TAASISI ya kifedha ya Bayport Financial Services inayojihusisha na mambo ya mikopo imepongezwa na serikali kwa hatua yake ya kufungua tawi wilayani Kwimba mkoani Mwanza
Shughuli za uzinduzi huo zilifanyika Machi 2 mwaka
huu, huku mgeni rasmi akiwa ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Kwimba, Vicent
Emmanuel, akiongozana na viongozi mbalimbali wa serikali wilayani humo.
Akizungumza
katika uzinduzi huo, Katibu Tawala huyo wa wilaya Kwimba, Emmanuel alisema
kwamba kufunguliwa kwa tawi hilo kutatoa huduma karibu na wananchi, kama njia
ya kukuza uchumi wao kwa ujumla, zikiwapo fursa za kukopeshwa bidhaa
mbalimbali, vikiwamo vyombo vya usafiri.
Alisema kwamba awali watu wa Kwimba walilazimika kusafiri umbali mrefu
kupata huduma za mikopo, lakini sasa wamesogezewa huduma karibu, hivyo ni
jukumu lao kutumia fursa hiyo kwa ajili ya kujinufaisha kwa ajili ya maisha
yao.
“Serikali tunaipongeza Bayport
Financial Services kwa hatua ya kuanzisha tawi hapa Kwimba, hivyo tunaamini kwa
pamoja tutafanikisha maendeleo kwa watu wote kwa kupitia njia ya mikopo kwa
watumishi wa umma na wafanyakazi waliodhinishwa,” alisema Emmanuel.
Naye Meneja Mauzo wa Bayport
Financial Services Kanda ya Ziwa, Lugano Kasambala, alisema kwamba tawi lao
limejipanga kutoa huduma bora kwa wakazi na wananchi wa Kwimba waliokuwa
wakisafiri umbali mrefu kupata huduma zao.
“Huu ni mwendelezo wa Bayport
Financial Services kuhakikisha kwamba tunaendelea kufungua matawi katika sehemu
mbalimbali, ambapo sasa tumefikisha matawi 79 nchini kote, ambapo uwapo wa
taasisi yetu umerahisisha maisha kwa watumishi wa umma na wafanyakazi
waliodhinishwa na taasisi yetu.
“Tunaomba wachangie fursa za mikopo
mbalimbali kama ile ya bidhaa, mikopo ya fedha, bima ya elimu kwa uwapendao,
ambapo katika mikopo ya bidhaa, mteja anaweza kukopeshwa bodaboda, vifaa vya
ujenzi, injini za boti, pembejeo za kilimo na huduma nyingine nzuri na muhimu
kwa Watanzania wote,” alisema.
Kwa
mujibu wa Kasambala, huduma za Bayport ni rahisi kupatikana ndani ya saa 24,
huku zikiwa hazina amana wala dhamana, jambo linaloonyesha mafanikio makubwa
kwa wateja wetu watakaoamua kupata huduma katika taasisi yao.
Bayport Financial Services ni
taasisi inayojihusisha na mikopo, huku ikiwa na matawi katika mikoa mbalimbali
ya Tanzania, ambapo kwa kupitia tawi la Kwimba, wateja wao hawatalazimika
kusafiri ili wapate huduma za taasisi hiyo.
Chanzo:
handeni ketu blog
No comments:
Post a Comment