ALIYEWAHI kuwa
Mbunge wa Viti Maalumu kwa tiketi ya Chadema, Leticia Nyerere amefariki dunia.
Leticia
alifariki dunia katika Hospitali ya Doctors Community iliyopo Lanham, Maryland
jana (Tar 11 jan 2016) saa 2 usiku kwa saa za Afrika Mashariki, alikokuwa
amelazwa kwa matibabu.
Taarifa
za awali kutoka Marekani, ambako msiba huo umetokea, ziliarifu kuwa msiba upo
DMV 9004 Brightlea Court, Lanham, MD 20706.
Msemaji
wa familia hiyo, Mbunge wa zamani wa Chadema, John Shibuda alithibitisha
kutokea kwa msiba huo. Alisema ndugu wanajipanga kukutana na kuamua cha
kufanya.
“Ndugu
yangu ni kweli msiba umetokea wa mpendwa wetu Leticia Nyerere, umetokea jana
mchana huko Marekani na huku kwetu ilikuwa ni usiku, hivyo ndugu bado
hatujakutana na kuamua kwa pamoja ni wapi tuweke msiba na lini tutazika,”
alisema Shibuda.
Shibuda
alisema kuwa leo familia itatoa taarifa kamili ya taratibu zote za msiba huo
baada ya wanafamilia kukutana.
Magufuli
ampa pole Mama Maria Wakati huohuo, Rais John Magufuli jana alimtembelea na
kumpa pole mke wa Baba wa Taifa, Mama Maria Nyerere kufuatia kifo cha mkwewe,
Leticia Nyerere.
Pamoja
na kutoa mkono wa pole kwa Mama Maria Nyerere nyumbani kwake Msasani jijini Dar
es Salaam, Rais Magufuli pia amewapa pole wanafamilia wote na amewaomba kuwa
wavumilivu katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na ndugu yao.
Msemaji
wa familia ya Mwalimu Nyerere, Joseph Butiku alimueleza Rais Magufuli kuwa
familia inaendelea na taratibu za kuusafirisha mwili wa marehemu kutoka nchini
Marekani na itatoa taarifa baadaye.
Mwezi
Julai mwaka jana, Leticia Nyerere alijiondoa rasmi Chadema na kurejea Chama Cha
Mapinduzi (CCM).
Leticia
aliolewa na Madaraka Nyerere na kujaliwa kupata watoto watatu. Madaraka ni
mmoja wa watoto wa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere.
Hata
hivyo Leticia alitengana na Madaraka katika miaka ya mwisho ya 1990.
Chanzo: HABARI LEO
Update: kuzikwa tar 21 jan 2016 butiama mkoa wa Mara
No comments:
Post a Comment