Mkurugenzi wa shirika la Under The Same Sun (UTSS), Peter Ash |
SHIRIKA la Under The Same Sun (UTSS) limeeleza
kusikitishwa kwake na viongozi wa kisiasa pamoja na mbunge wa jimbo la kwimba
kutofika kumjulia hali na kumfariji mama wa motto mwenye ulemavu wa ngozi,
Pendo Emmanuel (4) aliyeporwa na watu wasiojulikana mwishoni mwa mwaka jana.
Hayo yalielezwa jana na Mkurugenzi wa Mwanzilishi wa
shirika hilo, Peter Ash wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya
kumaliza ziara yake kwenye mikoa ya Mwanza na Shinyanga
“Nimefika kwenye kijiji cha Ndami wilayani Kwimba,
motto pendo alipotekwa na kuzungumza na
wazazi wake ambaye alieleza kuwa mbunge wa jimbo hilo hajaenda
kumtembelea ili kujua motto wake yupo wapi na anashangaa yeye kutoka Canada
amefika”, alisema na kuongeza kwanini mbunge ambaye yeye anampigia kura
hajaenda kumsikiliza.
Alisema January 6, mwaka huu katika eneo la Nyakato,
motto mwingine mwenye ulemavu wa ngozi , karim kassimalinusurika kutekwa ambapo
familia yake nayo inasema hakuna kiongozi wa siasa wala Mbunge walioenda
kuwajulia hali.
Ash alisema watu wenye ulemavu wa ngozi wamekuwa
wakiwindwa na wanaendelea kuwindwa hasa wakati huu kuelekea uchaguzi ambapo
Tanzania na Burundi zinafanya uchaguzi mwaka huu na kuhoji kwa nini vitendo vya
ukatili dhidi ya watu wenye ulemavu wa ngozi vinazidi kuongezeka kipindi hiki.
Alisema kumekuwepo na matukio 152 yakiwemo ya
utekaji nyara, kubakwa na mauaji ambayo yametokea kwa kipindi cha miaka 14
nchini Tanzania; lakini ni asilimia tano tu ya kesi ndio zimefikishwa
mahakamani ambazo hazilingani na idadi ya matukio na watu waliofanyiwa ukatili.
Alisema viungo vya watu wenye ulemavu wa ngozi
vinauzwa kwa bei juu, lakini cha kujiuliza ni nani atakuwa na maelfu ya dola
ili kununua hivyo viungo isipokuwa wale watu ambao ni matajiri, Watanzania
wengi ni masikini.
Mtoto Pendo Emmanuel (4) aliporwa na watu
wasiojulikana December 27, mwaka jana wakati akiwa amelala na wazazi wake
katika kijiji cha Ndami, tarafa ya Mwamashimba wilayani Kwimba, majira ya saa 4
usiku.
Chanzo:
Habari leo
No comments:
Post a Comment