JAMHURI
YA MUUNGANO WA TANZANIA
TUME
YA TAIFA YA UCHAGUZI
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
UTEUZI WA MADIWANI WANAWAKE WA VITI MAALUM
Kwa mujibu wa Kifungu cha 86 A (8) cha Sheria ya
Uchaguzi Serikali za Mitaa Sura ya 292, (Uchaguzi wa Madiwani) kikisomwa kwa
pamoja na Vifungu vya 35 (1) (c) na 19 (1) (c) vya Sheria za Serikali za Mitaa
(Tawala za Wilaya) na Na. 7 ya mwaka 1982 na Serikali za Mitaa (Tawala za Miji)
Na. 8 ya mwaka 1982, Tume ya Taifa ya Uchaguzi imepewa mamlaka ya kushughulikia
na kutangaza Viti Maalum vya Madiwani Wanawake visivyopungua 1/3 ya Madiwani wa
kuchaguliwa katika kila Halmashauri. Kwa kuwa Kata 3,957 zilifanya Uchaguzi
Mkuu 2015 hivyo 1/3 yaViti Maalum vya Madiwani Wanawake ni 1,406. Hata hivyo,
Tume haikuweza kugawa Viti vyote katika Halmashauri kutokana na kuahirishwa kwa
Uchaguzi wa baadhi ya Kata katika baadhi ya Halmashauri nchini. Mgawanyo wa
viti vilivyobaki utafanyika mara baada ya chaguzi zilizoahirishwa kufanyika.
Vyama vya Siasa vilivyoshiriki Uchaguzi Mkuu kwa
upande wa Madiwani na kukidhi vigezo vya kisheria vya kupata Viti Maalum ni
kama ifuatavyo:-
Jumla ya Viti vilivyogawanywa ni 1,392.
Viti 14
vilivyosalia vitagawanywa mara baada ya Kata zilizoahirishiwa Uchaguzi
kukamilisha zoezi la kupiga Kura
Majina ya Madiwani Wanawake wa Viti Maalum kwa kila
Halmashauri walioteuliwa yataweza kupatikana kutoka Vyama na kwenye Halmashauri
husika. Aidha tarehe 14/11/2015, Tume ya Taifa ya Uchaguzi itatangaza majina ya
Madiwani wa Viti Maalum walioteuliwa. Ikumbukwe kuwa Tume imefanya uteuzi kwa
kuzingatia Orodha iliyowasilishwa Tume na kila Chama kwa kuzingatia vipaumbele
vya Chama husika.
Imetolewa na:
Jaji
(Mst.) Damian Z. Lubuva
MWENYEKITI
TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI
12/11/2015
No comments:
Post a Comment