Thursday, February 5, 2015
Monday, February 2, 2015
KUHUSU SERIKALI ZA MITAA
Utawala wa Kijiji ni miongoni mwa tawala katika serikali za mitaa za Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania. Huu ni utawala wa chini
kabisa kimuundo ukitanguliwa na utawala wa Kitongoji. Kuwa utawala wa chini haimaanishi kuwa na umuhimu
mdogo, isipokuwa ni kupitia utawala huu ndiko ambako mambo mengi yanayoamuriwa
au kupangwa na tawala za juu kama serikali, hutekelezwa. Utawala wa kijiji
huelekeza wananchi katika kutumia madaraka yao ya kidemokrasia kuamua juu ya
mambo yanayowahusu kama wanakijiji moja kwa moja bila kupitia mlolongo au urasimu mrefu. Mambo yanayohusiana na tawala za serikali za
mitaa yanaratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu.
Saturday, January 24, 2015
RAIS KIKWETE KAFANYA MABADILIKO KWENYE BARAZA LA MAWAZIRI
Katibu
mkuu kiongozi, Balozi Ombeni sefue akizungumza na vyombo vya habari jioni hii wakati
akitangaza mabadiliko madogo ya baraza la mawazili, Ikulu jijini Dar es salaam
Rais wa
jamhuri ya muungano wa Tanzania, Dkt Jakaya Mrisho Kikwete leo amefanya
mabadiliko madogo katika Baraza lake la mawaziri, ambalo Ameliapisha jioni hii
Ikulu jijini Dar es salaam
Hayo
yamefanyika ikiwa ni baada ya aliyekuwa waziri wa Nishati na Madini kujiuzulu
wadhifa wake
Hawa ndiyo Mawaziri 8
walioteuliwa na rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete leo
1.George Simbachawene- Waziri wa Nishati na Madini
2.Mary Nagu -Waziri wa nchi Mahusiano na Uratibu
3.Harrison Mwakyembe - Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
4.Wiliam Lukuvi - Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi
5.Steven Wassira - Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika
6.Samwel Sitta - Waziri wa Uchukuzi
7.Jenista Mhagama - Waziri wa Sera na Uratibu wa Bunge
8.Christopher Chiza- Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji na Uwezeshaji
1.George Simbachawene- Waziri wa Nishati na Madini
2.Mary Nagu -Waziri wa nchi Mahusiano na Uratibu
3.Harrison Mwakyembe - Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
4.Wiliam Lukuvi - Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi
5.Steven Wassira - Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika
6.Samwel Sitta - Waziri wa Uchukuzi
7.Jenista Mhagama - Waziri wa Sera na Uratibu wa Bunge
8.Christopher Chiza- Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji na Uwezeshaji
Manaibu Waziri 5 walioteuliwa
1.Steven Masele - Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano
2.Angellah Kairuki - Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Makazi
3.Ummy Mwalimu- Naibu Waziri wa Katiba na Sheria
4.Anna Kilango- Naibu waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi
5.Charles Mwijage - Naibu Waziri wa Nishati na Madini
Thursday, January 22, 2015
Saturday, January 17, 2015
MATOKEO YA KIDATO CHA PILI
Baraza la mithani nchini limetangaza matokeo ya kidato cha pili yaliyofanyika mwaka 2014 huku idadi kubwa ya wanafunzi wakiwa wamefaulu na kujiunga na kidato cha tatu, ikiongezeka kwa asilimia 92.66 ikilinganishwa na mwaka 2013 ambapo idadi ya wanafunzi waliofaulu ilikuwa asilimia 89.34 matokeo hayo yametangazwa leo jijini Dar es salaam na katibu Mkuu wa Baraza la Mitihani nchini NECTA Dr Charles E Msonde wakati wa mkutano na waandishi wa habari ambapo alisema watahiniwa waliofanya mtihani huo uliofanyika novemba mwaka jana ilikuwa 405,204 sawa na asilimia 89.40. Kati ya hao wasichana walikuwa 233.834 sawa na asilimia 51.60 na wavulana walikuwa 219.357 sawa na asilimia 48.40
Dkt Msonde alisema kati ya watahiniwa hao waliofaulu na kupata alama za kuweza kuendelea na kidato cha tatu walikuwa 375,434 sawa na asilimia 92.6 ya watahiniwa wote waliofanya mtihani huo ambapo wasichana walikuwa 195,328 sawa na asilimia 92.8 na wavulana 180106 sawa na asilimia 92.69
Aidha Dokta Msonde aliwataja watahiniwa ambao wamepata alama ambazo hawawezi kuendelea na kidato cha tatu na itawalazimu kurudia kidato cha pili ambapo wapo 29770 sawana asilimia 7.34
Vilevile ameyataja masomo waliyofanya vizuri watahiniwa hao ni uraia, historia, kiswahili, kingereza na jeografia. Pia kwa masomo walifanya vibaya ni Hisabati, Kemia, kilimo, somo la biashara pamoja, fizikia pamoja na jeografia.
Kwa upande wa shule za
wilaya yangu, hasa za mjini hapo ambazo ni pamoja na NGUDU SECONDARY SCHOOL na
BUJIKU SAKILA kuna baadhi ya matokeo ya wanafunzi waliofanya vizuri zaidi kama inavyooneshwa hapo chini kwenye
majedwali
Wednesday, January 7, 2015
Mkuu wa mkoa wa Mwanza atoa siku tano kwa wanakijiji kwimba kuhakikisha wanampata mtoto Albino Aliyetekwa tangu Disemba 27, 2014
Mkuu wa mkoa wa Mwanza Magesa Mulongo
ametoa muda wa siku tano kwa wakazi wa kijiji cha Ndami na jeshi la jadi
Sungusungu wilayani kwimba, kuhakikisha wanampata mtoto mwenye ulemavu wa ngozi
– Alibinism, Pendo Emanuel akiwa hai au amekufa ikiwa ni pamoja na wahusika wa
tukio hilo kukamatwa na kufikishwa katika vyombo vya dola.
Agizo hili la mkuu wa mkoa wa Mwanza Magesa Mulongo,
linakuja kufuatia watu wasiojulikana kumuiba mtoto Pendo Emanuel mwenye ulemavu
wa ngozi majira ya saa 4 usiku Desemba 27 mwaka jana nyumbani kwao katika
kijiji cha Ndami na kutoweka naye kusikojulikana, mkasa ambao umeilazimu kamati
ya ulinzi na usalama ya mkoa wa Mwanza kuapa kuwa serikali haitalala usingizi
mpaka mtoto huy mwenye umri wa miaka minne apatikane.
Mwenyekiti wa chama cha watu wenye ulemavu wa ngozi
mkoa wa Mwanza Alfred Kapole amesema kuwa miongoni mwa kesi 72 zilizokuwa
mahakamani zikihusu mauaji ya walemavu wa ngozi, ni kesi tatu ndizo
zilizotolewa hukumu mpaka sasa, huku akiilaumu ofisi ya mkemia mkuu wa serikali
pamoja na mahakama kwa kuchelewesha kesi hizo.
Mama mzazi wa mtoto Pendo, Bi. Sophia
Juma pamoja na mkurugenzi wa shirika lisilokuwa la kiserikali la Chiriko Bi.
Specioza Kasoli wamesema kila mtu ana haki ya kuishi na kulindwa na kuongeza
kwamba mtoto huyo ni kati ya watu 74 wenye ulemavu wa ngozi wilayani kwimba na
alikuwa ni mtu wa 9 kwa kupatiwa ulinzi.
Kamanda wa Polisi mkoani Mwanza
Valentino Mlowola amesema tayari askari polisi wamepiga kambi katika kijiji
hicho kwa kazi moja tu ya kuhakikisha mtoto huyo anapatikana, lakini pia
watuhumiwa wanasakwa kwa udi na uvumba ili wafikishwe mahakamani kwa kosa la
jinai.
Tuesday, January 6, 2015
ZIFAHAMU SIFA, MAJUKUMU YA DIWANI WAKO, KISHA JITOKEZE KULETA MABADILIKO KWENYE JAMII YAKO.
Diwani
ni mwakilishi aliyechaguliwa kusimamia utekelezaji wa majukumu ya Serikali za
Mitaa. Madiwani ndio wanaounda
Halmashauri za Serikali za Mitaa na ndio wenye mamlaka ya kutekeleza majukumu
ya Serikali za Mitaa. Sheria
za Serikali za Mitaa zimeainisha majukumu ya kutekelezwa na Mamlaka hizi kuwa
ni ya kuwaletea wananchi maendeleo kwa kuwapatia huduma bora na kwa gharama
nafuu. Majukumu hayo ya Serikali za Mitaa ni haya yafuatayo:
i.
Kulinda na kutunza utulivu na amani na kusimamia Utawala
Bora;
ii. Kuendeleza ustawi wa jamii na kuinua uchumi wa wananchi
wake ikiwemo kuimarisha afya, elimu, utamaduni, burudani na ustawi wa wananchi
wake;
iii.
Kuhakikisha maendeleo ya kiuchumi na kijamii yanapatikana
kwa mujibu wa Sera za Taifa za Maendeleo Mijini na Maendeleo Vijijini;
iv.
Kuhakikisha na kuchukua hatua zozote zinazofaa katika
kuzuia au kuondoa uhalifu na kulinda watu pamoja na mali zao;
v.
Kuimarisha na kuendeleza kilimo, viwanda na biashara;
vi.
Kuuondoa umaskini na kero nyingine katika jamii hususan
kwa kuzingatia makundi ya vijana, wazee na walemavu wa aina mbalimbali na wale
wasiojiweza;
vii.
Kuhimiza dhana ya ushirikishwaji wa wananchi, vyama vya
hiari na visivyo vya hiari katika kujiletea maendeleo;
viii.
Kubuni vyanzo mbalimbali vya mapato vya kuwezesha
Halmashauri kutekeleza majukumu yake niliyoyataja hivi punde.
Hayo ndiyo majukumu ya Serikali za
Mitaa ambayo msimamizi mkuu katika halmashauri ni Diwani.
Subscribe to:
Posts (Atom)







