KOMANYA, BONIPHACE, mwandishi wa makala na mmiliki wa blogu |
BY NGUDU NYUMBANI BLOG
Ni ukweli usiopingika kuwa, jimbo la Kwimba tangu mfumo wa vyama vingi kuasisiwa mwaka 1992, na
uchaguzi wa kwanza ukihusisha mfumo huo limeongozwa na chama tawala(CCM)
kuanzia ngazi za serikali za mitaa, wawakilishi kama madiwani, mbunge, pia
halmashauli kuwa chini ya usimamizi wa Ccm. Hali hiyo imeendelea kuonekana
katika chaguzi zote zilizofuata nikimaanisha 2000,2005,2010 na 2015.
Japo kwenye uchaguzi wa
wawakilishi serikali za mtaa mwishoni mwa mwaka jana wapinzani walipata
uwakilishi kwenye baadhi ya vijiji na vitongoji japo haikubadili upepo kisiasa
katika jimbo hili.
Kuna baadhi ya mambo au
sababu zinazonipelekea kusema ndugu Mansoor alikuwa na nafasi kubwa kushinda
ubunge jimbo la kwimba. Machache kati ya mengi ni kama ifuatavyo..
Moja, kukubalika sana
maeneo mengi hasa vijijini. Hii
ni kete kubwa kwa mgombea yeyote kuweka mazingira ya kushinda uchaguzi hasa
ukizingatia vijijini ndio kuna mwitikio mkubwa wa wapiga kura. Imani hiyo
kaijenga tangu agombee awamu iliyopita. Pia wananchi wengi walipata kumwamini
katika miaka mitano iliyopita, kwa maana hiyo imani yao kubwa ilimjenga na
kumpa imani kubwa ya kushinda awamu nyingine. Hapa namaanisha muitikio wao hasa
kwenye kampeni zake.
Pili, nguvu ya pesa
aliyonayo. Pia katika hili
mgombea huyu alikuwa vizuri ukilinganisha na wapinzani wake. Katumia njia hii
kucheza na akili za wananchi kwa kugawa kiasi cha fedha, nguo na vifaa vya
chama. Pia katika hatua nyingine kupitia wapambe wake amegawa majembe baadhi ya
vijiji kuhamasisha maendeleo. Njia hii imeongeza imani kwa wana ccm na wananchi
wasio na vyama hata baadhi ya wapinzani wasio na msimamo kuwa na matumaini nae.
Japo uhalisia ni kwamba inakosekana elimu ya uraia kwa wananchi kujua zawadi
hizi kipindi cha kampeni hazina manufaa ya kudumu katika maisha yao ya kila
siku ukizingatia hutolewa mara moja kila baada ya miaka mitano.
Tatu, kukosekana kwa
upinzani imara wenye kuweza
kujenga hoja na kuja na sera za kuweza kuwashawishi wananchi wawachague. Katika
hili pia UKAWA kushindwa kufikia makubaliano ya kusimamisha mgombea mmoja na
badala yake kusimamisha wawili ndugu Mh shilogela(CDM) na Mh Ntiga Otto(CUF)
kulisaidia kwa kiasi kikubwa kugawana kura za upinzani na kumpa nafasi Mh
mansoor kuwaacha kwa mbali kwenye mchuano.
Nne, kuwaaminisha
wananchi baadhi ya mambo kama kayafanikisha. Kati hili ndugu Mansoor aliweza kuanisha mafanikio katika
awamu iliyopita kama kuwaletea wananchi maji kutoka ziwa Victoria, umeme,
kuwezesha ujengwaji wa zahanati/vituo vya afya kadhaa. Kuweka mambo sawa
ni kuwa kazi ya mbunge kwa mujibu wa katiba ni kuwakilisha wananchi, kutunga sheria na kusimamia
serikali katika masuala ya
maendeleo kama kusimamia miradi. Ila sio kweli kwamba kawaletea wananchi maji
wala umeme, bali ni kupitia kuishauri na kuikumbusha serikali kufanya hayo na
mengine jimboni kwake ila hana uwezo wa kutoa hela yake kufanikisha hayo.
Katika hili la maji limekuwa likipigiwa kelele tangu kale na limekuwa
likihubiliwa kwenye ilani ya ccm kila uchaguzi na limekuja kufanikishwa kwa
kucheleweshwa kwenye uongozi wa JK japo lilikuwepo tangu enzi za Mkapa. Hapa
naweza kuwapongeza Mh mansoor na Mh Leticia Nyerere ambao walipata kuliulizia
utekelezaji wake kila walipopata nafasi kwenye bunge kuuliza swali au kujenga
hoja kila mmoja katika nafasi yake. Katika hayo alifanikiwa kujipatia kura za
kutosha.
Tano, jimbo bado ni
ngome kuu(stronghood) ya chama tawala. Hili pia linachangia kwa asilimia kubwa kama sehemu ni ngome
ya chama fulani miaka nenda rudi ni rahisi kwa chama husika kushinda japo kuna
baadhi ya maeneo hali ilibadilika na ambaye hakutarajiwa kushinda.
Jimbo la Kwimba lipo
chini ya Ccm kabla ya mfumo wa vyama vingi, baada ya kuanzishwa mfumo wa vyama
vingi hadi leo huku wakijikusanyia madiwani wengi na kuweza kuisimamia
halmashauri. Kwahiyo upinzani walipaswa kutumia nguvu zaidi na njia mbadala za
kuwawezesha kushinda.
MAONI YANGU
Nilipata kufatilia
uchaguzi kwa kuwasikiliza wagombea kama Mh Mansoor, Mh shilogela na Ndugu Ntiga
kusikiliza sera zao na hoja zao juu ya uwakilishi wa jimbo letu.
Kiukweli nilimwelewa sana ndugu Ntiga Otto
jinsi alivyokuwa akiwasilisha Mipango na mikakati yake juu ya kuiongoza Kwimba,
japo ni hali isiyofichika kwamba ndiye alikuwa na wasikilizaji/wananchi
wachache zaidi ukilinganisha na hao wenzake wawili waliokuwa na watu wengi.
Hawa Iswalala(UDP) na mch. Yohana(ACT)
sikupata kuwasikia ama kuhudhulia kampeni zao. Bila shaka kilichomwangusha huyu
kijana aliyejimbanua(Otto) ni kutokukubaliana kwenye umoja wao. Pia ‘mind set’
za wananchi wengi ambao hawako tayari kusikiliza sera na kubakia kushabikia
vyama zaidi.
Salamu zangu hizi
zimfikie popote alipo na asikate tama ajipange kwa awamu ijayo.
Uchaguzi umeisha, mbunge
na madiwani wamepatikana, cha msingi ni kuwapa support tuweze kufikia lengo la
kupiga hatua ya maendeleo jimbo na wilaya yetu kwa ujumla.
Malalamiko ya kwamba huyu mhindi, sijui sio
mzawa hayatosaidia kitu zaidi ya kushirikiana na kiongozi aliyeshinda kusukuma
gurudumu la maendeleo. Pia ideology ya kuwa mbunge ndio mtu sahihi wa kuleta
maendeleo jimboni, ni ya kupuuzwa tu. kila mmoja wetu anayo nafasi ya kuleta
maendeleo kwenye jamii yake na sio kusubiri fulani akuletee maendeleo mlangoni.
tunawa support viongozi
wa ngazi zote tukiweka itikadi za vyama vyetu pembeni. Sote ni wamoja ubaguzi
ni kuonesha udhaifu.
kutokana na machache niliyoyagusia hapo juu, nashawishika kusema kwamba Ilikuwa ni lazima kwa mh. Mansoor kushinda ubunge kwenye jimbo la Kwimba mwaka 2015.
kutokana na machache niliyoyagusia hapo juu, nashawishika kusema kwamba Ilikuwa ni lazima kwa mh. Mansoor kushinda ubunge kwenye jimbo la Kwimba mwaka 2015.
KWIMBA TUITAKAYO
nguduone@gmail.com
No comments:
Post a Comment