TAARIFA KWA UMMA
Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai (Mb) amefanya
mabadiliko ya baadhi ya Wajumbe wa Kamati za Kudumu za Bunge ili kuzingatia
mahitaji mapya na changamoto zilizojitokeza baada ya kuunda Kamati hizo mwezi
Januari 2016. Mabadiliko hayo, yamefanywa chini ya Kanuni ya 116(3) ya Kanuni
za Kudumu za Bunge inayompa Mamlaka ya kuteua Wabunge kuunda Kamati Mbalimbali
za Bunge.
Aidha kufuatia mabadiliko hayo ambayo baadhi yake
yamehusu Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti au wote wawili, Kamati za Kudumu za
Bunge zilizoathirika na mabadiliko haya zitawajibika kufanya Uchaguzi wa
viongozi kwa mujibu wa kanuni ya 116 (10) kama ifuatavyo:
1. Kamati ya
Ardhi, Maliasili na Utalii itahitaji kupata Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti
wapya.
2. Kamati ya
Nishati na Madini itahitaji kupata Mwenyekiti mpya.
3. Kamati ya
Uwekezaji wa Mitaji ya Umma itahitaji kupata Mwenyekiti mpya.
4. Kamati ya
LAAC itahitaji kupata Makamu Mwenyekiti mpya.
5. Kamati ya
Huduma na Maendeleo ya Jamii itahitaji kupata Makamu Mwenyekiti mpya.
Mabadiliko
haya kwenye kamati zote yanaanza mara moja ambapo orodha ya wajumbe
waliobadilishwa imeambatishwa.
Imetolewa na:
Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano
Ofisi ya Bunge DAR ES SALAAM
22 Machi, 2016.
Taarifa kamili pamoja na list ya waheshimiwa wabunge kwenye kamati za kudumu za bunge soma HAPA