Mkuu
wa mkoa wa Mwanza Mh. Magessa Mulongo
jana kwenye uwanja wa CCM Kirumba akifungua mashindano ya Taifa ya vijana umri
chini ya miaka 13
Akifungu mashindano hayo Mh Mulongo amewataka vijana
hao kujituma katika michezo na masomo kwa kuwa vyote vinakwenda sambamba
Amesisitiza shirikisho la mpira Tanzania TFF
kuongeza juhudi katika kuendeleza soka la vijana
Katika salamu zake za utangulizi Rais wa TFF Jamal
Malinzi ameeleza kuwa lengo la mashindano hayo ni kuibua timu ya vijana wenye
umri wa miaka 13 ambao watahamishiwa kwenye shule ya Alliance, watakuwa hapo
kusoma na kufundishwa mpira.
Mpango wa TFF ni kuwa hadi kufikia mwaka 2019 timu
hii itakuwa imara kuiwakilisha Tanzania katika mashindanoya fainali za Afrika
umri chini ya miaka 17, fainali ambazo zitafanyika Tanzania
Mikoa yote 25 ya Tanzania bara inashiriki mashindano
haya na mkoa wa Dar es salaam umewakilishwa na timu tatu Kinindoni, Ilala na
Temeke.
TFF inashukuru Symbion power kwa ushirikiano wa
kuendeleza mpira wa vijana
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA(TFF)
No comments:
Post a Comment