BY NGUDU NYUMBANI BLOG
Baraza la Mitihani la
Tanzania (NECTA), limetangaza matokeo ya mitihani ya kujipima ya darasa la nne
huku matokeo hayo yakionyesha wanafunzi wengi wamefeli katika somo la
Kiingereza kwa asilimia 65.67 katika mitihani hiyo iliyofanyika mwishoni 2015.
Akitangaza matokeo hayo Jijini Dar es Salaam, Katibu Mtendaji wa Baraza hilo Dkt. Charles Msonde amesema juhudi za makusudi zinahitajika katika kuboresha mazingira ya ufundishaji na ujifunzia ili kuboresha kiwango cha ufaulu.
Jumla ya wanafunzi 869,057 kati ya wanafunzi 977,886 sawa na asilimia 88.87 waliofanya upimaji wamepata alama katika madaraja ya A,B,C, na D. Wanafunzi 108,829 sawa na asilimia11.13 wamepata alama za ufaulu usioridhisha.
Aidha wanafunzi wamefanya vizuri zaidi katika somo la Sayansi kwa asilimia 89.44, na baraza limewataka walimu kuweka mkazo zaidi kwa wanafunzi waliofanya vibaya ili wawasaidie kuimarika na waweze kupata ufaulu mzuri.

MATOKEO UPANDE WA
WILAYA YA KWIMBA
Kwa upande wa matokeo
hayo ya upimaji wa kitaifa darasa la nne, ambapo kuna jumla ya shule za msingi
151.
Baadhi ya Shule za
msingi zilizoongoza katika upimaji wa matokeo hayo ni kama ifuatavyo;
1. KINAMWELI PRIMARY SCHOOL
2. NG'WAMAKOYE PRIMARY SCHOOL
3. MWAKILYAMBITI PRIMARY SCHOOL
4. MWANG'HALANGA PRIMARY SCHOOL
Baadhi ya Shule zilizofanya vibaya katika upimaji
huo ni;
149. NG'WANG'HANGA PRIMARY SCHOOL
151. NG'WAMAPALALA PRIMARY SCHOOL
Matokeo yote upande wa wilaya yetu ya Kwimba unaweza
kuyapata kupitia link hii
>>>> MATOKEO
au ukiingia kwenye tovuti ya NECTA
No comments:
Post a Comment