RIPOTI
YA MWAKA JUU YA MAMBO YALIYOJIRI KWA HISANI YA NGUDU NYUMBANI BLOG
Hii ni ripoti
iliyojumuisha mambo mbalimbali ambayo blogu ya Ngudu nyumbani (www.ngudukwimba.blogspot.com)
ilipata kuyakusanya kwa mwaka huu kutoka vyanzo mbalimbali vya habari na watu
binafsi. Hivyo imepata kuyapanga mambo kwenye makundi kama yalivyoainishwa hapo
chini. Twende pamoja…
ULINZI
NA USALAMA
Katika hili mwenyekiti
wa kamati ya ulinzi na usalama wa wilaya ambaye ni mkuu wa wilaya ambapo chombo
cha ulinzi na usalama ndio washauri wake hivyo yeye ndiye mwenye jukumu kubwa
la kuhakikisha anafuatilia kwa ukaribu zaidi usalama wa raia wake. Ndani ya
mwaka huu kumepata kutokea matukio baadhi ambayo kwa namna moja au nyingine
hayakuleta picha nzuri kwenye jamii yetu.
1. Tukio la mkazi mmoja
wa ngudu kukutwa amefariki alipokuwa kwenye magereza kitu ambacho kilivuta
hisia za watu wengi ambapo kuna mambo kadhaa yaliendelea hapo baada ya kuzuka
sintofahamu juu ya kifo chake.
2.Pia tukio jingine ni
lile la mtoto mwenye ulemavu wa ngozi(Pendo Emanuel) kijiji cha ndamhi kata ya fukalo alipopotea kwenye mazingira ya
kutatanisha na kupelekea jeshi la polisi kuingilia kati kwa kufanya upelelzi na
msako mkali juu ya kupotea kwa mtoto huyo. Tukio hili lilitokea kati mwishoni
mwa mwaka jana na mwanzoni mwa mwaka huu.
ELIMU
(MATOKEO)
MSINGI-DARASA
LA SABA
Upande wa elimu naweza
kujikita zaidi katika matokeo ya shule zilizoongoza kiwilaya na zilizoshika
nafasi ya mwisho pia. Kwa upande wa shule za msingi
Kimiza primary school
inayopatikana kata ya lyoma iliongoza kati ya shule 151 katika wilaya, huku
ikiwa ya 30 kimkoa kati ya shule 900 na ya 126 kitaifa kati ya 16096. Ikumbukwe
kimiza primary ndiyo iliongoza hata kwenye matokeo ya mwaka jana
MATOKEO
KIDATO CHA 4
Mfumo mpya wa upangaji
wa matokeo kulingana na grade ulihusika mwaka huu. Baadhi ya matokeo ya shule
zilizojitahidi katika ufaulu yapo kama ifuatavyo;
Ngudu
sec
Distinction=2, merit=8,
credit=18, pass=39, fail=18
Bujiku
sec
distinction=2, merit=12,
credit=21, pass=38, fail=22
Nyamilama
sec
distinction=2, merit=7,
credit=17, pass=44, fail=34
**matokeo
ya form 2 pia yalihusisha mfumo mpya wa upangaji matokeo kwa grade
MATOKEO
YA KUJIUNGA NA KIDATO CHA 5
TAMISEMI; matokeo ya
kujiunga na kidato cha 5 yaliyotoka mwaka huu yakihusisha wanafunzi waliohitimu
kidato cha nne mwaka 2014 ambapo wilaya ya Kwimba ina jumla ya shule za
sekondari 28, ambapo 27 ni za serikali na 1 ya binafsi.
Sumve
girls sec school(private)
waliochaguliwa jumla=56
wavualana=0,
wasichana=56
Kwa shule za serikali, Bujiku sakila sekondari ndiyo iliongoza
kupeleka idadi kubwa(25) ya wanafunzi kidato cha 5, naya mwisho ni Bupamwa
sekondari iliyopeleka wanafunzi wawili na Mhande sec akipeleka wanafunzi watatu
tu..
Bupamwa
sec school
waliochaguliwa 2
wavulana =2,
wasichana=0
Bujiku
sakila sec school
Waliochaguliwa jumla=25
wavulana=16, wasichana=9
Shule nyingine
zilizofatia kwa kupeleka wanafunzi wengi ni Ngudu sec na Nyamilama ambapo
zilizopeleka wanafunzi 22 kila moja.
Pia katika hatua
nyingine NACTE katika hotuba yao juu ya kuvifuta usajili na kuvishusha hadhi
baadhi ya vyuo nchini, chuo cha afya, Ngudu School of Environmental Health
Sciences – Kwimba ni moja ya Taasisi na
Vyuo vilivyoshushwa hadhi baada ya kutotimiza masharti ya Ithibati ambapo (hadhi kabla ya notisi)-Ithibati ya
Awali, na (hadhi baada ya notisi)-Usajili wa Muda
TAKWIMU
MBALIMBALI
1. MAENEO YA UTAWALA KATIKA MAMLAKA ZA SERIKALI ZA MITAA (MAMLAKA ZA WILAYA MWAKA 2015 GN. 221 LA TAREHE 5/6/2015 )
Kupitia TAMISEMI
ilitolewa takwimu ya orodha ya mamlaka za wilaya zote nchini ambapo katika
wilaya ya Kwimba takwimu zilikuwa kama ifuatavyo;
Kata=30, vijiji=119, vitongoji=870
2. Makadilio ya idadi ya wapiga Kura wilaya ya kwimba (national bureau of
statistics)
Jimbo
la kwimba
Makadirio ya idadi ya
watu kwa mwaka 2015= 235,818.
Makadirio ya watu wenye
miaka 18 na zaidi= 102,763
Jimbo
la sumve
makadirio ya idadi ya
watu kwa mwaka 2015= 203,166
Makadirio ya watu wenye
miaka 18 na zaidi= 87,993
UKUAJI
WA TEKNOLOJIA
Katika secta hii
mitandao ya kijamii na vyombo vya upashaji habari ndio vinahusika. Ambapo kuna
baadhi ya blogu za kijamii zimepata kuanzishwa ndani ya mwaka huu
Ngudu
nyumbani blog
Jumla ya
machapicho(post) kwa mwaka huu ni 41
Jumla ya watembeleaji
kwenye blogu mpaka sasa=8085
Ngudu
nyumbani (facebook page)= like 251
Tatizo kubwa linakuja
pale ambayo wilaya inapokuwa haina Tovuti ya habari wala angalau blogu ambayo
inakuwa chini ya halimashauri ambapo taarifa za muhimu kama miradi ya
maendeleo, matangazo, maagizo, maazimio ya baraza la madiwani na mambo mengine
yangepatwa kuwekwa kule ili kuwapa uwezo wananchi kujua yanayoendelea kwenye
wilaya.
Katika hili NGUDU NYUMBANI BLOG ilipata kushauri wazo hili ambapo
mmiliki wa blogu alionana na uongozi wa halmashauri(DED) na kumwelezea, wazo
likapokelewa na kufikishwa kitengo cha Tehama na kushauri mhusika aandae
pendekezo(proposal) juu ya uendeshaji wa blogu hiyo.
Zoezi lilifanyika
pendekezo likaandaliwa na jinsi ambavyo mambo yatakuwa(kuanzisha blogu na
baadae kuwa na tovuti maalumu) lakini cha ajabu tangu kutumwa kwa mapendekezo
hayo(kwa barua pepe) mapema mwezi May mwaka huu hadi leo hakuna majibu yoyote
na hakuna jitihada zozote juu ya uanzishwaji wa tovuti wala nini, pengine ni kweli wazo halikuwa zuri kwao basi
jitihada za kulifikisha wazo hili na kufanyiwa kazi zilikomea hapo.
Ukiachana
na hilo kwenye tovuti ya mkoa(www.mwanza.go.tz)
kuna kiungo(link) ya Kwimbadc ambayo
kwa mwaka sasa ipo kwenye majaribio kitu cha ajabu sana hiki. Kwa wataalamu wa
IT wanajua tovuti inachukua siku 3 kukamilika(kuwa na domain name na kuwa
hosted) kwa blogu ni masaa kadhaa tu inakua hewani(blogu ni bure katika
kuifungua) lakini hili kwa wilaya yetu limekuwa janga.
Wadau wa maendeleo wenye
kujua umuhimu wa tovuti hizi wanaweza kusaidia kushauri pia kuanzia mwakani
tuanze na mambo mapya kwasababu najua kitengo cha Tehama kipo na kitengo cha
habari pia kipo wasisite kufanikisha hili(kumewahi kuwepo blogu ya wilaya miaka
ya 2012), na panapotokea kuhitaji msaada NGUDU NYUMBANI BLOG ipo kuwasaidia.
Katika upande wa blogs
pia kuna baadhi ya blogu zimeanzishwa mwaka huu lengo kuu ni kuhamasisha
maendeleo na kutoa taarifa husika.
1. KWIMBA KWETU (www.kwimbanyumbani.blogspot.com)
hii inajihusisha na miradi ya kimaendeleo hasa masuala ya elimu kwenye shule
zilizoko vijijini
2. NGUDU SCHOOL OF ENVIRONMENTAL
HEALTH SERVICE(www.nguduschool.blogspot.com)
hii blogu ikiwa maalumu kwa chuo cha afya japo bado haijawa na muonekano mzuri
mhusika anaweza wasiliana na ngudu nyumbani blog wakasaidiana katika hilo.
UCHAGUZI
MKUU
Katika uchaguzi mkuu
uliofanyika mapema mwezi octoba 25 mwaka huu
UBUNGE NA UDIWANI JIMBO
LA KWIMBA
Katika jimbo la kwimba
nafasi ya ubunge kulikuwa na washiriki wa5 kutoka vyama mbalimbali ambapo ndugu
Mansoor Shanif Hiran(CCM) alishinda na kutangazwa kuwa mbunge halali wa jimbo
hii ni mara ya pili mfululizo ambapo mwaka 2010 pia alishinda kiti hicho, akiwashinda wapinzani wake ndugu
Shilogela(CDM) na Otto(CUF).
Na kitu cha ajabu kidogo ni kuwa mgombea wa UDP ndugu Aloyce Iswalala Isanzu hakupata
hata kura 1 kwa jimbo zima
Kwenye nafasi ya
udiwani, jimbo la Kwimba lina kata 15 ambapo kata 14 walishinda CCM na kata
1(Ng’wangalanga) ikichukuliwa na CDM
UBUNGE NA UDIWANI JIMBO
LA SUMVE
Nafasi ya ubunge
ilikuwa na wagombea wa4, ambapo ndugu Ndassa Richard Mganga(CCM) alishinda na
kutangazwa kuwa mshindi katika uchaguzi huo huku akipata upinzani mkali kutoka
kwa ndugu Mchele(CUF) na Ng’holo(CDM)
Kwenye uchaguzi wa
madiwani ambapo jimbo la Sumve lina kata 15,
CCM alishinda kata 11, CDM kata 3 na CUF kata 1
UCHAGUZI VIONGOZI
HALMASHAURI YA WILAYA (M/KITI NA MSAIDIZI)
Katika baraza la
wawakilishi(madiwani) kulifanyika pia uchaguzi wa mwenyekiti wa halimashauri
ambapo baraza lilihusisha wajumbe 42.
Ambapo mchanganuo wake upo hivi; CCM
wajumbe 36(madiwani 14 kwimba, madiwani 11 sumve, wabunge 2, viti maalumu 9)
CDM ina wajumbe 4 + 1 viti maalumu jumla 5 na CUF ina mjumbe mmoja.
Katika
uchaguzi huo Ccm iliweza kuongoza na hivyo kuendelea kuiongoza halimashauri ya
wilaya ya Kwimba kwa awamu ya 5 mfululizo tangu kuanzishwa kwa mfumo wa vyama
vingi
MENGINEYO
1.
Kulifanyika uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura zoezi lililohusisha
mikoa na wilaya zote nchini
2. Taasisi ya kifedha
ya bayport financial service inayojihusisha na mambo ya mikopo kufungua tawi
kwimba mkoa wa mwanza
MWISHO
Ningependa kusikia
maoni, ushauri, marekebisho na kitu chochote juu ya report hii na blogu ya
Ngudu nyumbani kwa ujumla + page ya facebook(ngudu nyumbani) ili tuanze mwaka
mpya na mambo mapya.
Asanteni sana.
NGUDU NYUMBANI
nguduone@gmail.com
No comments:
Post a Comment