TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Mwanza, tarehe 21/04/2016 imemfikisha mahakamani Afisa Mtendaji wa kata ya Mwakilyambiti wilaya ya Kwimba BW. BONAVENTURA LUPILYA MAKUNGU(46) kwa kosa la kuomba hongo ya shilingi laki tatu (300,000/=) na kufanikiwa kupokea shilingi (190,000/=) kutoka kwa JOHN MASHOMALI LUKUNGU(45).
Afisa mtendaji huyo aliomba pesa hiyo ili
aweze kumpatia dhamana ndugu wa bwana
JOHN MASHOMALI LUKUNGU(45), Bi LUCIA SOBOLA JANELA ambaye yeye kama mlezi alikamatwa kwa kosa la utoro wa mwanafunzi LUCIA MABULA JOHN.
JOHN MASHOMALI LUKUNGU(45), Bi LUCIA SOBOLA JANELA ambaye yeye kama mlezi alikamatwa kwa kosa la utoro wa mwanafunzi LUCIA MABULA JOHN.
Mtuhumiwa BW. BONAVENTURA LUPILYA MAKUNGU
alitenda kosa hilo la kuomba na kupokea hongo mnamo tarehe 26/02/2016 ambapo ni
kinyume na kifungu cha 15(1a) cha sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Namba
11/2007.
Mashtaka hayo yamefunguliwa katika Mahakama
ya Wilaya ya Kwimba na Mwendesha Mashitaka wa TAKUKURU Bw. JOVINE MAJURA
ambapo yamesajiliwa kwa shauri la jinai namba 39/2016 na liko mbele ya
Mheshimiwa Hakimu BONAVENTURA LEMA.
Akisomewa shauri hilo mbele ya Hakimu,
Mtuhumiwa BW. BONAVENTURA LUPILYA MAKUNGU(46) alikana shtaka hilo na yuko
nje kwa dhamana hadi shauri hilo litakapotajwa tena tarehe 24 Mei, 2016.
Wakati huohuo TAKUKURU Mkoa wa Mwanza pia
inatarajia kumfikisha mahakamani Afisa Afya na Mazingira Bw. SOSPETER
JACOB SELEWA (29) wa kata ya Buswelu iliyopo Halmashauri ya Manispaa ya
Ilemela, kwa kosa la kuomba rushwa ya shilingi Laki 100,000/= kutoka kwa Bi.
LYDIA JULIUS TAMBILIJA ambaye ni mmiliki wa kituo cha kulelea watoto
kinachofahamika kwa jina la JITAMBUE.
Afisa Afya huyo aliomba pesa hiyo ili
aweze kufungua kituo hicho cha kulelea watoto ambacho awali alikifunga
kwa vile kituo hicho hakikuwa na baadhi ya sifa zinazostahili.
Imetolewa Tarehe
22/042016 na ERNEST MAKALE, Mkuu wa TAKUKURU(M)
No comments:
Post a Comment