Kikao cha Baraza la Madiwani kwaajili ya kupitisha hesabu za Halmashauri
ya Kwimba mkoani Mwanza pamoja na Kamati ya Ulinzi na usalama ya wilaya
kimeketi Sept 28 mwaka huu wilayani humo.
Sunday, October 2, 2016
Thursday, September 8, 2016
HATI ZENYE MASHAKA ZALALAMIKIWA MWANZA
SERIKALI imeshauriwa
‘kuwatumbua’ watumishi waliosababisha halmashauri za mkoa wa Mwanza kuendelea
kupata hati zenye mashaka baada ya kutozingatia viwango vya kimataifa vya
uandaaji wa hesabu (IPSAS).
Changamoto hiyo
ilitolewa na baadhi ya wajumbe wa kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC) wa
Mwanza kilichofanyika jijini hapa wiki iliyopita, ambapo taarifa ya Mdhibiti na
Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa mwaka wa fedha 2014/2015 ilionesha
kuwa halmashauri sita kati ya saba zinazounda mkoa huo zilipata hati zenye
mashaka.
Halmashauri zilizopata
hati zenye mashaka kutokana na ukaguzi huo wa CAG ni Jiji la Mwanza na wilaya
za Kwimba, Magu, Misungwi, Sengerema na Ukerewe, huku Ilemela ikiwa ndiyo
wilaya pekee iliyopata hati safi/inayoridhisha.
Taarifa
hiyo ya CAG inataja makosa yaliyosababisha halmashauri hizo kupata hati zenye
mashaka kuwa ni pamoja na watumishi husika kutozingatia viwango vya kimataifa
vya uandaaji wa hesabu ambapo hazikuonesha thamani ya ardhi na viwanja
vinavyomilikiwa katika hesabu za mwisho zinazoishia Juni 2015.
Sababu
nyingine ni kufanya malipo ya fedha yenye nyaraka pungufu, kutowasilisha vitabu
vya kukusanya mapato, kutopeleka fedha benki, kutoingiza madeni yanayodaiwa katika
hesabu za mwisho na kutowasilishahati za malipo ya fedha.
Baadhi
ya wajumbewa kikao hicho walielezea kukerwa kwao na makosa hayo ya kihesabu
wakionesha wasiwasi kwamba huenda ni mpango wa makusudi uliosukwa na watumishi
wachache kwa ajili ya kujinufaisha kiharamu na fedha za umma.
“Hali hii inatupa
wasiwasi kwamba huenda ni namna ya watu fulani waliojipanga kuhujumu na kula
fedha za umma kwa sababu haiwezekani halmashauri hizo sita kupata hati zenye
mashaka kutokana na makosa yanayofanana.
“Inawezekana
halmashauri hizo hazina wataalamu wa masuala ya usimamizi wa fedha na huenda
serikali imeajiri vilaza wasiyo na taaluma inayotakiwa,” alilalamika mjumbe wa
kikao hicho, Edward Mboje aliyejitambulisha kuwa ni Katibu wa UDP Mkoa wa
Mwanza.
Hata hivyo, licha ya
kauli hiyo ya Mboje kuungwa mkono na wajumbe wengine kadhaa, hakuna majibu wala
ufafanuzi uliotolewa katika kikao hicho kilichoongozwa na Mkuu wa Mkoa wa
Mwanza, John Mongella
CHANZO: RAIA MWEMA
Sunday, August 14, 2016
KWIMBA TUITAKAYO ITAPATIKANA KWA USHIRIKI MZURI WA WANANCHI NA VIONGOZI
(Hizi ni salamu zangu kwenu viongozi na wananchi wa
Kwimba katika awamu hii ya HAPA KAZI TU)
BY NGUDU NYUMBANI BLOG
14/08/2016
Ni imani yangu kuwa wote tu wazima wa afya,
tunaendelea na ujenzi wa taifa letu. Leo NGUDU NYUMBANI ingependa kuwakaribisha
rasmi viongozi mbalimbali waliopewa majukumu mazito kuiongoza wilaya yetu
kongwe ya KWIMBA katika awamu hii ya 5.
Bila shaka wengi wetu tunawafahamu viongozi wetu
kuanzia ngazi ya vijiji, vitongoji, mitaa, kata, tarafa na hadi ngazi ya
wilaya.
Kwa faida ya wengine ambao hawajui, Mkuu wa
wilaya(DC) ya Kwimba kwa sasa ni Mhandisi
Mtemi Msafiri Simeon, Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya(DED) ni Pendo
Anangisye Malabeja na Katibu tawala wa wilaya(DAS) ni Andrea Izziga Ng’hwani. DED si mgeni kwetu
sababu amewahi kuhudumu katika nafasi hiyo kabla.
Kuhusu wabunge wa majimbo ya Kwimba na Sumve bila
shaka tunawajua, madiwani wetu na viongozi wengine wote wa ngazi zote
tunawafahamu.
Awamu ya tano imeingia na kasi ya aina yake katika
kuhakikisha inatoa majibu ya changamoto zinazowakabili wananchi wake, ikiongozwa
vema na Rais wa JMT, Dr John Pombe Magufuli.
Katika mambo ambayo Rais amekuwa akisisitiza kufanyiwa kazi na viongozi
aliowateua katika ngazi mbalimbali hasa ngazi ya halmashauri za
wilaya(mkurugenzi, Mkuu wa wilaya na Katibu tawala n.k) ni pamoja na;
Usuluhishaji wa migogoro ya ardhi baina ya wakulima na wafugaji au wakulima
dhidi ya mwekezaji au viongozi wa serikali na wananchi. Mfano mzuri ni mwezi wa
pili mwaka huu pale Naibu waziri wa Ardhi, Nyumba na Maelndeleo ya Makazi
Angelina Mabula alipombana Afisa ardhi wa wilaya ampatie maelezo kuhusu idara
hiyo kuchukua fedha ya wananchi bila ya kuwagawia viwanja. Hayo na mengine
mengi yanapaswa kupatiwa majawabu ya kudumu.
Tatizo la elimu hasa upungufu wa madawati ambalo kwa
kiasi kikubwa limeshughulikiwa. Nilisoma taarifa moja ikimnukuu mkurugenzi wa
wilaya akisema wilaya ya Kwimba ina nakisi ya madawati 5,314 sawa na asilimia
15 kumaliza tatizo la uhaba kufikia julai 30 mwaka huu. Hayo aliyazungumza wakati wa hafla fupi ya kupokea
msaada wa madawati 60 yenye thamani ya Sh milioni 5 iliyofanyika shule ya
msingi Kakora Kata ya Ngudu Mjini, kutoka kwa uongozi wa Benki ya CRDB tawi la
Nyerere jijini Mwanza. Hivyo hadi kufikia julai 21 kulikuwa na upungufu wa
madawati 5,254.
Maagizo mengine ya Rais ni pamoja na kukabiliana na
baa la njaa pamoja na milipuko ya magonjwa katika mikoa na wilaya zote nchini.
Pia kupitia maagizo ya RC Mongella ya june 04 mwaka
huu alipokuwa akiwaapisha wakuu wa
wilaya, ambapo pamoja na yote
alisisitiza wakasimamie shughuli za kuhimiza maendeleo, suala la ulinzi na
usalama huku akitilia mkazo ukomeshwaji wa mauaji ya watu wenye ulemavu wa
ngozi na vikongwe.
Katika kuwakaribisha huko NGUDU NYUMBANI ingependa
kuwakumbusha machache yaliyopo ndani ya wilaya yetu.
ELIMU
Pamoja na kukabiliana na tatizo la madawati, zoezi
lililofanikiwa kwa kiasi kikubwa. Wilaya yetu bado ipo nyuma sana katika suala
la elimu. Ningependa kulielezea hili kwa kuhusianisha na matokeo ya vijana wetu
kwenye shule za msingi na sekondari.
Bahati nzuri teknolojia imekua kiasi hata cha
matokeo ya upimaji wa kitaifa darasa la nne(SFNA), Matokeo ya darasa la saba,
ya kidato cha pili yote yanawekwa kwenye mtandao. Ukipitia blogu yetu utayaona
na kukubaliana nami.
Tatizo ni kubwa sana katika ufaulu wa shule zetu,
mathalani vijana wanaohitimu kidato cha nne. Niliandika makala yenye jina
‘IDADI YA WALIOCHAGULIWA KIDATO CHA TANO KWA KILA SHULE ZILIZOPO WILAYA YA
KWIMBA’ pia NGUDU NYUMBANI ilifanya tathmini ya matokeo ya kidato cha 4 mwaka
2015. Kwa waliofuatilia matokeo kwa ujumla au walau kusoma tathmini wanaweza kukubaliana
nami kuwa bado tuna safari ndefu katika elimu yetu.
Shule za A-level zilizopo wilaya ya Kwimba walau
zinafanya vizuri katika matokeo yao. Ambapo katika matokeo ya mwaka huu, Mwamashimba H/school wameshika nafasi ya 2/25
kimkoa(ina division 1-3, hakuna four na zero), Sumve ikishika nafasi ya 11/25
kimkoa na Ngudu H/school nafasi ya 12/25 Kimkoa.
Mbali na matokeo, bado sekta ya elimu ina changamoto
lukuki, ikiwemo uhaba wa nyumba za walimu, madarasa, uhaba wa walimu n.k. ‘Elimu ni walimu’ kauli hii imewahi kutolewa
maelezo jadidi na mujarabu na Prof Kitila
Mkumbo katika moja ya makala zake kwenye gazeti la Raia mwema, pia wadau
wengine wamepata kusisistiza kauli hii. Bila kuwekeza katika changamoto
zinazowakabili waalimu bado elimu yetu itabaki nyuma daima dawamu.
Pamoja na yote hayo wilaya yetu inaburuza mkia
katika ufaulu kimkoa kwa muda sasa. Hivyo viongozi wenye dhamana ya kusimamia
sekta hii wasifanye kazi kwa mazoea tungependa kuona mabadiliko.
KILIMO NA HALI YA UCHUMI
MWANZA ni miongoni mwa mikoa(mitano)
inayoongoza kwa umaskini Tanzania na asilimia ya umaskini(35.3 %) hii ni
kulingana na mpango wa maendeleo wa Taifa kwa mwaka wa fedha 2016/167.
kupitia gazeti la mwananchi
waliandika kwamba, Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Dr, Tibeza alisema taarifa
alizonazo zinatofautiana na alizopewa zinaonyesha kuwa Mkoa wa Mwanza ni
miongoni mwa mikoa mitano inayokabiliwa na upungufu wa chakula.
Alinukuliwa akisema “Taarifa
nilizopewa na mthamini wa chakula zinasema Mwanza ni miongoni mwa (mikoa)
inayokabiliwa na upungufu wa chakula, hivyo itakuwa na njaa, lakini wewe
(Mongella-Mkuu wa Mkoa wa Mwanza) unaniambia kuna chakula cha kutosha,”.
Pamoja na yote hayo,asilimia kubwa
ya wakazi wa Kwimba ni wakulima na wafugaji. wakulima wanaotegemea zaidi mvua za masika ambazo mara
nyingi hazieleweki na sio za kutegemea sana katika kilimo chao.
Mazao kama pamba, alizeti, mpunga,
mahindi n.k ndiyo huliwa na wakulima japo ni kwa uchache ambao wengi wengi wao
hulima kukidhi mahitaji ya familia na wachache hutegemea kuuza kujipatia
kipato.
Changamoto zilizopo hasa kwenye zao la pamba mikoa ya kanda ya ziwa ni
nyingi na hazijapata ufumbuzi wa kudumu. Licha ya kuwa vinu kadhaa vya
kuchambulia pamba bado zao hili halimnufaishi ipasavyo mkulima.
Bwawa la mahiga maalumu kwa kilimo
cha umwagiliaji na uvuvi, kunapaswa kuwepo mipango mizuri katika kulitumia
bwawa hili ili liweze kuwanufaisha wananchi na serikali kwa ujumla.
Elimu inapaswa kutolewa kwa
wakulima, hasa kulima mazao yenye kuhimili ukame, utumiaji bora wa zana bora za
kilimo n.k
UKUAJI WA TEKNOLOJIA
Ukuaji wa sekta ya teknolojia ya habari na
mawasiliano kwa miaka ya hivi karibuni, imekuwa ikikua kwa kasi ukilinganisha
na uhitaji wa watumiaji wa huduma zihusianazo na sekta hiyo. Kumekuwa na
uwekezaji mkubwa katika hili, hali ambayo inatia moyo japo sio kwa kiwango
kinachotakiwa lakini walau inaridhisha.
Ukuaji wa TEHAMA umesababisha
mabadiliko ya uendeshaji wa shughuli za serikali na jamii kwa ujumla.
Ukuaji wa sekta hii unahusisha na vitu vingi ambapo
baadhi ni kama matumizi bora, sahihi na salama ya vifaa na mifumo ya
TEHAMA serikalini. Mbali na hilo pia,
lengo jingine kubwa ni kurahisisha upatikanaji wa habari, uhuru wa kupata
habari na kusambaza kwa wengine bila kuathiri, kuingilia, kukiuka au kuvunja
katiba na sheria zote za nchi zinazolinda uhuru huo.
Kwa leo nitaongelea zaidi kuhusu
matumizi bora na sahihi ya vyombo vya Tehama hasa kwenye matumizi ya mitandao
na intaneti(tovuti, barua pepe n.k)
Kuna uhitaji mkubwa kwa taasisi ama za serikali au
binafsi kuwa na tovuti katika hatua mojawapo ya kurahisisha upatikanaji wa
mambo muhimu yahusuyo taasisi husika. Hasa nikiongelea upande wa serikali,
mamlaka zake nyingi zinatunza na kutoa taarifa zao kwenye tovuti. Ofisi ya
Rais, na ofisi nyingine nyingi kubwa zinafanya hivyo pia.
Ni utaratibu mzuri unaokubalika katika kukuza secta
ya TEHAMA, ambapo unarahisisha upatikanaji wa habari muhimu kwa wale wenye
uwezo wa kutumia mitandao na intaneti kwa ujumla.
Ombi langu kwa hawa viongozi wetu ni kuhakikisha
wilaya inakuwa na tovuti rasmi ambapo, habari zote muhimu za wilaya yetu zenye
kupaswa kuwafikia wananchi ziweke kupatikana kule.
Sambamba na uanzishwaji wa hiyo tovuti, itasaidia
viongozi waandamizi wa serikali ngazi ya wilaya kutumia barua pepe za serikali.
Mwongozo wa matumizi bora, sahihi na salama ya vifaa
na mifumo ya Teknolojia ya habari na mawasiliano(TEHAMA) serikalini toleo la
julai 2012, umesisitiza matumizi wa anwani za barua pepe hasa usajiri wa barua
pepe za serikali.
Anwani za
barua pepe binafasi mfano ‘yahoo.com’, ‘hotmail.com’,
‘gmail.com’ n.k hazipaswi kutumika katika mawasiliano ya shughuli za serikali.
Sasa sijui viongozi wetu wanatumia anwani zipi maana
inaelekezwa taasisi za serikali anwani za barua pepe zao ziwe zenye kikoa cha
mfumo wa ‘.go.tz’ na mfumo wa kifupisho
cha cheo jina la taasisi na kikoa husika. Mfano anwani ya barua pepe ya
mkurugenzi inaweza kuwa.. md@kwimbadc.go.tz
na sio dedkwimba@yahoo.com
iliyokuwa inatumika kabla.
Hiyo kwimbadc.go.tz
ndio tovuti inayopaswa iwepo hewani kwa maana ya kupatikana muda wote(umiliki
wa domain name).
Kuna shida katika tovuti ya mkoa(www.mwanza.go.tz)
hasa katika viungo(links) za wilaya, waliopata kutembelea tovuti hii wanaweza
jua ninachomaanisha.
Mfano ukifungua kwenye link ya ‘Kwimba DC’
utafunguliwa ukurasa ukiwa wazi na ujumbe ukisema ‘Ukurasa huu upo kwenye matengenezo’ ni zaidi ya miaka miwili na zaidi sasa, enewei
pengine matengenezo yanahitaji mwongo mzima tuendelee kusubiri.
Pamoja na hayo yote, kuna blogu moja(www.kwimbadc.blogspot.com)
inayoripoti baadhi ya taarifa za halmashauri, japo sina hakika kama ndiyo
inayotambulika. Kupitia blogu hiyo kuna ‘jarida la Kwimba’ toleo la 45 lenye
jina ‘IJUE KWIMBA’.
Kwa ambao hamjapata kusoma ni vema mkapitia kuna mambo
mazuri ya kuyajua mule japo kwa ufupi. Pia kuna Documentary ya miaka 10 ya
maendeleo ya KWIMBA 2005-2015.
Ningependa kumaliza kwa leo, kwa kunukuu baadhi ya
maneno kwenye kitabu cha Uhuru na Maendeleo kilichoandikwa na Baba wa Taifa
hayati Mwl J.K Nyerere, alisema;
Kama maendeleo yanaongeza uhuru wa watu, basi lazima
yawe maendeleo yanayowafaidia watu. Lazima maendeleo hayo yawe na faida kwao,
na kumaliza shida zao. kila mpango uamuliwe kwa kupima kama unatimiza shabaha
ya maendeleo, na shabaha ya maendeleo ni
watu. Lakini kama mpango unasaidia maendeleo ya watu na kama unatimizwa
na watu kwa hiari yao, mpango huo utatimiza haja za watu, mradi masharti matatu
yametimizwa. Kwanza, kama watu wanaelewa shida zao. Pili, kama wanaelewa jinsi
shida hizo zinavyoweza kumalizwa. Na tatu, kama wana uhuru wa kujiamulia
mipango yao, na kuitimiza.
Itaendelea……
Tafakari!
nguduone@gmail.com
Friday, August 5, 2016
HALMASHAURI KWIMBA YAPOKEA MADAWATI 60 YA CRDB NYERERE JIJI LA MWANZA YATAKA WADAU WANANCHI KUCHANGIA ASLIMIA 15 ILIYOBAKI
HALMASHAURI ya Wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza, inahitaji madawati 5,314 sawa na asilimia 15 kukamilisha agizo la Rais Dk John Magufuli ifikapo Julai 30 mwaka huu.
Kauli hiyo imetolewa
jana na Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Pendo Malebeja, wakati wa hafla fupi ya
kupokea msaada wa madawati 60 yenye thamani ya Sh milioni 5 iliyofanyika shule
ya msingi Kakora Kata ya Ngudu Mjini, kutoka kwa uongozi wa Benki ya CRDB tawi
la Nyerere jijini Mwanza ikiwa ni kuunga jitiada za serikali ya awamu ya tano
katika kuboresha miundombinu ya elimu nchini.
Malebeja alisema
kwamba hadi juzi Halmashauri ilikuwa imetengeneza na kukarabati jumla ya
madawati 30,006 sawa na asilimi 85 ambapo mahitaji halisi ni madawati 35,000
hivyo upungufu uliopo ni 5,314 sawa na asilimia 15 baada ya kupokea madawati 60
kutoka kwa wadau Benki ya CRDB upungufu sasa ni 5,254.
Akizungumza wakati wa
kukabidhi msaada huo, Meneja wa CRDB tawi la Nyerere, Naomi Mwamfupe, alisema
kwamba wao wanaunga mkono juhudi za serikali za kuboresha miundombinu ya Elimu,
Afya, Mazingira, pamoja na kusaidi yanapotokea maafa na majanga lengo ikiwa ni kuleta
usitawi wa jamii na kukuza uchumi.
“Tumewezesha wanafunzi
120 kukaa kwenye madawati baada ya wananchi wa Wilayah ii nao kujitokeza na
kuchangia madawati kwa kushirikiana na serikali kwa asilimia 85 hivyo kwa
mafanikio ya miaka 20 ya Benki ya CRDB nchini tunaunga mkono juhudi za Rais Dk
Magufuli kuboresha miundombinu katika Sekta zote za utoaji huduma kuwa rafiki
kwa wananchi,”alisema.
Mwamfupe alimtaka
Mkurugenzi Malebeja na Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Peter Ngassa (CCM),
kufikisha ushauri kwenye Kikao cha Baraza la madiwani ili kuangalia uwezekano
wa kufungua Akaunti katika tawi la benki hiyo lililopo ofisi za Halmashauri
hiyo ili kuwapa fursa wadau mbalimbali na wananchi kujitokeza kwa hiali
kuchangia maendeleo ikiwemo madawati.
Kwa upande wake mgeni
rasmi aliyemuwakirisha Mkuu wa Wilaya hiyo, Katibu Tawala wa Wilaya (DAS),
Andreaw Ng’hwani, alipongeza uongozi wa Benki hiyo tawi la Nyerere kwa
kujitokeza kusaidia madawati ili kuwezesha Halmashauri kufikia lengo kwa
asilimia 100 kama ilivyoagizwa na Rais Dk Magufuli nhini kote.
Chanzo: GSENGO BLOG
SENGA AZIKWA KIJIJINI KWAO KWIMBA
Mbunge wa jimbo la Sumve, Richard Ndasa akiweka shada la maua |
Bi. Winfrida Senga akiweka shada la maua kwenye Kaburi la Mumewe, wakati wa mazishi yaliyofanyika kwenye Makaburi ya Kijijini kwao, Shushu Kwimba, Jijini Mwanza. |
Senga (58) aliyefariki dunia Julai 27
mwaka huu nchini India, alizikwa nyumbani kwao katika Kijiji cha Shushi
wilayani Kwimba.
Maziko hayo yaliongozwa na Kiongozi wa
Kambi rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe ambaye pia mwenyekiti wa
Chadema. Pia alikuwapo Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Vincent Mashinji
na mamia ya waombolezaji.
Akizungumza katika maziko hayo, Mbowe
alimuelezea Senga kuwa ni shujaa wa mapambano ya kupigania haki na demokrasia
ya kweli nchini.
Alisema kazi za Senga
aliyoiacha hapa duniani ni kielelezo thabiti cha uwajibikaji usioogopa vitisho.
“Senga alikuwa mfanyakazi na mtumishi
mwenzetu. Senga hakuwa baraka kwa wana Kwimba pekee, bali alikuwa mtu wa wote.
Nimefanya kazi naye kwa zaidi ya miaka 16. Tumezunguka naye kila eneo ndani ya
nchi hii. Hakuna operesheni ya Chadema tuliyomuacha Senga,” alisema
Mbowe.
Vilevile, alisimulia mazingira tatanishi
yaliyosababisha kifo cha aliyekuwa mwandishi wa habari wa Kituo cha Channel Ten
mkoani Iringa, Daud Mwangosi.
Mbowe aliyetumia dakika 20
kumzungumzia marehemu Senga, alisema usingekuwa ujasiri wake kupiga picha za
tukio la kifo cha Mwangosi, dunia isingefahamu polisi ndiyo waliohusika
na mauaji hayo.
Senga ameacha mke mmoja na watoto saba,
kati yao wanne wa kike na watatu wa kiume.
Mungu ailaze mahala pema peponi, roho ya
marehemu, Joseph Senga.
Chanzo: MTANZANIA
Mpango wa Chandarua Kliniki wagawa vyandarua mkoani Mwanza.
Malaria yapungua mkoani mwanza
Mpango wa ugawaji wa vyandarua
unaojulikana kama CHANDARUA KILINIKI ulioanzishwa na serikali ya Marekani
kupitia shirika la USAID umewafikia wananchi wa Mwanza mwishoni mwa wiki ikiwa
lengo lake ni kuendeleza dhamira yake yakupambana na malaria nchini hasa kwa
Mama wajawazito na watoto.
Akitoa taarifa, wakati wa utambulisho wa mpango na ugawaji vyandarua kupitia kliniki ya wajawazito na watoto,Mratibu wa Malaria mkoa wa Mwanza Dk Saula Baichumila alisema Jumla ya wagonjwa 235 wa Malaria katika Mkoa wa Mwanza wamepoteza maisha kwa kipindi cha miezi sita kuanzia Januari hadi Juni mwaka huu ambapo vifo 121 sawa na asilimia 51.5 ni vya watoto chini ya miaka mitano.
“Kutokana na vifo hivyo halmashauri ya Sengerema inaongoza kwa asilimia 27.6, Magu 20.4, Ukerwe 14.5, Nyamagana 11.9, Misungwi 11.1, Kwimba 8.5, Buchosa 3.4 na Ilemela 2.6,” alisema Dk Baichumila
Alisema mkoa umeendelea kupambana na ugonjwa huo kwa kushirikiana wadau mbalimbali ambapo kumekuwa na matokeo mazuri kwa ugonjwa huo kupungua hasa toka waliposhirikiana na USAID kupitia mpango wa CHANDARUA KLININKI mkoani Mwanza hadi sasa jumla ya vyandarua 142,360 tayari vimesambazwa kupitia vituo vya kutolea huduma za afya mkoani hapo.
Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella, Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Marry Onesmo, alisema maambukizi ya ugonjwa wa Malaria mkoani hapo yamepungua kutoka asilimia 19.1 ya mwaka 2011/12 hadi kufikia asilimia 15.1 mwaka2015/16.
Alisema lengo la mpango huo ni kupunguza vifo vya wajawazito na watoto wenye umri chini ya miaka mitano vinavyosababishwa na malaria.Alisema takwimu za kitaifa za mwaka 2012 zinaonyesha kuwa kila vizazi hai 1000, watoto 54 hupoteza maisha huku malaria ikiongoza kuchangia vifo hivyo, huku kila vizazi hai 100,000 wajawazito 432 hupoteza maisha wakati wa kujifungua.
Mpango wa chandarua kliniki unatekelezwa na USAID chini ya mradi wa Vectorworks ambao ni mradi wa miaka mitano 2014-2019 ukiwa na dhumuni la kuongeza upatikanaji na matumizi ya vyandarua vyenye viatilifu vya muda mrefu kwa kushirikikiana na serikali ambapo wamejiweke lengo kuwa hadi kufikia mwaka 2016 kitaifa iwe imefikia asilimia 6 na mwaka 2020 iwe asilimia 1 kutoka asilimia 9 ya sasa.
Akitoa taarifa, wakati wa utambulisho wa mpango na ugawaji vyandarua kupitia kliniki ya wajawazito na watoto,Mratibu wa Malaria mkoa wa Mwanza Dk Saula Baichumila alisema Jumla ya wagonjwa 235 wa Malaria katika Mkoa wa Mwanza wamepoteza maisha kwa kipindi cha miezi sita kuanzia Januari hadi Juni mwaka huu ambapo vifo 121 sawa na asilimia 51.5 ni vya watoto chini ya miaka mitano.
“Kutokana na vifo hivyo halmashauri ya Sengerema inaongoza kwa asilimia 27.6, Magu 20.4, Ukerwe 14.5, Nyamagana 11.9, Misungwi 11.1, Kwimba 8.5, Buchosa 3.4 na Ilemela 2.6,” alisema Dk Baichumila
Alisema mkoa umeendelea kupambana na ugonjwa huo kwa kushirikiana wadau mbalimbali ambapo kumekuwa na matokeo mazuri kwa ugonjwa huo kupungua hasa toka waliposhirikiana na USAID kupitia mpango wa CHANDARUA KLININKI mkoani Mwanza hadi sasa jumla ya vyandarua 142,360 tayari vimesambazwa kupitia vituo vya kutolea huduma za afya mkoani hapo.
Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella, Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Marry Onesmo, alisema maambukizi ya ugonjwa wa Malaria mkoani hapo yamepungua kutoka asilimia 19.1 ya mwaka 2011/12 hadi kufikia asilimia 15.1 mwaka2015/16.
Alisema lengo la mpango huo ni kupunguza vifo vya wajawazito na watoto wenye umri chini ya miaka mitano vinavyosababishwa na malaria.Alisema takwimu za kitaifa za mwaka 2012 zinaonyesha kuwa kila vizazi hai 1000, watoto 54 hupoteza maisha huku malaria ikiongoza kuchangia vifo hivyo, huku kila vizazi hai 100,000 wajawazito 432 hupoteza maisha wakati wa kujifungua.
Mpango wa chandarua kliniki unatekelezwa na USAID chini ya mradi wa Vectorworks ambao ni mradi wa miaka mitano 2014-2019 ukiwa na dhumuni la kuongeza upatikanaji na matumizi ya vyandarua vyenye viatilifu vya muda mrefu kwa kushirikikiana na serikali ambapo wamejiweke lengo kuwa hadi kufikia mwaka 2016 kitaifa iwe imefikia asilimia 6 na mwaka 2020 iwe asilimia 1 kutoka asilimia 9 ya sasa.
Friday, July 15, 2016
Thursday, July 14, 2016
TCU WAMETANGAZA MABADILIKO YA TARATIBU,VIGEZO NA SIFA ZA KUJIUNGA CHUO KIKUU MWAKA WA MASOMO 2016/2017
FORM SIX LAZIMA UWE NA TWO PRINCIPAL PASSES (YAANI D MBILI KATIKA COMBINATION YAKO) BADALA YA E MBILI KAMA ILIVYOKUWA AWALI*
*EQUIVALENT APPLICANTS (DIPLOMA) LAZIMA UWE NA GPA 3.5 KUENDELEA,AU WASTANI WA B KWENYE MASOMO YAKO KWA DIPLOMA YA ELIMU NA AFYA,AU UPPER SECOND CLASS FOR DIPLOMA*
*PRENTRY COURSE ZOTE KWA WANAFUNZI WALIOKUWA HAWANA SIFA KUJIUNGA NA CHUO KIKUU ZIMESIMAMISHWA
SOMA VIGEZO VYOTE>>> HAPA
Thursday, July 7, 2016
UTEUZI WA WAKURUGENZI, PENDO MALABEJA ABAKIZWA KWIMBA.
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 07 Julai, 2016
amefanya uteuzi wa wakurugenzi wa halmashauri za majiji 5, Manispaa 21, Miji 22
na Wilaya (DC) 137 za Tanzania Bara.
Uteuzi huo umetangazwa
na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)
Mhandisi Mussa Iyombe ambapo kati ya wakurugenzi wote 185 walioteuliwa, 65
wameteuliwa kutoka orodha ya wakurugenzi wa zamani na 120 ni wakurugenzi wapya.
Orodha ya wakurugenzi
walioteuliwa kulingana na mikoa yao ni kama ifuatavyo;
ARUSHA
1.
Arusha
Jiji
- Athumani Juma
Kihamia
2.
Arusha
DC
- Dkt. Wilson
Mahera Charles
3.
Karatu
DC
- Banda Kamwande
Sonoko
4.
Longido
DC
- Jumaa Mohamed
Mhiwapijei
5.
Meru
DC
- Kazeri
Christopher Japhet
6.
Monduli
DC
- Stephen Anderson
Ulaya
7.
Ngorongoro
DC
- Raphael John
Siumbu
DAR ES SALAAM
1.
Dar es salaam
Jiji
- Siporah Jonathan Liana
2.
Kinondoni
Manispaa
- Aron Titus
Kagurumjuli
3.
Temeke
Manispaa
- Nassibu Bakari
Mmbaga
4.
Ilala
Manispaa
- Msongela Nitu
Palela
5.
Kigamboni
Manispaa
- Stephen Edward
Katemba
6.
Ubungo
Manispaa
- Kayombo Lipesi
John
DODOMA
1.
Dodoma
Manispaa
- Dkt. Leonard M.
Masale
2.
Kondoa
DC
- Kibasa Falesy
Mohamed
3.
Kondoa
Mji
- Khalifa Kondo
Mponda
4.
Mpwapwa
DC
- Mohamed Ahamed
Maje
5.
Kongwa
DC
- Mhandisi Ngusa
Laurent Izengo
6.
Chemba
DC
- Semistatus
Hussein Mashimba
7.
Chamwino
DC
- Athuman Hamis
Masasi
8.
Bahi
DC
- Rachel Marcel
Chuwa
Tuesday, July 5, 2016
Maagizo ya RC Mongella kwa wakuu wa wilaya wapya mkoa wa Mwanza
Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella, amewaapisha wakuu wapya wa
Wilaya za Mkoa wa Mwanza na kuwapa vitendea kazi ikiwapo katiba ya Jamhuri ya
muungano wa Tanzania na Ilani ya Chama Tawala Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya
Mwaka 2015- 2020, kwaajili ya kwenda kutimiza wajibu wao wa kikatiba kwenye
wilaya walizo pangiwa.
Akizungumza baada yakuwaapisha, Mhe. Mongella, amewataka waende
wakasimamie shughuli za kuhimiza maendeleo, suala la ulinzi na usalama kwenye
wilaya zao, huku akitilia mkazo ukomeshwaji wa mauwaji ya watu wenye ulemavu wa
Ngozi albino pamoja na Vikongwe. Amesema, ikiwa jamii ya watu hao itapata
madhara basi ni dhahiri Mkuu huyo wa Wilaya atakuwa ameshindwa kusimamia
majukumu yake.
Mkuu huyo wa mkoa pia, amerudia kauli yake nakuwataka viongozi
hao wapya watambue wanajukumu zito lililoko mbele yao, ikiwa ni pamoja na
kukomesha Utumiaji wa dawa zakulevya.
Aidha ameonya uchezaji wa Pool na unywaji wa Pombe wakati wa saa
kazi, huku akimsisitiza mkuu wa Wilaya ya Nyamagana kuhakikisha ifikapo Agosti
mosi, suala la wafanyabiashara wanaofanya biashara kwenye maeneo ambayo
hayaruhusiwi liwe limepatiwa ufumbuzi.
Mongella amesema, katika mkoa wa Mwanza, Hotel na Clabu, yeyote
ile, iwe ya kawaida au ya Kitalii, ikibainika inafanya biashara ya Shisha,
hawataivumilia na badala yake wataifutia Leseni ya biashara.
Walio apa mbele ya Mkuu wa Mkoa, ambao waliteuliwa na Mhe. Rais
Tarehe 26, Juni, 2016 ni Emmanuel Enock Kipole, Mkuu wa Wilaya ya Sengerema,
Estomin Francis Chang’a Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe, Hadija Rashid Nyembo Mkuu wa
Wilaya ya Magu, wengine ni Juma Samwel Sweda Mkuu wa Wilaya ya Misungwi, Dkt.
Leonard Moses Masale Mkuu wa Wilaya ya Ilemela, Mary Onesmo Tesha Mkuu wa
Wilaya ya Nyamagana na Mhandisi Mtemi Msafiri Simioni Mkuu wa Wilaya ya Kwimba.
Imetolewa na
Atley J. Kuni
Afisa habari na Mahusiano
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa.
MWANZA.
04, Julai, 2016.
Thursday, June 30, 2016
Sunday, June 26, 2016
UTEUZI WA WAKUU WA WILAYA WAPYA
JAMHURI YA MUUNGANO WA
TANZANIA
KURUGENZI YA MAWASILIANO
YA RAIS IKULU
Simu : +255-22-2114512, 2116898
OFISI YA RAIS,
IKULU,
1 BARABARA YA BARACK OBAMA,
11400 DAR ES SALAAM,
TANZANIA
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 26 Juni, 2016 amefanya
mabadiliko madogo katika safu ya wakuu wa mikoa na amewateua wakuu wa wilaya
139.
Katibu Mkuu Kiongozi
Balozi John Kijazi amesema katika mabadiliko hayo Rais Magufuli amemteua
aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Sengerema Bi. Zainab R. Telack kuwa Mkuu wa Mkoa wa
Shinyanga.
Bi. Zainab R. Telack
anajaza nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bi. Anna
Kilango Malecela ambaye uteuzi wake ulitenguliwa.
Rais Magufuli pia
amemteua Dkt. Binilith Satano Mahenge kuwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma.
Dkt. Binilith Satano
Mahenge anajaza nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Bw.
Said Thabit Mwambungu ambaye amehamishiwa Ofisi ya Waziri Mkuu Dar es salaam
ambako atapangiwa majukumu mengine.
Aidha, Rais Magufuli
amemteua Dkt. Charles F. Mlingwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara.
Dkt. Charles F. Mlingwa
anajaza nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Stanslaus Magesa Mulongo ambaye uteuzi
wake umetenguliwa.
Wakuu wapya wa mikoa
walioteuliwa wataapishwa tarehe 29 Juni, 2016 saa tatu kamili asubuhi Ikulu
Jijini Dar es salaam na mara baada ya kuapishwa watakula kiapo cha maadili ya
uongozi.
Wakati
huo huo, Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 26 Juni, 2016 amefanya
uteuzi wa Wakuu wa Wilaya 139.
Katibu Mkuu Kiongozi
Balozi John Kijazi amesema katika uteuzi huo Rais Magufuli amezingatia mambo
kadhaa ikiwa ni pamoja na umri ambapo kwa wale ambao umri wao ni zaidi ya miaka
60 ameamua wastaafu.
Mhe. Rais amewashukuru
sana kwa utumishi wao mzuri na amesema pale ambapo itahitajika, serikali
itaendelea kuwatumia katika majukumu mengine.
Katika uteuzi huo, Wakuu
wa Wilaya waliopo sasa ambao wamebaki katika nafasi zao ni 39. Pia Rais
Magufuli amewateua Wakurugenzi Watendaji wa halmashauri 22 kuwa Wakuu wa Wilaya
kutokana na utendaji wao mzuri.
Aidha, nafasi 78 za
uteuzi wa Wakuu wa wilaya zimejazwa na watanzania wengine ambao wameteuliwa kwa
mara ya kwanza wengi wao wakiwa ni vijana, wenye elimu ya kutosha na uzoefu
katika maeneo mbalimbali.
Walioteuliwa kuwa wakuu
wa wilaya ni kama ifuatavyo (Orodha imepangwa kulingana na mikoa)
ARUSHA
1.
Arusha
- Mrisho Mashaka
Gambo
2.
Arumeru
- Alexander Pastory
Mnyeti
3.
Ngorongoro
- Rashid Mfaume
Taka
4.
Longido
- Daniel Geofrey
Chongolo
5.
Monduli
- Idd Hassan
Kimanta
6.
Karatu
-Therezia Jonathan
Mahongo
DAR ES SALAAM
1.
Kinondoni
- Ally Hapi
2.
Ilala
- Sophia Mjema
3.
Temeke
- Felix Jackson
Lyaviva
4.
Kigamboni
- Hashim Shaibu
Mgandilwa
5.
Ubungo
- Hamphrey Polepole
Subscribe to:
Posts (Atom)