BY NGUDU NYUMBANI BLOG
05/04/2016.
(SEHEMU YA KWANZA)
KATIKA maisha, hali ya kujiamini juu ya kile
unachokifanya na kukifanya kwa utashi na utulivu mkubwa ndiyo silaha muhimu
kuelekea mafanikio. Licha ya kujiamini ni lazima kukubaliana na matokeo kwa
kukubali changamoto zinazokukabili na kujua namna bora ya kuzikabili ili usonge
mbele.
Leo nimeamua kuwakumbuka baadhi ya ndugu zangu hasa
kwenye tasnia ya sanaa kwa ujumla wake. Nimejaribu kuwazungumzia vijana baadhi
waliojihusisha na sanaa hasa ‘wasanii’ kipindi cha nyuma. Ambapo wengi wao walifanya kama hobby(kwa
kipindi hicho baadae wakaachana nayo) na wengine waliwekeza muda mwingi
kuhakikisha wanaendelea na utaratibu huo na leo tunawatambua kama wasanii.
Nakumbuka kipindi hicho, vijana wengi walikuwa
wanapenda hasa kuimba. Jamaa zangu, Omary
Kigoda na Juma Damas( mwenyezi amlaze mahala pema) walikuwa ni watu wa kuandika mashairi mara
kadhaa ila changamoto ilikuwa namna ya kupata au kuvifikia vyombo vya kurekodia
mashairi hayo, kipindi hicho hapakuwa/hawakuwa na simu za kurekodi japo sauti
kama ilivyo leo. Mbali na kuimba bwana omary alipenda kuigiza pia.
Kwa sasa Omary licha ya kuwa mtumishi wa serikali
lakini anajihusisha na sanaa pia(kuigiza na kuandaa filamu), ambapo amehusika
kwenye baadhi ya filamu ikiwemo ‘MADNESS’ iliyopo sokoni kwa sasa unaweza kuitafuta na
kuitazama. Mdogo wake pia msharo (Shaban) ni msanii anayewakilisha kundi la THE
WINNERS ambapo naye amepata kufanya kazi kadhaa ikiwemo ‘Bolingo nangaye’ akimshirikisha Man M the winner. Video yao na video nyingine
unaweza kuzipitia HAPA
Kipindi hicho
wasanii wakubwa walikuja kutoa
burudani wilayani katika kumbi tofauti enzi hizo ‘Safari club’ na KWIDECO ndio
zilitumika zaidi. Wasanii kama Inspecta haroun(Babu), Bwana misosi, Mzee wa ‘mashikolo mageni(jina nimesahau)’ na
wengine wengi walitumbuiza. Sikupata kuwapo katika show ya Inspecta Haroun
ambapo ilitokea vurumai kubwa ikisemekana kwamba hakuwa yeye bali ni jamaa tu
aliyekuwa akicheza ‘Track’ na kufatiliza na sio kuimba Live kama wanavyofanya
wengi kwa kuwekewa mdundo tu.
Ni kipindi ambacho watu kama Cosmas Kulwa(CK) na
wenzie kipindi wapo Ngudu sekondari
walionekana kufanya mziki na kukubalika na wengi. Sina kumbukumbu nzuri
kama Dickson Philipo na sullu cosmas nao walihusika pamoja na CK wakati huo. CK
aliendelea na kujihusisha na mziki ila wenzie walijihusisha kwa muda na kuacha
pengine sababu ya majukumu mengine waliyokuwa nayo.
Ni kipindi hicho ambapo Storyteller Rhymes au ‘Aron
Deus’, au ‘Mboni’ na wengine tulipenda
kumwita ‘Mwibonya’. Enzi izo akiwa Ngudu sec kwenye sherehe kama Graduation na
nyinginezo alipata kuonesha uwezo wa kuFlow kwa aina yake, mziki wa hip hop.
Alikuwa na uwezo wa kuandika mashairi yenye vina na kuyaimba kwa namna
iliyowavutia wengi. Sina hakika kama anaendelea na kufanya mziki licha ya kuwa
na kipaji cha kucheza mpira wa miguu pia. Nilipata kusikiliza wimbo wake mmoja,
japo sina hakika na pengine kumbukumbu sahihi
ya nyimbo alizowahi kurekodi na kama anaendelea kujihusisha nao mpaka
leo.
Kuna vijana wengine wengi pia walikuwa wakiimba
kipindi hicho, PUNGU na wadogo zake ni mfano mzuri kwa wanaolifahau jina hili.
Pia Igo Lyric Re-chird au ‘Richard’, akiwakiwakilisha vizuri kutoka pande za Welamasonga
. Japo hata sasa bwana Igo lyric anaonekana kama kujihusisha na mziki licha ya
kuwa mwanafunzi wa chuo.
Ni kipindi hicho ambapo ‘Dj Jigga’ akifanya vizuri
zaidi kutoa burudani murua pande za Kwideco(akishirikiana vizuri na jamaa zake
Masuka na Edo). kulikuwepo na ma DJ
wengi kipindi hicho pengine nisiweze kuwakumbuka wote. Baadae akaja DJ
Kisandu kabla ya kuachana na kazi hiyo
na kujihusisha na kazi nyingine. Vijana kadhaa walipata kuvutiwa na kazi hii
wakiwemo DJ SOLEJI, DVJ COLINE na wengine wengi ambao wengi wao wanaendelea na
kazi hiyo hadi leo.
Raymond akiwakilisha toka pande za kwa ‘madiba’ au
Ngudulugulu kama inavyofahamika kwa wengi. Huyu nae alikuwa anapenda kuimba
tangu yupo shuleni. Japo maisha yanaenda kwa kasi sina hakika kama bado anaendelea
nao au ilikuwa ni uchakaramu wa shuleni
tu enzi hizo. Mtu kama FREDRICK MASHUDA katika ubora wake wa kutangaza na sauti
yake nzito ile kipindi hicho ilikuwa burudani ya aina yake.
Bwana mdogo ‘Physical GoldChain’ au kwa jina jingine
Danny Sayi, nae hakuwa nyuma kipindi hicho kwenye kuimba. Pengine
Ukiachana na waliokuwa wakiimba, kuna waliokuwa
wanacheza hasa mziki wa Dancehall, kundi hili lilikuwa na vijana wengi baadhi
yao ni Shirugu, Tunda(kulwa & dotto), Dome, na wengineo ambapo kuna kipindi
walivuma sana kiasi cha kuvutia vijana wengi kupenda kucheza pia. Ndio kipindi
hicho sherehe za kuzaliwa(birthday) zikifanyika kwa wingi sana ama ukumbi ukiwa
nyumbani kwa mwenye sherehe au mara kadhaa ukumbi wa ‘Chuo cha afya’, KWIDECO
au Safari Club na kwingineko.
HALI ILIVYO KWA SASA.
Maisha yanaenda kasi sana kiasi cha umri kwenda na
kila mmoja kuwa na majukumu yake. Kuna
ambao wanatambulika kama wasanii kwa sasa na wengine walikomea enzi hizo na kwa
sasa kila mmoja ana ‘mishe’ zake. Baadhi ya wanaotambulika na kujulikana kwa
wengi;
LEDDY CHOMBO(RED MAN)
Wengi wetu tunamfahamu huyu jamaa na amewahi fanya
nyimbo nyingi. Sina kumbukumbu vizuri lakini nakumbuka aliwahi kutoa Album na
kuizindua pale KWIDECO miaka ya 2007 au 2008 hivi. Mpaka sasa anafanya mziki
japo kwa upande wangu naona sio kwa kasi kama aliyokuwa nayo kipindi kile cha nyuma. Mwezi wa pili mwaka huu alitoa wimbo
‘Happy Birthday’ bila shaka wengi wetu mliusikia. Pia kwa kiasi Fulani anajihusisha
katika kutayarisha muziki pia.
STAR JAY
Huyu pia ni zao la Kwimba ila kwa kiasi kikubwa kazi
zake za muziki anazifanyia Dar es salaam. Naambiwa pia licha ya kuimba, anaweza
kutengeneza beat(producer). Mzee wa zidisha makopa na Good time. Nilikuwa
namsikia mara kadhaa ila nilimsikia katika ubora wake kwenye uzinduzi wa album
ya Leddy Chombo ambapo alikuwa akimpa support. Unaweza kusaka nyimbo zake zipo
mtandaoni kwa wale wasiomjua.
CK
Huyu brother licha ya kufanya shughuli nyingine
zinazomwingizia kipato pia anaendelea kufanya mziki. Nimepata kuongea nae mara
kadhaa changamoto yake kubwa ikiwa ni namna ya kurekodi mziki wake na
kuusambaza uufikie umma kwa haraka na urahisi. Kipindi ambacho leddy anafanya
vizuri na kusikika kwa kasi ndipo hata CK nae alikuwa ‘hot’ vile vile.
JOE DASUKUMA
Kwa wale waliopo kwenye groups za facebook bila
shaka wamewahi kuona akijinasibu mara kadhaa. Kuna wimbo wa ‘ONE DAY’ amepata
kufanya. Simfahamu vizuri lakini inatosha kwa namna ambavyo anavyotoa updates
za kazi zake anazofanya. Anaweza kama akiwepa muda wakusikilizwa na kupata
support inayostahili, bila shaka nyota yake itang’aa zaidi.
DOGO SILVER
Kama yeye jinsi anavyojiita au unaweza mwita MABEYO,
uchakaramu wake ulianza kuonekana tangu yupo shuleni hasa pale NGUDU sekondari.
Katika harakati za kutaka kutoka na kufanya anachoamini kinaweza kumtoa.
Amefanikiwa kutoa nyimbo kadhaa mojawapo akimshirikisha PNC(shino) kwenye wimbo unaoitwa ‘Ukweli wa
mambo’(unaweza kuutafuta mtandaoni ukaupa nafasi kwenye masikio yako).
Aliwahi kuwa
na mpango wa kufanya Track na Ommy dimpoz kipindi cha nyuma lakini sijui nini
kilimkwamisha pengine. Kwa sasa naambiwa analitumikia jeshi la wananchi hivyo nafasi
yake kujihusisha na masuala ya muziki ni ndogo sana.
WENGINEO MBALI NA KUIMBA.
LUCY CHARLES
Huyu ni mwana mitindo mzawa wa Kwimba, ni binti
mrembo na msomi pia. Amewahi kushinda mataji kadhaa huko nyuma kama MISS MWANZA
na MISS LAKE ZONE. Kwa sasa anajishughulisha zaidi na masuala ya mitindo pamoja
na shughuli nyingine.
Kupitia huyu
vijana wengi(wakike) wanaweza kuvutiwa na kuwa inspired na kile anachokifanya
endapo tu watautambua mchango wake na msaada wake katika kuwasaidia njia kwa
wale wenye lengo la kuwa kama yeye na zaidi. Binafsi siwezi kuelezea mchango
wake, zaidi ya kujivunia kuwa na mtu
kama yeye kwenye jamii yetu.
Blogu yetu kupitia HAPA ilipata kuweka picha zake kama kutambua
anachokifanya pia. Unaweza kufungua link hiyo kuziona hasa kwa wasiomjua.
KING SUKA.
Huyu kaka mkubwa yupo kwenye tasnia ya filamu kama
mwigizaji na muongozaji ambapo amehusika
kwenye filamu kadhaa. Pia ni mmiliki wa blogu ya kijamii KING OF NEWS
Kupitia yeye , anaweza saidia vijana wengi nyuma
yake njia sahihi za kufuata na hatimaye kutoka kupitia tasnia hiyo ya filamu na
uigizaji. Na imani analijua hilo na analifanya kwa ustadi mkubwa kusaidia
wengine katika sanaa.
Hawa ni baadhi ya ninaowafahamu na kuwasikia
wakifanya mambo yao kwenye tasnia ya sanaa kwa ujumla. Pengine wapo wengine
wengi ambao siwajui lakini mmojawapo miongoni mwetu akawa anawajua na taarifa
zao anaweza kutujuza pia.
Kila mmojawetu ana jukumu kubwa la ku-support hawa
watu na wengine kwenye tasnia ya sanaa ili kuwafanya waendelee kufanya vizuri.
Pia wao nao kila mmoja wao kwa nafasi yake anapaswa
kujua jamii iliyomzunguka inataka nini kwake. Pia tunategemea mchango wao mkubwa kwenye ujenzi wa jamii yetu pia.
Ningependa kuweka sawa kitu kimoja kwamba, kwa
asilimia kubwa hao niliowazungumzia wanatokea kata ya NGUDU, japo kama wilaya
tuna kata 30 hivyo naamini watakuwepo wengine wengi.
Itaendelea sehemu ya pili siku nyingine kulingana na
mahitaji na mapendekezo ya wadau….
Tafakari!
KWIMBA TUITAKAYO
nguduone@gmail.com
No comments:
Post a Comment