Wednesday, February 10, 2016

MCHANGO WA CHUO CHA MALYA KWA MAENDELEO YA MICHEZO


(Makala hii ipo katika toleo la gazeti la habarileo la may 9 2015)
MICHEZO ni afya walisema wahenga tangu enzi za mababu zetu. Nami sina budi kukubaliana na msemo wa wahenga hawa kwani nimeshuhudia michezo ikijenga afya na kudumisha undugu ama kujenga urafiki.
Mafanikio na maendeleo ya michezo Tanzania ni matokeo ya muda mrefu ya juhudi za serikali kwa kushirikiana na wadau wengine kuhakikisha taifa linapata wanamichezo wenye vipaji na kuwaendeleza ili wafikie ndoto za kutwaa ubingwa kwenye mashindano mbalimbali ndani na nje ya nchi.
Katika kuzungumzia mafanikio haya ya michezo na maendeleo ya taaluma hii, makala haya yatajikita zaidi katika kuzungumzia chuo pekee cha kuzalisha wataalamu na walimu wa michezo Tanzania, Chuo cha Michezo cha Malya.

Monday, February 8, 2016

SHINDANO LA MISS ALBINO MWANZA


 
Zawadi Dotto Mshindi wa shindano la miss albino mkoa wa Mwanza
HATIMAYE shindano la kumsaka mrembo albino jijini Mwanza limefikia tamati baada ya Zawadi Dotto (17) kuibuka kidedea na kutawazwa kuwa mshindi katika shindano hilo baada ya kuwagaragaza wapinzani wake sita.

Shindano hilo lilifanyika juzi usiku jijini hapa huku likiwakutanisha wasichana saba wenye ualbino ili kumpata mshindi atakayewakilisha mkoa kitaifa.
Warembo hao ni Hajra Sadru, Furaha Elias, Zabibu Abdalah, Anthonia Mathias, Pendo Faustine na Asteria Christopher walionyesha madaha na ubunifu jukwaani wakisaka nafasi hiyo.

Hata hivyo, walioingia tatu bora katika mpambano huo ni Zawadi Dotto, Furaha Elias na Hajra Sadru ambapo Dotto aliweza kung’ara zaidi na kuwaacha wawili hao.
“Kwakweli sikutarajia kama ningeweza kushinda taji hili, kwa sababu wote umewaona walivyo safi, mimi nakiri kuwa ni kudra za Mungu labda nitapambana kupigania haki za watu wa albino,” alisema Dotto.
Mlimbwende huyo alijinyakulia zawadi ya simu aina ya Solar5, kitita cha Sh 100,000 na godoro, huku mshindi wa pili, Hajra Furaha, akijinyakulia simu, godoro na Sh 80,000 na mshindi wa tatu akijinyakulia simu, godoro na Sh 50,000.


Chanzo: Gazeti la Mtanzania

Saturday, January 30, 2016

MBUNGE MANSOOR SHANIF HIRAN, JIMBO LA KWIMBA NA KWIMBA TUITAKAYO.

Mh Mansoor Shanif Hirani, Mbunge jimbo la KWIMBA(2015-2020)

By NGUDU NYUMBANI BLOG
30/01/2016.

NDUGU Mansoor Shanif Hirani alizaliwa Tar 05/05/1967, kwa maana hiyo ikifika Tarehe 05 may mwaka huu atafikisha miaka 49. Amesoma katika shule ya msingi “Nyakahoja” kuanzia 1975-1981, pia kasoma shule ya sekondari ya “Lake” kuanzia mwaka 1982-1986.

Kwa sasa ndiye Mbunge halali wa Jimbo la KWIMBA kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), pia ndiye mweka hazina wa mkoa wa Mwanza (Ccm) wadhifa aliokuwa nao tangu 2012. Pia ndiye katibu mkuu mtendaji wa kampuni la "Mansoor industries ltd". Bila kusahau kuwa ni mjumbe wa kamati za kudumu za bunge (bunge la 11) kwenye kamati ya “MIUNDOMBINU”. Anafahamika Kwa nick-name “MOIL”.

HISTORIA

“Mkoa wa mwanza ulianzishwa rasmi mwaka 1963 ukiwa na wilaya nne za Ukerewe. Geita, Mwanza na Kwimba. Mwaka 1972  baada ya sera ya madaraka mikoani wilaya zaidi  zilianzishwa kwa kuanza na Magu mwaka 1974. Wilaya ya  Sengerema ilianzishwa mwaka 1975 ambapo awali ilikuwa  ni tarafa mojawapo ya wilaya ya Geita.  Misungwi  ilianzishwa mwaka 1995 ambapo awali ilikuwa ni eneo la tarafa za wilaya ya Kwimba, Ilemela na Nyamagana  zilianzishwa mwaka 2002 ambazo zilikuwa zinaunda  wilaya ya mwanza”. [TAARIFA YA MKOA WA MWANZA WAKATI WA MAADHIMISHO YA MIAKA 50 YA UHURU WA TANZANIA BARA 1961-2011]


Sunday, January 24, 2016

MATOKEO YA UPIMAJI WA KITAIFA DARASA LA NNE(SFNA) 2015


BY NGUDU NYUMBANI BLOG

Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA), limetangaza matokeo ya mitihani ya kujipima ya darasa la nne huku matokeo hayo yakionyesha wanafunzi wengi wamefeli katika somo la Kiingereza kwa asilimia 65.67 katika mitihani hiyo iliyofanyika mwishoni 2015.

Akitangaza matokeo hayo  Jijini Dar es Salaam, Katibu Mtendaji wa Baraza hilo Dkt. Charles Msonde amesema juhudi za makusudi zinahitajika katika kuboresha mazingira ya ufundishaji na ujifunzia ili kuboresha kiwango cha ufaulu.

Jumla ya wanafunzi 869,057 kati ya wanafunzi 977,886 sawa na asilimia 88.87 waliofanya upimaji wamepata alama katika madaraja ya A,B,C, na D. Wanafunzi 108,829 sawa na asilimia11.13 wamepata alama za ufaulu usioridhisha.

Aidha wanafunzi wamefanya vizuri zaidi katika somo la Sayansi kwa asilimia 89.44, na baraza limewataka walimu kuweka mkazo zaidi kwa wanafunzi waliofanya vibaya ili wawasaidie kuimarika na waweze kupata ufaulu mzuri.

MATOKEO UPANDE WA WILAYA YA KWIMBA

Kwa upande wa matokeo hayo ya upimaji wa kitaifa darasa la nne, ambapo kuna jumla ya shule za msingi 151.

Baadhi ya Shule za msingi zilizoongoza katika upimaji wa matokeo hayo ni kama ifuatavyo;

1. KINAMWELI PRIMARY SCHOOL

2. NG'WAMAKOYE PRIMARY SCHOOL

3. MWAKILYAMBITI PRIMARY SCHOOL

4. MWANG'HALANGA PRIMARY SCHOOL



Baadhi ya Shule zilizofanya vibaya katika upimaji huo ni;

149. NG'WANG'HANGA PRIMARY SCHOOL


151. NG'WAMAPALALA PRIMARY SCHOOL

Matokeo yote upande wa wilaya yetu ya Kwimba unaweza kuyapata kupitia link hii


>>>> MATOKEO

au ukiingia kwenye tovuti ya NECTA

Thursday, January 21, 2016

MCHANGANUO WA WABUNGE KATIKA KAMATI ZA BUNGE LA KUMI NA MOJA

MCHANGANUO WA WABUNGE KATIKA KAMATI ZA BUNGE LA KUMI NA MOJA




Wabunge wa majimbo ya KWIMBA na SUMVE wilaya ya KWIMBA wamepata nafasi katika kamati hizo za kudumu za bunge ambapo;

Mbunge wa Kwimba, MH Mansoor Shanif Hirani yupo kwenye kamati namba 14 ya MIUNDO MBINU

Mbunge wa SUMVE Ndugu Richard Mganga Ndasa yupo kwenye kamati  namba 20 ya “UWEKEZAJI WA MITAJI YA UMMA”

Orodha kamili ya kamati zote 20 na wajumbe wake unaweza kuipata kupitia link hii




RIPOTI YA MWAKA 2015 JUU YA MAMBO YALIYOJIRI KWA HISANI YA NGUDU NYUMBANI BLOG


RIPOTI YA MWAKA JUU YA MAMBO YALIYOJIRI KWA HISANI YA NGUDU NYUMBANI BLOG

Hii ni ripoti iliyojumuisha mambo mbalimbali ambayo blogu ya Ngudu nyumbani (www.ngudukwimba.blogspot.com) ilipata kuyakusanya kwa mwaka huu kutoka vyanzo mbalimbali vya habari na watu binafsi. Hivyo imepata kuyapanga mambo kwenye makundi kama yalivyoainishwa hapo chini. Twende pamoja…

ULINZI NA USALAMA
Katika hili mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wa wilaya ambaye ni mkuu wa wilaya ambapo chombo cha ulinzi na usalama ndio washauri wake hivyo yeye ndiye mwenye jukumu kubwa la kuhakikisha anafuatilia kwa ukaribu zaidi usalama wa raia wake. Ndani ya mwaka huu kumepata kutokea matukio baadhi ambayo kwa namna moja au nyingine hayakuleta picha nzuri kwenye jamii yetu.

LETICIA MAGENI NYERERE AFARIKI DUNIA


ALIYEWAHI kuwa Mbunge wa Viti Maalumu kwa tiketi ya Chadema, Leticia Nyerere amefariki dunia.
Leticia alifariki dunia katika Hospitali ya Doctors Community iliyopo Lanham, Maryland jana (Tar 11 jan 2016) saa 2 usiku kwa saa za Afrika Mashariki, alikokuwa amelazwa kwa matibabu.
Taarifa za awali kutoka Marekani, ambako msiba huo umetokea, ziliarifu kuwa msiba upo DMV 9004 Brightlea Court, Lanham, MD 20706.
Msemaji wa familia hiyo, Mbunge wa zamani wa Chadema, John Shibuda alithibitisha kutokea kwa msiba huo. Alisema ndugu wanajipanga kukutana na kuamua cha kufanya.
“Ndugu yangu ni kweli msiba umetokea wa mpendwa wetu Leticia Nyerere, umetokea jana mchana huko Marekani na huku kwetu ilikuwa ni usiku, hivyo ndugu bado hatujakutana na kuamua kwa pamoja ni wapi tuweke msiba na lini tutazika,” alisema Shibuda.
Shibuda alisema kuwa leo familia itatoa taarifa kamili ya taratibu zote za msiba huo baada ya wanafamilia kukutana.
Previous Page Next Page Home