Thursday, July 14, 2016

TCU WAMETANGAZA MABADILIKO YA TARATIBU,VIGEZO NA SIFA ZA KUJIUNGA CHUO KIKUU MWAKA WA MASOMO 2016/2017



































FORM SIX LAZIMA UWE NA TWO PRINCIPAL PASSES (YAANI D MBILI KATIKA COMBINATION YAKO) BADALA YA E MBILI KAMA ILIVYOKUWA AWALI*
*EQUIVALENT APPLICANTS (DIPLOMA) LAZIMA UWE NA GPA 3.5 KUENDELEA,AU WASTANI WA B KWENYE MASOMO YAKO KWA DIPLOMA YA ELIMU NA AFYA,AU UPPER SECOND CLASS FOR DIPLOMA*
*PRENTRY COURSE ZOTE KWA WANAFUNZI WALIOKUWA HAWANA SIFA KUJIUNGA NA CHUO KIKUU ZIMESIMAMISHWA

SOMA VIGEZO VYOTE>>> HAPA


Thursday, July 7, 2016

UTEUZI WA WAKURUGENZI, PENDO MALABEJA ABAKIZWA KWIMBA.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 07 Julai, 2016 amefanya uteuzi wa wakurugenzi wa halmashauri za majiji 5, Manispaa 21, Miji 22 na Wilaya (DC) 137 za Tanzania Bara.
Uteuzi huo umetangazwa na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhandisi Mussa Iyombe ambapo kati ya wakurugenzi wote 185 walioteuliwa, 65 wameteuliwa kutoka orodha ya wakurugenzi wa zamani na 120 ni wakurugenzi wapya.
Orodha ya wakurugenzi walioteuliwa kulingana na mikoa yao ni kama ifuatavyo;
ARUSHA
1.     Arusha Jiji                              -           Athumani Juma Kihamia
2.     Arusha DC                            -           Dkt. Wilson Mahera Charles
3.     Karatu DC                             -           Banda Kamwande Sonoko
4.     Longido DC                          -           Jumaa Mohamed Mhiwapijei
5.     Meru DC                               -           Kazeri Christopher Japhet
6.     Monduli DC                         -           Stephen Anderson Ulaya
7.     Ngorongoro DC                   -           Raphael John Siumbu

DAR ES SALAAM
1.     Dar es salaam Jiji                  -           Siporah Jonathan Liana
2.     Kinondoni Manispaa           -           Aron Titus Kagurumjuli
3.     Temeke Manispaa               -           Nassibu Bakari Mmbaga
4.     Ilala Manispaa                      -           Msongela Nitu Palela
5.     Kigamboni Manispaa           -           Stephen Edward Katemba
6.     Ubungo Manispaa               -           Kayombo Lipesi John
DODOMA
1.     Dodoma Manispaa              -           Dkt. Leonard M. Masale
2.     Kondoa DC                          -           Kibasa Falesy Mohamed
3.     Kondoa Mji                           -           Khalifa Kondo Mponda
4.     Mpwapwa DC                       -           Mohamed Ahamed Maje
5.     Kongwa DC                           -           Mhandisi Ngusa Laurent Izengo
6.     Chemba DC                          -           Semistatus Hussein Mashimba
7.     Chamwino DC                      -           Athuman Hamis Masasi
8.     Bahi DC                                -           Rachel Marcel Chuwa

Tuesday, July 5, 2016

Maagizo ya RC Mongella kwa wakuu wa wilaya wapya mkoa wa Mwanza


Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella, amewaapisha wakuu wapya wa Wilaya za Mkoa wa Mwanza na kuwapa vitendea kazi ikiwapo katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania na Ilani ya Chama Tawala Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya Mwaka 2015- 2020, kwaajili ya kwenda kutimiza wajibu wao wa kikatiba kwenye wilaya walizo pangiwa.

Akizungumza baada yakuwaapisha, Mhe. Mongella, amewataka waende wakasimamie shughuli za kuhimiza maendeleo, suala la ulinzi na usalama kwenye wilaya zao, huku akitilia mkazo ukomeshwaji wa mauwaji ya watu wenye ulemavu wa Ngozi albino pamoja na Vikongwe. Amesema, ikiwa jamii ya watu hao itapata madhara basi ni dhahiri Mkuu huyo wa Wilaya atakuwa ameshindwa kusimamia majukumu yake.

Mkuu huyo wa mkoa pia, amerudia kauli yake nakuwataka viongozi hao wapya watambue wanajukumu zito lililoko mbele yao, ikiwa ni pamoja na kukomesha Utumiaji wa dawa zakulevya.

Aidha ameonya uchezaji wa Pool na unywaji wa Pombe wakati wa saa kazi, huku akimsisitiza mkuu wa Wilaya ya Nyamagana kuhakikisha ifikapo Agosti mosi, suala la wafanyabiashara wanaofanya biashara kwenye maeneo ambayo hayaruhusiwi liwe limepatiwa ufumbuzi.

Mongella amesema, katika mkoa wa Mwanza, Hotel na Clabu, yeyote ile, iwe ya kawaida au ya Kitalii, ikibainika inafanya biashara ya Shisha, hawataivumilia na badala yake wataifutia Leseni ya biashara.

Walio apa mbele ya Mkuu wa Mkoa, ambao waliteuliwa na Mhe. Rais Tarehe 26, Juni, 2016 ni Emmanuel Enock Kipole, Mkuu wa Wilaya ya Sengerema, Estomin Francis Chang’a Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe, Hadija Rashid Nyembo Mkuu wa Wilaya ya Magu, wengine ni Juma Samwel Sweda Mkuu wa Wilaya ya Misungwi, Dkt. Leonard Moses Masale Mkuu wa Wilaya ya Ilemela, Mary Onesmo Tesha Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana na Mhandisi Mtemi Msafiri Simioni Mkuu wa Wilaya ya Kwimba.

Imetolewa na
Atley J. Kuni
Afisa habari na Mahusiano
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa.
MWANZA.
04, Julai, 2016.


Previous Page Next Page Home