Sunday, December 7, 2014

MAWAZO HURU JUU YA MAENDELEO YETU

MAWAZO YANGU.
Wilaya yetu ni moja kati ya wilaya kongwe mkoa wa MWANZA, japo nadhani ndio inaongoza kwa umaskini.Nilifikili nikadhani kuna baadhi ya mambo yanayotufanya tubaki hapa tulipo, machache kati ya mengi

1. Aina ya uongozi mbovu wa serikali uliopo katika wilaya yetu kwa ujumla, kuanzia ngazi ya kijiji hadi ile ya juu kabisa kwenye halmashauri ya wilaya.
hatutaki mabadiliko ya uongozi
2. Kukosekana kwa elimu dunia kwa wananchi juu ya kwenda na wakati kuachana na mawazo ya kizamani(wengi wetu ikiwemo mimi hatujui haki zetu za msingi za kujikomboa kifikra)
3. kukosekana kwa fursa, vijana wengi wazembe japo wapo wanaojituma, bila kupata fursa mambo hayaendi.mfano mzuri ulikuwa kwa mbunge wetu MH. BUJIKU SAKILA, wengi tunajua mchango wake.
4 .Mengine mengi ambayo mi siyajui tutasaidizana kuyaweka wazi
ZAMANI KULIKUWA NA BWANA MARANDO, KAMA RIPOTA WETU JAPO NAE HAKUWA NA UMUHIMU KIVILE LEO KAINGIA KWENYE SIASA. KWIMBA YETU HAKUNA MEDIA (KAMA IPO MI SIIJUI) YEYOTE INAYOTOA HABARI ZA WILAYA KUSIKIKA ILI HATA WALIO MBALI NA NYUMBANI KUJUA KINACHOENDELEA NYUMBANI.

NILICHOFIKILIA AMBACHO KINAWEZEKANA.
>>.Kupatikana kwa ripota wa kutoa matukio/mambo muhimu yanayoendelea wilayani kwetu (kama yupo sawa)
>>blog ya wilaya inayoweza kutoa update ya kila kinachojili katika nyanja zote(naweza kutengeneza ila mbali na nyumbani jinsi ya kupata habari kama watu watajitolea kunitumia nitafanya hivyo)
>>Email ambayo kila mwenye uwezo wa kutoa mawazo yake na mwisho wa siku yanakuwa organized na kupelekwa kwenye uongozi wa wilaya/mbunge ili kufanyia kazi
>>Na mengine mengi, mapendekezo muhimu kwa kila mpigania maendeleo
N.B NAJIVUNIA MAJI KUTOKA VICTORIA KUFIKA KWETU MAANA KILIKUWA KILIO CHA MUDA MREFU, PIA BARABARA YENYE KIWANGO CHA LAMI JAPO SIO LAMI HALISI TAKRIBANI KIL 3 KUTOKA HOSPITAL KWENDA KIWANJA CHA MPIRA(KWIDEKO), NA MENGINE MENGI YALIYOFANYIKA KATIKA KULETA MAENDELEO KATIKA JAMII YETU.
NAWATAKIA TAFAKURI NJEMA WANANCHI WAKEREKETWA WA NGUDU NA KWIMBA KWA UJUMLA
ANGALIZO: POST HII ISIHUSHWE NA SIASA
koh koh koh!.

No comments:

Post a Comment

Previous Page Next Page Home