MATOKEO YA KIDATO CHA PILI
Jumla ya wanafunzi 324,068 wa kidato cha pili sawa
na asilimia 89.12 ya wanafunzi 363,666
waliofanya mtihani wamefaulu kuendelea
na kidato cha 3 mwaka 2016.
Jumla ya watahiniwa 164,547 sawa na asilimia 89.00
ya watahiniwa wote wa kike waliofanya mtihani huo wamefaulu. Kwa upande wa watahiniwa wa kiume,
watahiniwa
159,521 sawa na asilimia 89.24 ya watahiniwa wote wamefaulu mtihani.
Huku
wanafunzi 39,567 sawa na asilimia 10.88 wameshindwa kukidhi viwango vya
kuwaruhusu kuendelea na kidato cha 3
Ufaulu umeshuka kwa baadhi ya masomo kama Uraia,
Historia, Jiografia, Kingereza, Fizikia, Biolojia, Hisabati na Book keeping
ukilinganisha na mwaka jana
Mikoa ya Mwanza, Dar es salaam, Mbeya na Iringa
ndiyo imetoa shulle 10 bora, huku shule 10 zilizofanya vibaya zikitoka katika
mikoa ya Tanga, Mtwara, Lindi na Dar es salaam.
MATOKEO YA NGUDU SEC NA BUJIKU SAKILA SEC
NGUDU SECONDARY SCHOOL
Shule ilikuwa na watahiniwa 103 ambao walitakiwa
kufanya mtihani wa kidato cha pili ambapo mpangilio wa madaraja (class) upo
kama ifuatavyo;
Distinction-4
Merit-12
Credit-18
Pass-53
Absent-6 (hawakufanya mtihani)
Referred-10 (waliorudia mwaka wa masomo)
-------------------------------------------------------------------------------------------------------
Repeater-7 (hawa ni wale waliokuwa wamerudia mwaka)
WALIOONGOZA
-
JONIA JULIAS WANJARA. Ana GPA ya 3.3, Class
ni MERIT (Upande wa wasichana)
-
ABDALLAH HEMED NG'OE. Ana GPA ya
5.0 Class ni DISTINCTION (Upande wa
wavulana)
BUJIKU SEC SCHOOL
Shule ilikuwa na watahiniwa 143 ambao walitakiwa
kufanya mtihani wa kidato cha pili ambapo mpangilio wa madaraja(class) upo kama
ifuatavyo;
Distinction-16
Merit-17
Credit-30
Pass-69
Absent-8
Referred-4
--------------------------------------------------------------------------------------------
Repeaters-25
WALIOONGOZA
-
DEVOTHA JERAD LUCAS. Ana GPA ya 4.4,
Class ni Distinction
-
HASSANI RAJABU HASSAN. Ana GPA ya 4.7,
Class ni DISTINCTION
-
PETER LAMECK YUMBU. Ana GPA ya 4.7, Class ni DISTINCTION
Matokeo yote ya kidato cha pili unaweza kuyapata
kupitia link hii http://necta.go.tz/matokeo/ftna2015/html/index.htm
au tembelea tovuti ya NECTA kwa maelezo zaidi.
Ukijaribu kulinganisha matokeo ya shule hizi mbili
utaona Bujiku Sakila wamefanya vizuri kuliko Ngudu sec. Hali hii imekuwa
ikijitokeza hata kwenye matokeo ya kidato cha 4, kwamba Bujiku wanaendelea
kuwazidi Ngudu sec katika ufaulu.
Ukichunguza zaidi unashindwa kujua sababu za kwanini
shule kongwe kama Ngudu inakuwa na muendelezo wa matokeo mabaya kuanzia form 2
na form 4 ukilinganisha na shule nyingine ambazo bado hazijawa na miundombinu
na rasilimali nyingi kama ilivyo kwa shule hii kongwe
Bado shule nyingi zimekuwa na changamoto nyingi hasa
za mazingira mazuri ya kusomea, walimu wa kutosha, upatikanaji wa huduma za
kijamii n.k. Mwishoni mwa mwaka jana tumeshuhudia walimu takribani 300(wa
msingi na sekondari) wakipanga kugoma kufundisha kama madai yao
hayajashughulikiwa.
Wanafunzi waliopata Merit, Credit na Pass wana kazi kubwa ya kufanya ili
kuhakikisha wanafanya vizuri kidato cha nne vinginevyo ndiyo tutaendelea
kuzalisha vijana wengi wasio na cha kufanya maeneo mengi ya wilaya yetu hasa ya
stend almaarufu kama SOKO MJINGA, kusinda wakitabiri matokeo(BETTING) ili siku
ziende. Na pengine wahusika wa elimu hawaoni kama kuna tatizo lolote katika
mfululizo wa matokeo mabovu haya,.
Mwaka huu tunaanza sera ya ELIMU BURE kuanzia darasa
la kwanza hadi kidato cha nne, japo sidhani kama inaweza kuwa bora kama kwanza
changamoto za miaka mingi zinazoikumba sekta hii hazijapatiwa ufumbuzi wa
kudumu.
NGUDU NYUMBANI
@2016
No comments:
Post a Comment