BY
NGUDU NYUMBANI BLOG
Japo kwa ufupi tupate kujua maelezo machache juu ya taasisi hizi
zisizo za kiserikali kwa faida ya wasiojua, kisha kama kuna wahusika au wadau
wa maendeleo wanaojua kinachoendelea ndani ya taasisi hizi waujuze umma wa wana
Kwimba maendeleo yake yako vipi japo kwa muhtasari kufikia mwezi huu.
Nikimaanisha miradi ya maendeleo kupitia taasisi hizo,
mwitiko wa watu kushirikiana na taasisi na mchango wa serikali pamoja na
wafadhili kutoka ndani na nje umewezesha kwa kiasi gani kuikuza taasisi husika
na hatimaye kufikia malengo yake. Na kama kuna utaratibu maalumu wa kupata
taarifa husika hizo pia ni vema ikajulikana wenye nia ya kujua wakafuata..
1.
SHIKOME ORGANISATION GROUP
Ni taasisi isiyo ya kiserikali inayojihusisha na masuala ya
maendeleo kwenye jamii na demokrasia, ambapo imejikita hasa kusaidia makundi ya
watu kwenye jamii kama watoto, vijana, wanawake na masuala ya kijinsia kwenye
jamii.
Imeanzishwa mwaka 2007 na wamepata kuanzisha na kusimamia baadhi
ya miradi ikiwemo SHIKOME
ORGANISATION TAILORING CENTER hapo
Ngudu chini ya ufadhili wa shirika moja la nje Vraag en Aanbod International.
Katika moja ya report zao wameweza kuelezea baadhi ya mambo ya
uanzishwaji wa mradi, malengo, wanufaika, kazi zitakazofanyika kwenye mradi huo
na mengineyo. Coordinator wa mradi huo alikuwa ndugu MADELEKE SULEIMAN
Pia kuna katiba ya taasisi hii ambayo imejaribu kuelezea utaratibu
mzima juu ya uendeshaji wa taasisi, masuala ya uanachama na mengine yote
yahusuyo umoja huo. Pia kuna cheti cha usajiri kinachothibitisha kuwa taasisi
hiyo imesajiliwa kihalali kwa mujibu wa sheria.
Kwa sasa hakuna report zao zinazoonesha mwendelezo wa miradi
wanayoisimamia na hatua walizofikia kwenye miradi hiyo. Kwa msaada ya anayejua
ama mhusika ama mdau wa maendeleo anayejua juu ya taasisi hii ni vyema na
busara akaujuza umma hatua waliyopo kwa sasa…….
2. KWIMBA WOMEN DEVELOPMENT (KWIWODE)
Taasisi hii imeanzishwa mnamo mwaka 2004 na kikundi cha wanawake
wajasiliamali wa Kwimba kusaidia kutetea haki za mwanamke na kuleta usawa wa
kijinsia kwa maana ya fursa sawa kwa jinsia zote.
Kazi kubwa ya kikundi hiki ni kulinda haki za mwanamke, kumpa
mafunzo mbalimbali ya ujasiliamali ya kumwezesha kujikwamua na hali ngumu ya
maisha na mambo mengine yanayoihusu jamii.
Moja ya miradi yao ni ule wa mwaka 2010 uliojulikana kama REHABILITATION AND SANITATION
FACILITIES FOR NYAMILAMA PRIMARY SCHOOL
PROJECT chini ya
support nzuri kutoka kwa Tanzania
development trust na
coordinator wa mradi alikuwa ni Edina
Ihonde
3. NEEDFUL ACTION FOR DEVELOPMENT SEARCH ORGANISATION(NADSO)
Ni taasisi inayohusisha umoja wa wanafunzi waliosoma Ngudu
sekondari au na kuishi wilaya ya Kwimba kwa ujumla. Lengo kubwa la taasisi hii
ni kusaidia jamii za watanzania kwenye Nyanja za maendeleo hususani wilaya yetu
ya Kwimba hasa katika elimu, ujasiliamali,na shughuli za maendeleo kwa ujumla.
Ambapo itafanya kazi na wadau wote wa maendeleo nchi nzima lakini kwa kuelekeza
zaidi wilaya ya Kwimba.
Katika moja ya mafanikio ya taasisi ni pamoja na kutembea
shule ya sekondari Ngudu Msafara uliofanikisha Ununuzi wa vitabu na pia kuwapo
kwa documentary juu ya kilichojiri kwenye safari hiyo kwa ujumla safari hii
ilifanyika mwezi wa 5 mwaka huu.
Kwa anayetaka kujiunga na taasisi hii kuna utaratibu ulitolewa
hapo kabla ambapo kuna katiba ya taasisi ambayo imeongelea mambo yote kwa
undani kabla ya kutaka kuwa mwanachama.
MWISHO.
Lengo la kuelezea yote haya ni kutambua uwepo wa taasisi, kuonesha
kujali na kuzitakia taasisi hizi mafanikio ambapo ni maendeleo ya wilaya yetu
pia.
Pengine zikawepo nyingine tofauti na hizi nilizozitaja
ambapo lengo lao pia ni kusaidia maendeleo ya wilaya yetu pia. Ushauri kwa
vijana na wadau wote wa Kwimba kujiunga katika vikundi mbalimbali vya
kimaendeleo mkianza kujisimamia wenyewe kwa mtaji mdogo mlionao, ambapo
mkionesha nia ya dhati juu ya mnachokifanya bila shaka support itapatikana tu.
KWIMBA TUITAKAYO.
nguduone@gmail.com .
No comments:
Post a Comment