BY NGUDU NYUMBANI BLOG
12/02/2016
WILAYA ya KWIMBA ni moja kati ya wilaya 7 zinazounda mkoa wa
MWANZA. Katika sensa ya mwaka 2012, idadi ya wakazi wa wilaya ya KWIMBA
ilihesabiwa kuwa 406,509. Pia makadirio ya idadi ya watu kwa mwaka 2015 takwimu
zinaonesha majimbo mawili yanayopatikana wilaya ya KWIMBA yana jumla ya
wakazi 438,984 ambapo jimbo la Kwimba ni 235,818 na Sumve ni 203,166.
Nimejaribu kuandaa majedwali yanayohusisha sensa ya mwaka 2012,
pia makadirio ya idadi ya watu mwaka 2015 kwa majimbo ya KWIMBA na SUMVE kama
ifuatavyo;
WILAYA
|
JIMBO
|
KATA
|
SENSA YA MWAKA
2012
|
MAKADIRIO YA IDADI YA WATU 2015
|
KWIMBA
|
KWIMBA
|
MWANG’HALANGA
|
11, 099
|
11,986
|
NYAMILAMA
|
7,
611
|
8,219
|
||
MWAKLYAMBITI
|
16, 079
|
17,364
|
||
HUNGUMALWA
|
16,
508
|
17,
827
|
||
MWAMALA
|
10, 582
|
11,427
|
||
KIKUBIJI
|
22, 032
|
23,792
|
||
MHANDE
|
19, 629
|
21, 197
|
||
BUPAMWA
|
17,366
|
18,753
|
||
FUKALO
|
17,534
|
18,935
|
||
NG’HUNDI
|
9,255
|
9,994
|
||
IGONGWA
|
11,705
|
12, 640
|
||
NGUDU
|
27,630
|
29,837
|
||
MWANKULWE
|
9,495
|
10,254
|
||
ILULA
|
11,966
|
12,
922
|
||
SHILEMBO
|
9,882
|
10, 671
|
WILAYA
|
JIMBO
|
KATA
|
SENSA YA MWAKA
2012
|
MAKADIRIO YA IDADI YA WATU 2015
|
KWIMBA
|
SUMVE
|
WALLA
|
17,190
|
18,563
|
BUNGULWA
|
10,361
|
11,189
|
||
SUMVE
|
16,436
|
17,749
|
||
NGULLA
|
12,692
|
13,706
|
||
MWABOMBA
|
10,096
|
10,903
|
||
MWAGI
|
11,325
|
12,230
|
||
ISENI
|
10,349
|
11,176
|
||
NYAMBITI
|
13,731
|
14,828
|
||
MALIGISU
|
20,788
|
22,449
|
||
MWANDU
|
11,132
|
12,021
|
||
MALYA
|
15,437
|
16,570
|
||
LYOMA
|
12,
561
|
13,564
|
||
BUGANDO
|
7,173
|
7,746
|
||
NKALALO
|
7,266
|
7,
846
|
||
MANTARE
|
11, 599
|
12, 526
|
wilaya ya KWIMBA ina Ukubwa wa eneo la nchi kavu 3903km ambapo
Asilimia za eneo kwenye mkoa ni 15.5
Wilaya ya Kwimba inaundwa na tarafa tano ambazo ni Ngudu, Nyamilama, Mwamashimba, Ibindo na Ngulla. Tarafa 2
zikiwa jimbo la Sumve na 3 jimbo la KWIMBA.
Wilaya pia ina kata 30, vijiji 119 na vitongoji 870. Hii ni
kulingana na takwimu za TAMISEMI mwaka 2015.
UZALISHAJI NA MAPATO
Makusanyo ya mamlaka za serikali za mitaa kwa wilaya ya Kwimba
kuanzia mwaka 2005 mpaka june 2015 kuna ongezeko la asilimia 128, ambapo
kupitia ongezeko hilo la ukusanyaji wa mapato ndipo kunakuwa na ongezeko la
wigo wa utoaji huduma kwa wananchi.
Katika hili wataalamu wa uchumi wanaweza kutusaidia kueleza kama
mapato haya yanatumika ipasavyo kuongeza utoaji bora wa huduma kwenye wilaya
yetu.
Kweny upande wa kilimo, uzalishaji wa zao la pamba umeshuka
kutokana na ukame na kusababisha mapato yatokanayo na ushuru wa pamba
kupungua. Ukiacha suala la ukame pia soko zuri kwa wakulima wa pamba bado ni
tatizo na changamoto kubwa kwa wakulima wa zao hilo. Pia uzingatiaji wa kilimo
bora na cha kisasa kinachohusisha utumiaji wa mbolea na madawa ya kuzuia wadudu
waharibifu wa mimea bado ni tatizo. Mbolea za ruzuku bado hazifanyiwi mzunguko
unaostahili mpaka kumfikia mkulima.
katika kuimarisha huduma za ugani shirikishi(ushauri kwa
wakulima), Mkoa wa MWANZA umetumia mbinu shirikishi katika kuibua miradi ya
ASDP na kuanzisha mashamba darasa.
Katika sekta ya uzalishaji mali, wilaya ya KWIMBA ndiyo yenye
idadi kubwa ya mashamba darasa(113) ukilinganisha na wilaya nyingine mkoa wa
MWANZA. ASDP huu ni mpango wa maendeleo ya sekta ya kilimo.
Idadi ya zana za kilimo wilaya ya KWIMBA kufikia 2015, matrekta
makubwa ni 57, matrekta madogo(power tillers) yapo 45, majembe ya kukokotwa na
ng'ombe(plau) jumla yapo 9,933.
Katika uhamasishaji wa ujenzi wa maghala bora ya kuhifadhia mazao,
wilaya ya KWIMBA ina maghala manne ya kuhifadhia chakula hasa baada ya mavuno.
Japo tatizo la njaa hasa wilaya hii bado ni changamoto kubwa ambayo inapaswa
mikakati katika kupata utatuzi na ufumbuzi wa kudumu.
Itakumbukwa gazeti la Habari Leo liliwahi kuandika habari juu ya
mbunge wa jimbo la Sumve kuomba msaada serikalini kuletewa chakula cha
msaada jimboni. Mbunge aliyasema hayo kwa kile alichoikiita kukauka kwa mazao
kutokana na ukosefu wa mvua. Hii ilikuwa mwaka jana 2015
TAASISI ZA ELIMU.
Wilaya ya KWIMBA ina shule za awali 148(zote serikali), na shule
za awali 151. ikiwa ni wilaya pekee kwa mkoa isiyokuwa na shule za binafsi
upande wa awali na msingi mpaka kufikia mwaka 2015.
W ilaya pia ina Shule za sekondari 31, ikiwa ni wilaya ya
pili yenye idadi kubwa ya shule za sekondari baada ya wilaya ya Sengerema yenye
shule 48. Japo inahitajika ongezeko la shule za kidato cha tano na sita, ambapo
mpaka sasa katika kata zote 30 za wilaya kuna shule 3 tu.
Wilaya ya KWIMBA ina vyuo vitatu vinavyotoa elimu na mafunzo kwa
ngazi ya astashahada na stashahada.
1. MALYA COLLEGE OF SPORTS DEVELOPMENT. Ni moja ya vyuo vikubwa
vya michezo kipo kata ya Malya. Inasemekana ndicho chuo pekee cha kuzalisha
wataalamu na walimu wa michezo Tanzania.
Makala inayochambua mafanikio na mwenendo wa chuo hiki unaweza
kuisoma HAPA
2. NGUDU SCHOOL OF ENVIRONMENTAL HEALTH SCIENCES. Kilichopo tarafa
ya NGUDU na kata ya NGUDU jirani kabisa na hospital ya wilaya.
3. SUMVE SCHOOL OF NURSING-KWIMBA. Hiki kinapatikana ilipo
hospital ya rufaa ya SUMVE kata ya Sumve
UWEZESHAJI.
Katika kuhamasisha uimarishaji wa mifuko ya wanawake iliyopo
katika halmashauri, ili wanawake wengi zaidi waweze kupata mikopo na kunufaika.
Wilaya ya Kwimba ina jumla ya vikundi 13 hadi kufikia 2015.
Naweza kusema kuwa idadi hii ni ndogo sana ukilinganisha na
uhitaji wa huduma hii. ambapo tunatarajia vikundi vingi zaidi vikiandikishwa na
kuwezeshwa ili kumkwamua mwanamke ambapo viongozi wenye dhamana wana wajibika
katika hili.
WILAYA MBILI AU HALMASHAURI MBILI?
Baada ya kuona takwimu na maelezo mengine baadhi yanayohusu wilaya
ya KWIMBA, turudi kwenye mada kuu inayolenga kujua kama kutatakiwa mgawanyo
kwenye wilaya ulenge haswa wapi.
Mwaka jana(2015) mwezi June Mbunge wa
Jimbo la Sumve alipata kunukuliwa akimwomba katibu mkuu wa chama tawala ndugu Abdulrahman Kinana kupitia moja ya
mikutano ya siasa jimboni kwake kwamba wilaya igawanywe ziwe wilaya
mbili(KWIMBA na SUMVE).
“Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara
mjini Sumve, mbunge huyo alisema wilaya hiyo ina watu wapatao 400,000 ambao ni
wengi kiasi cha kuhitaji kugawanywa.”. Hata hivyo, Katibu Mkuu wa Chama Cha
Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana alishauri waanzie kuomba halmashauri badala
ya mgawanyo wa wilaya.
Alisema halmashauri ndiyo inapata
fedha za maendeleo kwa maana kwamba, wakiwa na halmashauri mbili, kila moja
itapata fedha zake.
Nadhani pia angeshauriana na mbunge
mwenzie wa jimbo la Kwimba kisha wakawa na msimamo wa pamoja. Baadae wangeandaa
hoja binafsi kwenye bunge(endapo kama hoja hiyo ni mahsusi kwa bunge) juu ya
agenda hiyo wakiwa tayari wamefanya upembuzi yakinifu juu ya watakachoenda
kukiwasilisha.
Kila mmoja anaweza kuwaza kwa namna yake
ya kipekee kwamba kilingana na vigezo vya uanzishaji wa mamlaka mpya ya
serikali za mtaa, wilaya yetu inakidhi vigezo vipi kati ya kugawanywa na kuwa
wilaya mbili au kuwa na halmashauri mbili ambazo zote zitakuwa chini ya wilaya
moja?
Katika msingi wa majadiliano yetu,
tunaweza kushauri kulingana na taratibu na kanuni zinazoongoza ugawanywaji au
uundwaji wa mamlaka mpya chini ya serikali za mitaa. Pia umuhimu wa kugawanya
mamlaka ni upi na pengina kama kutakuwa na athari pia ni vyema zikabainishwa.
VIGEZO NA TARATIBU ZA KUANZISHA/KUPANDISHA
HADHI MAMLAKA ZA
SERIKALI ZA MITAA
SERIKALI ZA MITAA
Mamlaka za Serikali za Mitaa huanzishwa
kwa kuzingatia Ibara 145 na 146 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Ibara hizi zinaelekeza kuanzishwa kwa vyombo vya Serikali za Mitaa katika eneo
la Mikoa, Wilaya, Mji na Kijiji. Ili kutekeleza matakwa haya,
Sheria za Serikali za Mitaa zimeweka masharti, misingi na taratibu za kufuatwa katika kuanzisha Mamlaka za Serikali za Mitaa.
Sheria za Serikali za Mitaa zimeweka masharti, misingi na taratibu za kufuatwa katika kuanzisha Mamlaka za Serikali za Mitaa.
Utaratibu wa kuanzisha Mamlaka za Serikali
za Mitaa ni mapendekezo au maombi ya kuanzisha Mamlaka hizo kupata ridhaa ya
wananchi kupitia vikao vilivyowekwa Kisheria katika ngazi husika.
Katika makala hii inayohusisha wilaya na
halmashauri, ngazi ya halmashauri ni kupitia Baraza la madiwani. Na upande wa
wilaya suala hili linakuwa chini ya “KAMATI YA USHAURI YA WILAYA-DDC”
VIGEZO VYA KUANZISHA HALMASHAURI ZA WILAYA:
i. Kuwepo na idadi ya Kaya zinazotakiwa kwa eneo kuwa
Halmashauri ya Wilaya;
ii. Kuwepo kwa idadi ya watu wanaotakiwa kwa eneo kuweza
kutambuliwa kuwa Halmashauri ya Wilaya;
iii. Kuwa na eneo la ardhi ya kutosha kuendeleza shughuli za
kiuchumi, kijamii na kimaendeleo katika Halmashauri ya Wilaya kiwango;
iv. Kuwepo na mapato yanayotarajiwa kukusanywa kama kodi au
tozo nyingine zenye kutosheleza utoaji wa huduma muhimu pamoja na uendeshaji wa
shughuli za Serikali katika eneo zima la Halmashauri ya Wilaya;
v. Kuwepo kwa huduma za kijamii na kiuchumi, kama vile shule,
vituo vya afya, zahanati, maji, barabara kwa kuzingatia viwango vilivyowekwa
kitaifa kwa kila sekta husika.
Vigezo vya kuanzisha Halmashauri ya Mji (Town Council)
i. Kuwe na watu wasiopunga 30,000.
ii. Mji uwe na uwezo wa kujiendesha angalau kwa asilimia 50% ya
bajeti yake.
iii. Mji uwe na kiwango cha juu cha utoaji huduma ya hospitali,
kuwe na shule ya Sekondari, kuwe na angalau maduka ya rejareja yenye leseni
yasiyopungua 50, Kituo cha Polisi na pawe na Makao makuu ya Tarafa..
Kwa hayo machache unaweza ukawa ni mwanzo mzuri wa wasomaji wa
makala hii kujenga hoja juu ya kipi ni bora na halali kwa mazingira ya sasa ya
wilaya yetu.
Ni nafasi nzuri pia kwa wataalamu wa masuala ya sheria kuweza
kutuchambulia kanuni na taratibu zinasemaje juu ya uanzishwaji wa mamlaka mpya
ya serikali za mitaa, Lengo ni kuona wilaya inasonga mbele kimaendeleo kutoka
hatua hii tuliyopo.
Pia kwa wataalamu wa kada nyinginezo zote kuweza kuchangia
katika hili, ili mwisho wa siku tuwe na mawazo ya wengi yanayoweza kukubalika
na umma wa wana KWIMBA wote.
Nitoe RAI yangu kwa wasomaji wote wa makala haya kwamba,
wapitie vizuri kisha wachangie kulingana na kilichoongelewa. Ni imani yangu
kwamba wilaya hii kongwe ina wasomi wengi katika ngazi mbalimbali hivyo kwa
watakaopata wasaa wa kupitia hapa wanaweza kusaidia sana kuchangia kwa weledi
na ustadi mkubwa.
Je inatakiwa wilaya mbili au inatakiwa tuwe na halmashauri mbili
ndani ya wilaya yetu?
Tafakari.
NGUDU NYUMBANI BLOG
nguduone@gmail.com
No comments:
Post a Comment