Friday, June 26, 2015

HOTUBA YA KAIMU KATIBU MTENDAJI WA BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI (NACTE) KUHUSU TAMKO LA BARAZA LA KUVIFUTIA USAJILI BAADHI YA VYUO NA KUVISHUSHA HADHI VINGINE



Ndugu waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari, ninayo furaha kubwa kuwakaribisha katika ofisi za Baraza. Lengo la kuwaita hapa leo ni kuwapa taarifa juu ya maamuzi yaliyofikiwa na Baraza ikiwa ni katika jitihada za kuinua ubora wa elimu ya ufundi nchini.

Ndugu Waandishi wa Habari

Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi ni chombo kilichoanzishwa kwa Sheria ya Bunge Sura ya 129, kwa lengo la kusimamia na kuratibu taaluma zinazotolewa na taasisi na vyuo vva elimu ya ufundi nchini, ambavyo siyo vyuo vikuu au vyuo vikuu vishiriki. Jukumu kubwa la Baraza ni kuendeleza na kuinua ubora wa elimu ya ufundi nchini kwa kusimamia kikamilifu shughuli za kuendesha mafunzo ili tuzo zinazotolewa na taasisi na vyuo ziwe na ubora unaokubalika kitaifa na kimataifa.

Kwa kutumia Sheria na Kanuni za Baraza za Usajili (2001) na zile za Ithibati na Utambuzi (2001), mnamo tarehe 20 Februari 2015, Baraza lilitoa notisi ya siku 30 kwa taasisi na vyuo vilivyokiuka taratibu na vyenye mapungufu makubwa ya Usajili na Ithibati kupitia taarifa yake kwa Umma. Notisi hii ililenga kuzipa taasisi na vyuo nafasi ya kujirekebisha. 

Baraza linakiri kuwa taasisi na vyuo vingi kama vilivyoorodheshwa kwenye Jedwali Na. 1, Jedwali Na. 3, na baadhi kwenye Jedwali Na. 5 vimechukua hatua mbalimbali za kurekebisha mapungufu yaliyojitokeza. Hata hivyo, hadi kufikia leo tarehe 24 Juni 2015 yaani siku 124 baada ya Notisi ya Baraza, kuna vyuo ambavyo havijachukua hatua yoyote ya kurekebisha mapungufu yake kama inavyooneshwa kwenye Jedwali Na. 2 na Jedwali Na. 4.

Tamko la Baraza

Kutokana na mapungufu hayo Baraza limeamua kuchukua hatua kwa mujibu wa Sheria na Kanuni zake kwa taasisi na vyuo vyote vilivyoorodheshwa katika Jedwali Na. 2 na Jedwali Na. 4 kwa makosa yafuatayo:

a)    Ama kumalizika kwa muda wa  Usajili wa Awali (Preparatory Registration) na Usajili wa Muda (Provisional Registration); au
b)    Kutoanza mchakato wa kupata Ithibati baada ya kupata Usajili Kamili; au
c)    Kumalizika kwa muda wa Ithibati na kutochukua hatua ya kuomba upya Ithibati (re-affirmation); na
d)    Taasisi na Vyuo kuamua vyenyewe kusitisha kutoa mafunzo kwa sababu mbalimbali.

        
Jedwali Na. 1: Taasisi  na Vyuo vinavyoruhusiwa kuendelea na taratibu za Usajili baada ya kutimiza masharti

Na
Jina la Chuo/Taasisi
Namba ya Usajili
1
Regional Aviation College – Dar es Salaam
REG/EOS/028P
2
Zoom Polytechnic College – Dar es Salaam
REG/EOS/030P
3
Gataraye Research and Training Centre – Dar es Salaam
REG/EOS/034P
4
Modern Commercial Institute (MCI) – Dar es Salaam
REG/BMG/024P
5
Evin School of Management – Dar es Salaam
REG/BMG/026P
6
Agape School of Management – Dar es Salaam
REG/BMG/027P


Jedwali Na. 2: Taasisi  na Vyuo vilivyofutiwa Usajili na kuzuiliwa kudahili wanafunzi wapya baada ya kutotimiza masharti ya Usajili

Na.
Jina la Chuo/Taasisi
Namba ya Usajili/Maelezo
1
Dar es Salaam College of Clinical Medicine – Kinondoni
Usajili wa Awali
2
Ndatele School of Medical Laboratory Sciences – Dar-es-Salaam
Usajili wa Awali
3
Institute for Information Technology – Dar es Salaam  
REG/EOS/014
4
DARMIKI College of Educational Studies
Hakijasajiliwa. Kimezuiliwa kudahili wanafunzi

Jedwali Na. 3: Taasisi  na Vyuo vinavyoruhusiwa kuendelea na taratibu za Ithibati baada ya kutimiza masharti

Na.
Jina la Taasisi/Chuo
Namba ya
Usajili
Hadhi Kabla ya
Notisi
Hadhi Baada ya
Notisi
1
Mabughai Community Development Technical Training Institute – Lushoto
REG/EOS/040
Usajili Kamili
Usajili Kamili
2
Kizimbani Agricultural Training Institute - Zanzibar
REG/ANE/027
Usajili Kamili
Ithibati ya Awali
3
Civil Aviation Training Centre – Dar es Salaam
REG/EOS/006
Ithibati ya Muda
Ithibati ya Muda
4
Ardhi Institute – Tabora
REG/EOS/010
Ithibati ya Muda
Ithibati Kamili
5
Bandari College – Dar es Salaam
REG/EOS/018
Ithibati ya Awali
Ithibati ya Awali
6
Tanzania Institute of Rail Technology – Tabora
REG/EOS/012
Ithibati ya Awali
Ithibati ya Awali
7
RETCO Business College (RBC) – Iringa
REG/BMG/025
Usajili Kamili
Usajili Kamili
8
Aseki Business School – Dodoma
REG/BMG/030
Usajili Kamili
Usajili Kamili
9
Western Tanganyika College – Kigoma
REG/BMG/032
Usajili Kamili
Usajili Kamili
10
Law School of Tanzania
REG/BMG/040
Usajili Kamili
Usajili Kamili
11
Royal College of Tanzania  (RCT) – Dar es Salaam
REG/PWF/004
Ithibati ya Awali
Ithibati ya Awali
12
Tanzania Regional  Immigration Training Academy  (TRITA) – Moshi
REG/PWF/030
Ithibati ya Awali
Ithibati ya Awali
13
Morogoro School of Journalism (MSJ) – Morogoro
REG/PWF/005
Ithibati ya Muda
Ithibati ya Muda
14
Taasisi ya Sanaa na Utamaduni (TaSUBa) – Bagamoyo (former Bagamoyo College of Arts – Bagamoyo)
REG/PWF/010            
Ithibati Kamili
Ithibati Kamili
15
Newman Institute of Social Work (NISW) – Kigoma
REG/PWF/016
Ithibati Kamili
Ithibati Kamili
16
Njuweni Institute of Hotel, Catering & Tourism Management - Kibaha
REG/ANE/016
Ithibati ya Awali
Ithibati ya Awali
17
Geita School of Nursing – Geita
REG/HAS/079
Ithibati ya Awali
Ithibati ya Awali
18
St. Gaspar Nursing School – Itigi
REG/HAS/090
Usajili Kamili
Usajili Kamili
19
Bugando School of Nursing – Mwanza
REG/HAS/052
Ithibati ya Awali
Ithibati ya Awali
20
COTC Mafinga – Iringa
REG/HAS/047
Ithibati ya Awali
Ithibati ya Awali
21
Kagemu School of Environmental Health  Sciences – Bukoba
REG/HAS/034
Ithibati ya Awali
Ithibati ya Awali
22
Mvumi Institute of Health Sciences – Dodoma
REG/HAS/011
Ithibati ya Awali
Ithibati ya Awali
23
Tanzania Training Centre for International Health – Ifakara
REG/HAS/003
Ithibati ya Muda
Ithibati ya Muda
24
Mbeya Polytechnic College (former Ilemi Polytechnic College) – Mbeya
REG/BMG/031
Usajili Kamili
Usajili Kamili
25
Institute of Sports Development Malya - Mwanza
REG/PWF/019
Usajili Kamili
Usajili Kamili
26
Ruaha Community Development Training Institute (CDTI) - Iringa
REG/PWF/028
Usajili Kamili
Usajili Kamili
27
Uyole Community Development Training Institute (CDTI) - Mbeya
REG/PWF/027
Usajili Kamili
Usajili Kamili
28
Institute of Rural Development Planning (IRDP) - Mwanza
REG/PWF/043
Usajili Kamili
Usajili Kamili
29
Rungemba Community Development Institute (CDTI) - Mufindi
REG/PWF/007
Ithibati Kamili
Ithibati Kamili
30
Time School of Journalism (TSJ) – Dar es Salaam
REG/PWF/013
Ithibati Kamili
Ithibati Kamili
31
COTC Machame – Hai
REG/HAS/087
Usajili Kamili
Usajili Kamili
32
Mwambani School of Nursing – Chunya
REG/HAS/089
Usajili Kamili
Usajili Kamili
33
Kiomboi School of Nursing – Iramba
REG/HAS/091
Usajili Kamili
Usajili Kamili
34
College of Health Sciences Zanzibar
REG/HAS/095
Usajili Kamili
Usajili Kamili
35
Kabanga School of Nursing – Kasulu
REG/HAS/023
Usajili Kamili
Ithibati ya Awali
36
Kondoa School of Nursing – Dodoma
REG/HAS/040
Ithibati ya Awali
Ithibati ya Awali
37
Lugarawa School of Nursing  – Ludewa  
REG/HAS/036
Ithibati ya Awali
Ithibati ya Awali
38
Tosamaganga School of Nursing  – Iringa
REG/HAS/020
Ithibati ya Awali
Ithibati ya Awali
39
Vector Control training Centre – Muheza
REG/HAS/031
Ithibati ya Muda
Ithibati ya Muda
40
Training Centre for Health Records Technology – Moshi
REG/HAS/072
Ithibati ya Muda
Ithibati ya Muda
41
Dar es Salaam School of Journalism (DSJ) – Dar es Salaam
REG/PWF/012
Ithibati Kamili
Ithibati Kamili
42
Financial Training Centre – Dar es Salaam
REG/BMG/004
Ithibati ya Awali
Ithibati ya Awali


Jedwali Na. 4: Taasisi  na Vyuo vilivyoshushwa hadhi baada ya kutotimiza masharti ya Ithibati

Na.
Jina la Taasisi/Chuo
Namba ya
Usajili
Hadhi Kabla ya
Notisi
Hadhi Baada ya
Notisi
1
Sura Technologies – Dar es Salaam
REG/EOS/019
Usajili Kamili
Usajili wa Muda
2
Institute of Management and Information Technology – Dar es Salaam
REG/EOS/016
Ithibati ya Awali
Usajili wa Muda
3
Techno Brain - Dar es Salaam
REG/EOS/021
Ithibati ya Awali
Usajili wa Muda
4
Ministry of Agriculture Training Institute Igurusi - Mbeya
REG/ANE/009
Ithibati ya Awali
Usajili wa Muda
5
Mbozi School of Nursing – Mbeya
REG/HAS/062
Usajili Kamili
Usajili wa Muda
6
KCMC AMO Ophthalmology School – Moshi
REG/HAS/085
Usajili Kamili
Usajili wa Muda
7
KCMC AMO Anaesthesia School – Moshi
REG/HAS/094
Usajili Kamili
Usajili wa Muda
8
Advanced Pediatrics Nursing KCMC - Moshi
REG/HAS/076
Ithibati ya Awali
Usajili wa Muda
9
AMO Training Centre Tanga – Tanga
REG/HAS/049
Ithibati ya Awali
Usajili wa Muda
10
CATC – Songea
REG/HAS/054
Ithibati ya Awali
Usajili wa Muda
11
CATC – Sumbawanga
REG/HAS/055
Ithibati ya Awali
Usajili wa Muda
12
COTC Maswa – Shinyanga
REG/HAS/014
Ithibati ya Awali
Usajili wa Muda
13
COTC – Musoma
REG/HAS/033
Ithibati ya Awali
Usajili wa Muda
14
Dental Therapists Training Centre – Tanga
REG/HAS/057
Ithibati ya Awali
Usajili wa Muda
15
Ngudu School of Environmental Health Sciences – Kwimba
REG/HAS/058
Ithibati ya Awali
Usajili wa Muda
16
KCMC AMO General School – Moshi
REG/HAS/096
Ithibati ya Muda
Usajili Kamili


Jedwali Na. 5: Taarifa kuhusu Taasisi  na Vyuo vyenye maelezo maalum

Na.
Jina la Taasisi/Chuo
Namba ya
Usajili
Hadhi Kabla ya
Notisi
Hadhi Baada ya
Notisi
Maelezo
1
Lake Teachers College – Singida
REG/TLF/001
Usajili wa Muda
Usajili Kamili
Kimeruhusiwa kudahili wanafunzi
2
Patricia Metzger Academy of Health and Beauty – Dar-es-Salaam
REG/PWF/022P
Usajili wa Muda
Usajili wa Muda
Kimesitisha kutoa mafunzo
3
Institute of Management and Entrepreneurship Development – Dar es Salaam
REG/BMG/039
Usajili Kamili
Usajili Kamili
Kimesitisha kutoa mafunzo
4
Tanga School of Nursing – Tanga
REG/HAS/084
Ithibati Kamili
Ithibati Kamili
Haijamaliza muda wa Ithibati
5
ESACS School of Journalism and Business Studies – Dar es Salaam
REG/PWF/044
Usajili Kamili
Usajili Kamili
Kimesitisha kutoa mafunzo
6
Fire and Rescue Training Centre – Dar es Salaam.
REG/EOS/032P
Usajili wa Muda
Usajili wa Muda
Kimesitisha kutoa kozi za muda mrefu. Sasa kinatoa kozi za muda mfupi ambazo hazipitishwi na Baraza (NACTE).

Asanteni kwa kunisikiliza.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA KATIBU MTENDAJI
BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI




No comments:

Post a Comment

Previous Page Next Page Home