano ya dharura inaweza kuitishwa. Akidi (qorum) ya vikao vya
halmshauri ya kijiji ni nusu ya wajumbe wote wa halmashauri ya kijiji. Wakati
Mkutano Mkuu ni kama Bunge, halmshauri ya kijiji ni kama serikali. Huchaguliwa na Mkutano
Mkuu wa Kijiji.
Uchaguzi wa halmashauri wa kijiji husimamiwa na Mkurugenzi wa halmshauri ya Wilaya. Mkazi wa kijiji mwenye umri
usiopungua miaka 21 ana sifa za kuchaguliwa kwenye halmshauri ya kijiji.
Wajumbe wa halmashauri ya kijiji wanatakiwa wasizidi 25 na wasiopungua 15.
Mkutano Mkuu kwa kushirikiana na Msimamizi wa uchaguzi idadi ya wajumbe
wanayotaka kutokana na mazingira yao kutegemea na wingi wa wakazi na ukubwa wa eneo lao
(idadi ya vitongoji). Wajumbe wa halmashauri ya kijiji
ni Mwenyekiti wa kijiji, wenyeviti wa vitongoji, wanawake ambao watakuwa theluthi moja ya wajumbe wote na
wajumbe wengine. Mwenyekiti wa kijiji ni mwenyekiti wa halmshauri ya kijiji na
mwenyekiti wa Mkutano Mkuu. Wenyeviti wa vitongoji huchaguliwa na wakazi wa
vitongoji huingia kwenye halmashauri ya kijiji kwa mujibu wa nyadhifa zao.
Wajibu na Majukumu ya Mkutano Mkuu wa Kijiji
·
Kupokea
na kujadili taarifa za utekelezaji wa shughuli mbalimbali.
·
Kupokea
na kujadili mapato na matumizi ya fedha.
·
Kupokea
na kujadili taarifa za makusanyo ya fedha yakiwamo ya ushuru, ada na mapato
mengine
yanayopaswa kukusanywa ndani ya kijiji kwa mujibu wa sheria
·
Kupokea
na kujadili taarifa za watu walioomba kupewa ardhi.
·
Kupokea
na kujadili mapendekezo yatakayotolewa na Halmashauri ya Kijiji au Kitongoji.
·
Kupokea
maagizo (kama yapo) kutoka ngazi za juu za Serikali na kuweka mkakati wa
utekelezaji.
·
Kufanya
maamuzi yanayozingatia demokrasia.
·
Kuchagua
Mwenyekiti na Wajumbe wa Halmashauri ya Kijiji.
·
Kujadili
na kupitisha bajeti na mipango ya maendeleo ya Kijiji.
·
Kuidhinisha
utungwaji wa sheria ndogo kabla ya kupelekwa kwenye Halmashauri ya wilaya kwa
ajili ya kupitishwa kwa manufaa ya kijiji.
·
Kufanya
maamuzi yanayozingatia demokrasia.
·
Kujadili
na kupitisha bajeti na mipango ya maendeleo ya Kijiji.
·
Kupitisha azimio la kukaripia rasmi mjumbe
yoyote wa halmashauri au halmashauri kwa ujumla kwa utendaji mbovu
Kazi za Mwenyekiti wa Kitongoji
·
Kutunza
rejesta ya wakazi wa kitongoji na nyaraka nyingine muhimu zinazohusu maendeleo
ya kitongoji kwa jumla ikiwa ni pamoja na kumbukumbu za vizazi na vifo.
·
Kusimamia
shughuli za ulinzi na usalama wa watu na mali zao waishio katika eneo lote la
kitongoji.
·
Kuhamasisha
ulipaji wa kodi na ushuru mbalimbali, kama utakavyoamuliwa na kuwekwa mara kwa
mara na Halmashauri ya Kijiji na Wilaya. Jukumu hilo pia linatekelezwa na
Mwenyekiti wa kitongoji kilicho kwenye eneo la Mji, Manispaa au Jiji.
·
Kusimamia
katika eneo lake suala zima la Hifadhi ya mazingira hususan vyanzo vya maji
n.k.
·
Kusimamia
suala la afya katika eneo lake ikiwa ni pamoja na utekelezaji wa kampeni za
afya za Kitaifa, Kimkoa au Kiwilaya dhidi ya magonjwa ya kuambukiza, na hasa,
vita dhidi ya UKIMWI.
·
Kufuatilia
hali ya lishe na uchumi wa wakazi wa kitongoji.
·
Kufuatilia
na kuhakikisha kuwa kila mtoto mwenye umri wa kwenda shule anapatiwa nafasi na
kushirikiana na viongozi wa shule katika udhbiti utoro shuleni.
·
Kuhamasisha
elimu ya watu wazima.
·
Kusimamia
na kuwahamasisha wakazi wa kitongoji katika kutekeleza shughuli za kujitegemea.
·
Kusuluhisha
migogoro midogo midogo isiyostahili kushughulikiwa na Mabaraza ya Kata au
Mahakama.
·
Kuwakilisha
kitongoji katika Serikali ya Kijiji.
·
Kuwaongoza
na kuwahamasisha wakazi wa kitongoji washiriki katika sherehe za Taifa na
mikutano ya hadhara itakayoandaliwa na kuitwa na Serikali au Halmashauri.
·
Kutekeleza
kazi nyingine atakazopangiwa na Halmashauri ya Kijiji na Wilaya. Jukumu hili
pia linatekelezwa kwa vitongoji vilivyo kwenye Halmashauri za Miji, Manispaa au
Jiji
·
Kufanya
maamuzi yanayozingatia demokrasia.
·
Kuchagua
Mwenyekiti na Wajumbe wa Halmashauri ya Kijiji.
·
Kujadili
na kupitisha bajeti na mipango ya maendeleo ya Kijiji.
·
Kuidhinisha
utungwaji wa sheria ndogo kabla ya kupelekwa kwenye Halmashauri ya wilaya kwa
ajili ya kupitishwa kwa manufaa ya kijiji.
Mamlaka na Majukumu ya Halmashauri
ya Kijiji
- Kutafakari maamuzi, mapendekezo
na maazimio ya mkutano Mkuu wa kijiji na kubuni mbinu na njia za
kutekeleza.
- Wajumbe wa halmshauri wenyewe
wakiwa hawaridhiki kabisa na utendaji wa Mwenyekiti wa kijiji wana haki ya
kumwondoa kwa kura theluthi mbili ya wajumbe wote na kuitisha Mkutano Mkuu
wa kijiji ili kuchagua mwenyekiti mwingine.
- Kupokea taarifa za mikutano ya
vitongoji na kamati zake
kufanyia kazi na kupeleka Mkutano Mkuu wa kijiji.
- Kupokea, kutafakari na kufanyia
kazi maagizo na mapendekezo kutoka kamati ya maendeleo ya kata (WDC) na halmshari ya wilaya.
- Kubuni na kuendekeza sera na
mwelekeo wa kijiji kwa mkutano mkuu wa kijiji.
- Kuandaa na kupendekeza mipango ya maendeleo ya
muda mrefu kwa Mkutano Mkuu wa kijiji.
- Kutunga sheria ndogondogo kwa
kushauriana na Mkutano Mkuu wa kijiji.
- Kuwaalika wataalamu panapokuwa
na haja ya kufanya hivyo ila hawatakuwa na haki ya kupiga kura.
- Kupokea, kutafakari na
kupendekeza kwa Mkutano Mkuu wa kijiji maombi ya ugawaji wa ardhi zaidi
ya ekari 100
hadi 500 rasilimali zingine
kwa maamuzi.
- Kupokea, kutafakari na
kuamua ugawaji wa ardhi chini
ya ekari 100.
- Kutoa taarifa za utendaji kwa
Mkutano Mkuu wa Kijiji.
- Kumiliki mali na kuingia
mikataba kwa niaba ya kijiji.
Ushiriki wa wananchi ni jambo la msingi sana katika
kujiletea maendeleo yao katika vijiji na mitaa. Mahali ambapo wananchi hawashiri
wala hawashirikishwi kunakuwa na lawamana mizozo mingi kwa viongozi hasa pale
ambapo maamuzi yaliyopitishwa yanawaumiza wananchi. Hapa ndipo wengi huona
umuhimu wa kushiriki unapojitokeza zaidi.
No comments:
Post a Comment