Richard Ndasa, mbunge wa jimbo la SUMVE |
RICHARD Ndasa,
Mbunge wa Sumve, (CCM) amepandishwa kizimbani katika mahakama ya Hakimu
Mkazi Kisutu kujibu shtaka la tuhuma ya kuomba rushwa ya Shilingi milioni 30,
Akisoma mashtaka hayo wakili wa Taasisi ya
Kuzia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Denis Lukayo mbele ya hakimu, Amilisi
Mchaura amesema kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo akiwa kama mjumbe wa Kamati
ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma.
Amesema
kwamba mbunge huyo anatuhumiwa kwa kosa la kuomba Rushwa kwa Mkurugenzi wa
Shirika la Umeme (Tanesco), Felichesmi Mramba ila amsaidie kuandika mapendekezo
safi ya shirika hilo.
Mbunge
huyo anakuwa wa nne kupandishwa kizimbani kwa kosa la rushwa ambako tayari jana
walipandishwa wengine wa Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) ambao ni
Ahmad Saddiq (53) mbunge wa Mvomero, Kangi Lugola (54) mbunge wa Mwibara na
Victor Mwambalaswa (63) mbunge wa Lupa.
Kutokana na uchunguzi
unaoendelea upo uwezekano wa wabunge zaidi kufikishwa mahakani kujibu tuhuma
hizo ambazo zimetikisa taasisi ya Bunge ambacho ndicho chombo kikuu cha kutunga
sheria.
Mbunge
huyo alifikishwa majira ya saa mbili asubuhi huku idadi kubwa ya watu wakiwa
wamefurika kushuhudia kesi hiyo ambayo imekuwa na mvuto kwa wananchi wengi wa
jiji la Dar es Salaam.
Baada
ya kusomewa mashtaka hayo mbunge Ndasa alikana kutenda kosa hilo ambako upande
wa serikali ulisema upelelezi bado unaendelea.
Chanzo: MWANAHALISI
No comments:
Post a Comment