Sunday, December 6, 2015
Sunday, November 29, 2015
TAARIFA KWA UMMA JUU YA KILIMO MKOA WA MWANZA.
OFISI
YA WAZIRI MKUU TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
OFISI
YA MKUU WA MKOA WA MWANZA TAARIFA KWA UMMA TAREHE 18/11/2015
Ndugu
Wanahabari.
Mkoa wa Mwanza kwa kawaida hupata misimu miwili ya
mvua kwa mwaka. Misimu hiyo ni ya mvua za vuli na masika ambapo mvua za vuli
huanza kunyesha mwezi Septema/Oktoba hadi kufikia mwezi Januari; na msimu wa
mvua za masika hunyesha Kuanzia mwezi Machi hadi Mei ya kila mwaka. Wastani wa
mvua ni mm 720 hadi mm 1200 kwa mwaka ambazo hutawanyika kati ya mm 570 mm kwa
mwaka hadi mm 1800 kwa mwaka.
Ndugu
Wanahabari.
Mkoa wa
Mwanza unatarajiwa kupata mvua za wastani hadi juu ya wastani kwa maana ya mvua
za juu ya wastani wa mm 1300 katika kipindi hicho cha Oktoba – Desemba, 2015.
Hii ni kwa mujibu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA).
Kwa kuzingatia utabiri huo wa hali ya hewa,
tunawashauri wakulima na wananchi katika Mkoa wa Mwanza kufanya yafuatayo:-
Kulima mazao ya chakula aina ya wanga yanayohitaji
au kustahimili mvua za wastani hadi mvua za juu ya wastani na pia kukomaa kwa
muda mfupi kiasi cha kuweza kukomaa kufikia mwezi Desemba, 2015/Januari, 2016.
Mkazo zaidi utiliwe kwenye mazao ya:-
Viazi vitamu hasa mbegu (Variety) zisizolikishwa
(Non-Orange Fortified) aina ya Polista na Ukerewe, “Kishiga Mdege” na
matembele; pamoja na mbegu zilizolikishwa (Orange Fortified) kama Ejumla,
Karotoda na Kabode.
Mazao mengine ni mahindi hasa katika ukanda wa mazao
(agro-ecological zone) unaopata mvua za wastani wa mm 1100 hadi 1200 kwa mwaka
au Zaidi ukanda ambao unajumuisha Tarafa za Ukara na Ilangala katika Wilaya ya
Ukerewe na Tarafa za Kahunda na Buchosa katika Halmashauri ya Wilaya ya
Buchosa. Aina ya mbegu (variety) za mahindi zinazopendekezwa ni:-
(i) Aina ya mbegu ya mahindi chotara (hybrid) ni
pamoja na SeedCo yenye alama ya pundamilia (SC 513), Pannar inayokomaa kwa muda
mfupi (PAN 4M-19) na kati PAN 15), Delkab (DKC 8053).
(ii) Aina ya
mbegu ya mahindi isiyochotara/ya chavua huria (OPV) ni pamoja na Kilima, Stuka,
TAN 600H, Kitale na TMV 1. Mpunga hususan mbegu aina ya SARO 5 (TXD 306) na
Supa inayolimwa mabondeni (low land rice); na NERICA 2 na 4 zinazolimwa nchi
kavu.
Ndugu
Wanahabari.
Tunawashauri wananchi wetu kutenga fedha na kununua
pembejeo za kilimo hasa mbegu, mbolea na dawa za kilimo mapema kwa kuzingatia
kuwa matumizi ya pembejeo yanaweza kuongezeka kutokana na mvua hizo ambazo
zinaweza kusababisha kuoshwa ama dawa za kudhibiti wadudu waharibifu na
magonjwa au mfumuko wa magonjwa hasa ya ukungu kutokana na mazingira ya
unyevunyevu mwingi katika ardhi na hewani. Aidha, pembejeo zinaweza kupanda bei
na kuwa adimu kutokana na kutopatikana kwa wingi na kwa urahisi kwa sababu ya
mvua kuharibu miundombinu ya barabara hasa katika maeneo ya vijijini na
kuathiri usafirishaji mazao. Ili kupunguza gharama za uzalishaji kutokana na
mvua, wakulima wanaweza kugawanya kiasi cha mbolea kinanchohitajika kwa eneo na
kuweka kwa awamu lakini pia tunawashauriwa kuwatumia Maafisa Ugani katika
Wilaya.
Vilevile tunawashauri wakulima kulima kwa kukinga au
kuzuia mmomonyoko wa udongo kutokana na mvua hasa katika maeneo yenye miinuko
na vilima. Mmomonyoko wa udongo unaweza kukingwa au kuzuiliwa kwa kutumia mbinu
mbalimbali ikiwa ni pamoja na kulima kilimo cha matuta kwa kukinga/kukata
mteremko, kulima na kuacha mistari (strip) ya nyasi au kufanya kilimo hifadhi.
Zaidi, wakulima katika maeneo yanayo hifadhi unyevu kwa wingi au kutwaamisha
maji (mabonde) wanaweza kulima kwa kufuata uelekeo wa maji kwa kuacha mistari
ya nyasi kuzuia mmomonyoko wa udongo au kulima kilimo hifadhi kinachopunguza
ukwatuaji wa udongo.
Ndugu
wanahabari.
Tunawashauri wananchi kujiwekea akiba ya chakula
hasa cha aina ya wanga kutokana na sababu kwamba mvua zinazotarajiwa katika
kipindi hicho cha Oktoba na Desemba, 2015 zinaweza kuharibu miundombinu ya
barabara na kusababisha ugumu wa usafirishaji wa vyakula hivyo kuleta uhaba wa
vyakula katika masoko. Msisitizo wa kujiwekea akiba ya chakula unatolewa Zaidi
kwa kuzingatia ukweli kwamba, Mkoa wa Mwanza wenye wakazi 2,772,509 huhitaji
jumla ya Tani 708,376 za chakula aina ya wanga kwa mwaka mzima, ambapo, katika
msimu wa kilimo wa 2014/2015 Mkoa ulizalisha Tani 495,863.2 za chakula aina ya
wanga hivyo kuuwezesha kujitosheleza kwa 70% tu kwa chakula aina ya wanga.
Aidha, tunahimiza wafanyabishara kuleta chakula
kutoka kwenye maeneo yenye ziada ya chakula aina ya wanga , lakini pia wananchi
kutumia chakula kwa umakini na kuuza sehemu ya mazao ya biashara na mifugo ili
kuweza kununua chakula. Aidha, Mkoa unasisitiza kuwa wafanyabiashara
walioidhinishwa kununua na kuuza chakula kutoka katika maghala ya Wakala wa
Taifa wa Hifadhi ya Chakula Sumbawanga kufanya hivyo kwani mkoa umeutengewa
jumla ya Tani 5,400 za mahindi kwa lengo la kuongeza upatikanaji wa nafaka
katika masoko ya Mkoa wa Mwanza hii nikutokana na tathmini iliyofanywa na
wadau.
Ndugu
wanahabari
Kupitia kwenu
tunawaomba wananchi kujiwekea akiba ya chakula aina ya wanga katika ngazi ya
kaya, kwa kuzingatia kuwa wastani wa watu katika kaya ya watu 6 katika mkoa
wetu, tunawashauri kuhifadhi magunia 3 ya mahindi yenye uzito wa kilo 100
lakini pia magunia 5 ya muhogo mkavu yenye uzito wa kilo 60 kila moja sawa na
kilo 314.64 katika kipindi cha Novemba 2015 na Januari 2016 endapo kaya hiyo
itatumia mahindi au muhogo kama chakula cha wanga katika kipindi hicho.
Kwa upande wa
wakulima wanaotumia miundombinu ya umwagiliaji katika
Skimu ya Umwagiliaji Mahiga kwenye Wilaya ya Kwimba tunawashauri kuchukua
tahadhari kwani mabwawa yanaweza kukatika kutokana na mvua zinazotarajiwa na
inaweza kusababisha mmomonyoko wa udongo, kusombwa mazao shambani, kukosa maji
ya kumwagilia, kuongezeka kwa gharama za ukarabati wa mabwawa na hata kupoteza
maisha ya watu na mali zao.
Mwisho
wakulima na wananchi kwa ujumla tunawashauri kuchukua tahadhari dhidi ya
madhara yanayoweza kusababishwa na mvua zinazotarajiwa na kuzitumia vizuri mvua
hizo katika kuzalisha mazao yanayopendekezwa ili Mkoa uzalishe chakula cha
kuutosheleza katika msimu wa 2016/2017. Mara baada yakusema hayo niwashukuru
sana kwakuja lakini zaidi sana kuweza kuchukua taarifa hii na kutufikishia kwa
umma wa watanzania kupitia vyombo vyenu vya habari.
Mungu Awabariki Sana , Ahsanteni kwa
Kunisikiliza!
Chanzo:HAPA
Thursday, November 26, 2015
Hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, akifungua rasmi Bunge jipya la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dodoma, 20 Novemba 2015
Friday 20th November 2015
Chanzo :ikulu
Mheshimiwa
Spika;
Niko hapa leo kutimiza matakwa ya
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ibara ya 91 Ibara ndogo ya kwanza
inayonitaka kulihutubia na kulifungua rasmi Bunge hili. Naomba nimshukuru
Mwenyezi Mungu kwa kutujalia uzima na afya njema, na kutuwezesha kuwepo hapa
siku ya leo. Aidha nitumie fursa hii kuwakumbuka wenzetu ambao, kwa namna na
nafasi mbalimbali, walishiriki katika mchakato wa uchaguzi huu na kwa bahati
mbaya walipoteza maisha yao kabla ya mchakato haujakamilika. Kwa hao wote
waliotangulia mbele za haki ninamuomba Mwenyezi Mungu azirehemu roho zao na
awape pumziko la amani. Nitumie nafasi hii kuwapa pole ndugu na jamaa ambao
ndugu zao walifariki na wengine kupata ulemavu wakati wa mchakato wa uchaguzi
huu.
Wednesday, November 25, 2015
HAWA NDIO WABUNGE 256 WALIOTHIBITISHWA NA TUME YA NEC
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Joseph Magufuli tayari
ameapishwa na kuanza kazi… kwa upande wa Wabunge wenyewe bado.
Kinachosubiriwa
ni kuitishwa kwa Bunge la 11 ambapo Spika Mteule pamoja na Wabunge wote
wataapishwa… kingine kitakachofanyika ni uthibitisho wa jina la Waziri
Mkuu, uchaguzi wa Naibu Spika na ufunguzi rasmi wa Bunge
la 11.
Kulikuwa
na stori nyingi sana wakati wa mchakato mzima wa Uchaguzi Mkuu ikiwemo
matokeo kukataliwa na baadhi ya Wagombea, kwingine Uchaguzi haukufanyika
kabisa, kwingine uchaguzi ulisogezwa mbele kwa sababu mbalimbali. Lakini mpaka
leo November 12 2015 hapa ninayo majina ya Wabunge 256 ambayoTume ya
Uchaguzi NEC imeyathibitisha kwamba wamepita kwenye Uchaguzi.
ILIKUWA NI LAZIMA MH MANSOOR ASHINDE UBUNGE JIMBO LA KWIMBA 2015
KOMANYA, BONIPHACE, mwandishi wa makala na mmiliki wa blogu |
BY NGUDU NYUMBANI BLOG
Ni ukweli usiopingika kuwa, jimbo la Kwimba tangu mfumo wa vyama vingi kuasisiwa mwaka 1992, na
uchaguzi wa kwanza ukihusisha mfumo huo limeongozwa na chama tawala(CCM)
kuanzia ngazi za serikali za mitaa, wawakilishi kama madiwani, mbunge, pia
halmashauli kuwa chini ya usimamizi wa Ccm. Hali hiyo imeendelea kuonekana
katika chaguzi zote zilizofuata nikimaanisha 2000,2005,2010 na 2015.
Japo kwenye uchaguzi wa
wawakilishi serikali za mtaa mwishoni mwa mwaka jana wapinzani walipata
uwakilishi kwenye baadhi ya vijiji na vitongoji japo haikubadili upepo kisiasa
katika jimbo hili.
Kuna baadhi ya mambo au
sababu zinazonipelekea kusema ndugu Mansoor alikuwa na nafasi kubwa kushinda
ubunge jimbo la kwimba. Machache kati ya mengi ni kama ifuatavyo..
Moja, kukubalika sana
maeneo mengi hasa vijijini. Hii
ni kete kubwa kwa mgombea yeyote kuweka mazingira ya kushinda uchaguzi hasa
ukizingatia vijijini ndio kuna mwitikio mkubwa wa wapiga kura. Imani hiyo
kaijenga tangu agombee awamu iliyopita. Pia wananchi wengi walipata kumwamini
katika miaka mitano iliyopita, kwa maana hiyo imani yao kubwa ilimjenga na
kumpa imani kubwa ya kushinda awamu nyingine. Hapa namaanisha muitikio wao hasa
kwenye kampeni zake.
Pili, nguvu ya pesa
aliyonayo. Pia katika hili
mgombea huyu alikuwa vizuri ukilinganisha na wapinzani wake. Katumia njia hii
kucheza na akili za wananchi kwa kugawa kiasi cha fedha, nguo na vifaa vya
chama. Pia katika hatua nyingine kupitia wapambe wake amegawa majembe baadhi ya
vijiji kuhamasisha maendeleo. Njia hii imeongeza imani kwa wana ccm na wananchi
wasio na vyama hata baadhi ya wapinzani wasio na msimamo kuwa na matumaini nae.
Japo uhalisia ni kwamba inakosekana elimu ya uraia kwa wananchi kujua zawadi
hizi kipindi cha kampeni hazina manufaa ya kudumu katika maisha yao ya kila
siku ukizingatia hutolewa mara moja kila baada ya miaka mitano.
Tatu, kukosekana kwa
upinzani imara wenye kuweza
kujenga hoja na kuja na sera za kuweza kuwashawishi wananchi wawachague. Katika
hili pia UKAWA kushindwa kufikia makubaliano ya kusimamisha mgombea mmoja na
badala yake kusimamisha wawili ndugu Mh shilogela(CDM) na Mh Ntiga Otto(CUF)
kulisaidia kwa kiasi kikubwa kugawana kura za upinzani na kumpa nafasi Mh
mansoor kuwaacha kwa mbali kwenye mchuano.
Nne, kuwaaminisha
wananchi baadhi ya mambo kama kayafanikisha. Kati hili ndugu Mansoor aliweza kuanisha mafanikio katika
awamu iliyopita kama kuwaletea wananchi maji kutoka ziwa Victoria, umeme,
kuwezesha ujengwaji wa zahanati/vituo vya afya kadhaa. Kuweka mambo sawa
ni kuwa kazi ya mbunge kwa mujibu wa katiba ni kuwakilisha wananchi, kutunga sheria na kusimamia
serikali katika masuala ya
maendeleo kama kusimamia miradi. Ila sio kweli kwamba kawaletea wananchi maji
wala umeme, bali ni kupitia kuishauri na kuikumbusha serikali kufanya hayo na
mengine jimboni kwake ila hana uwezo wa kutoa hela yake kufanikisha hayo.
Katika hili la maji limekuwa likipigiwa kelele tangu kale na limekuwa
likihubiliwa kwenye ilani ya ccm kila uchaguzi na limekuja kufanikishwa kwa
kucheleweshwa kwenye uongozi wa JK japo lilikuwepo tangu enzi za Mkapa. Hapa
naweza kuwapongeza Mh mansoor na Mh Leticia Nyerere ambao walipata kuliulizia
utekelezaji wake kila walipopata nafasi kwenye bunge kuuliza swali au kujenga
hoja kila mmoja katika nafasi yake. Katika hayo alifanikiwa kujipatia kura za
kutosha.
Tano, jimbo bado ni
ngome kuu(stronghood) ya chama tawala. Hili pia linachangia kwa asilimia kubwa kama sehemu ni ngome
ya chama fulani miaka nenda rudi ni rahisi kwa chama husika kushinda japo kuna
baadhi ya maeneo hali ilibadilika na ambaye hakutarajiwa kushinda.
Jimbo la Kwimba lipo
chini ya Ccm kabla ya mfumo wa vyama vingi, baada ya kuanzishwa mfumo wa vyama
vingi hadi leo huku wakijikusanyia madiwani wengi na kuweza kuisimamia
halmashauri. Kwahiyo upinzani walipaswa kutumia nguvu zaidi na njia mbadala za
kuwawezesha kushinda.
MAONI YANGU
Nilipata kufatilia
uchaguzi kwa kuwasikiliza wagombea kama Mh Mansoor, Mh shilogela na Ndugu Ntiga
kusikiliza sera zao na hoja zao juu ya uwakilishi wa jimbo letu.
Kiukweli nilimwelewa sana ndugu Ntiga Otto
jinsi alivyokuwa akiwasilisha Mipango na mikakati yake juu ya kuiongoza Kwimba,
japo ni hali isiyofichika kwamba ndiye alikuwa na wasikilizaji/wananchi
wachache zaidi ukilinganisha na hao wenzake wawili waliokuwa na watu wengi.
Hawa Iswalala(UDP) na mch. Yohana(ACT)
sikupata kuwasikia ama kuhudhulia kampeni zao. Bila shaka kilichomwangusha huyu
kijana aliyejimbanua(Otto) ni kutokukubaliana kwenye umoja wao. Pia ‘mind set’
za wananchi wengi ambao hawako tayari kusikiliza sera na kubakia kushabikia
vyama zaidi.
Salamu zangu hizi
zimfikie popote alipo na asikate tama ajipange kwa awamu ijayo.
Uchaguzi umeisha, mbunge
na madiwani wamepatikana, cha msingi ni kuwapa support tuweze kufikia lengo la
kupiga hatua ya maendeleo jimbo na wilaya yetu kwa ujumla.
Malalamiko ya kwamba huyu mhindi, sijui sio
mzawa hayatosaidia kitu zaidi ya kushirikiana na kiongozi aliyeshinda kusukuma
gurudumu la maendeleo. Pia ideology ya kuwa mbunge ndio mtu sahihi wa kuleta
maendeleo jimboni, ni ya kupuuzwa tu. kila mmoja wetu anayo nafasi ya kuleta
maendeleo kwenye jamii yake na sio kusubiri fulani akuletee maendeleo mlangoni.
tunawa support viongozi
wa ngazi zote tukiweka itikadi za vyama vyetu pembeni. Sote ni wamoja ubaguzi
ni kuonesha udhaifu.
kutokana na machache niliyoyagusia hapo juu, nashawishika kusema kwamba Ilikuwa ni lazima kwa mh. Mansoor kushinda ubunge kwenye jimbo la Kwimba mwaka 2015.
kutokana na machache niliyoyagusia hapo juu, nashawishika kusema kwamba Ilikuwa ni lazima kwa mh. Mansoor kushinda ubunge kwenye jimbo la Kwimba mwaka 2015.
KWIMBA TUITAKAYO
nguduone@gmail.com
Friday, November 13, 2015
TUME YATOA MAELEZO NA IDADI YA MADIWANI VITI MAALUM
JAMHURI
YA MUUNGANO WA TANZANIA
TUME
YA TAIFA YA UCHAGUZI
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
UTEUZI WA MADIWANI WANAWAKE WA VITI MAALUM
Kwa mujibu wa Kifungu cha 86 A (8) cha Sheria ya
Uchaguzi Serikali za Mitaa Sura ya 292, (Uchaguzi wa Madiwani) kikisomwa kwa
pamoja na Vifungu vya 35 (1) (c) na 19 (1) (c) vya Sheria za Serikali za Mitaa
(Tawala za Wilaya) na Na. 7 ya mwaka 1982 na Serikali za Mitaa (Tawala za Miji)
Na. 8 ya mwaka 1982, Tume ya Taifa ya Uchaguzi imepewa mamlaka ya kushughulikia
na kutangaza Viti Maalum vya Madiwani Wanawake visivyopungua 1/3 ya Madiwani wa
kuchaguliwa katika kila Halmashauri. Kwa kuwa Kata 3,957 zilifanya Uchaguzi
Mkuu 2015 hivyo 1/3 yaViti Maalum vya Madiwani Wanawake ni 1,406. Hata hivyo,
Tume haikuweza kugawa Viti vyote katika Halmashauri kutokana na kuahirishwa kwa
Uchaguzi wa baadhi ya Kata katika baadhi ya Halmashauri nchini. Mgawanyo wa
viti vilivyobaki utafanyika mara baada ya chaguzi zilizoahirishwa kufanyika.
Vyama vya Siasa vilivyoshiriki Uchaguzi Mkuu kwa
upande wa Madiwani na kukidhi vigezo vya kisheria vya kupata Viti Maalum ni
kama ifuatavyo:-
Jumla ya Viti vilivyogawanywa ni 1,392.
Viti 14
vilivyosalia vitagawanywa mara baada ya Kata zilizoahirishiwa Uchaguzi
kukamilisha zoezi la kupiga Kura
Majina ya Madiwani Wanawake wa Viti Maalum kwa kila
Halmashauri walioteuliwa yataweza kupatikana kutoka Vyama na kwenye Halmashauri
husika. Aidha tarehe 14/11/2015, Tume ya Taifa ya Uchaguzi itatangaza majina ya
Madiwani wa Viti Maalum walioteuliwa. Ikumbukwe kuwa Tume imefanya uteuzi kwa
kuzingatia Orodha iliyowasilishwa Tume na kila Chama kwa kuzingatia vipaumbele
vya Chama husika.
Imetolewa na:
Jaji
(Mst.) Damian Z. Lubuva
MWENYEKITI
TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI
12/11/2015
Wednesday, November 11, 2015
HOTUBA YA NAIBU WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA, MHE. UMMY A. MWALIMU KATIKA UZINDUZI WA MKAKATI WA USAJILI WA VIZAZI KWA WATOTO WENYE UMRI WA CHINI YA MIAKA MITANO MKOANI MWANZA
HOTUBA YA NAIBU WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA, MHE. UMMY A. MWALIMU KATIKA UZINDUZI WA MKAKATI WA USAJILI WA VIZAZI KWA WATOTO WENYE UMRI WA CHINI YA MIAKA MITANO (THE UNDERFIVE BIRTH REGISTRATION INITIATIVE - U5BRI). MALAIKA HOTEL, TAREHE 11 MEI 2015
SOMA HAPA
Friday, July 10, 2015
HOTUBA YA MHESHIMIWA DR. JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WAKATI WA KUAGANA NA BUNGE NA KULIVUNJA BUNGE LA KUMI LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, UKUMBI WA BUNGE, DODOMA TAREHE 9 JULAI, 2015
Chanzo :ikulu
Mheshimiwa
Spika;
Tunayo kila sababu ya
kumshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa rehma kwa kutujalia uzima na kutuwezesha
kuishuhudia siku hii adhimu katika historia ya Bunge letu na nchi yetu.
Hatimaye siku ya kuvunja Bunge la Kumi imewadia ili kuwezesha hatua husika za
mchakato wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 ziweze kutekelezwa.
Nakushukuru sana
Mheshimiwa Spika kwa kunipatia nafasi hii ya kulihutubia Bunge lako tukufu ili
niweze kutimiza wajibu wangu huo wa msingi Kikatiba. Lakini, shukrani
zangu kubwa ni kwa uongozi wako mahiri na shupavu. Umeliongoza Bunge
vizuri. Najua haikuwa kazi rahisi. Penye wengi pana mengi. Lakini kwa
uhodari mkubwa umeweza kulifikisha jahazi bandarini salama salmini.
Hakika wewe ni nahodha makini na jemedari hodari, uliyethibitisha uhodari na
umakini wako katika uwanja wa medani. Wewe ndiwe mwanamke wa kwanza
kushika wadhifa huu wa juu kabisa katika mhimili huu wa kutunga sheria na
umeidhihirishia dunia kuwa wanawake wakipewa nafasi wanaweza.
Thursday, July 2, 2015
Majina ya Waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Tano,wilaya ya KWIMBA 2015/ 2016
OWM-TAMISEMI inawatangazia
majina ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano na Vyuo vya
Ufundi kwa mwaka 2015.Wanafunzi waliochaguliwa ni kutoka shule za Serikali na
zisizo za Serikali.
Jumla ya wanafunzi 55,003 wakiwemo wasichana 23,303 na wavulana31,700 wamechaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano na Vyuo vya Ufundi.
Kati ya wanafunzi waliochaguliwa 29,744 wakiwemo wasichana 11,450 nawavulana 18,294 sawa na asilimia 54.08 watajiunga na masomo ya Sayansina Hisabati; na wanafunzi 25,259 wakiwemo wasichana 11,853 nawavulana 13,406 sawa na asilimia 45.92 wamechaguliwa kusoma masomoya Sanaa na Biashara.
Jumla ya wanafunzi 55,003 wakiwemo wasichana 23,303 na wavulana31,700 wamechaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano na Vyuo vya Ufundi.
Kati ya wanafunzi waliochaguliwa 29,744 wakiwemo wasichana 11,450 nawavulana 18,294 sawa na asilimia 54.08 watajiunga na masomo ya Sayansina Hisabati; na wanafunzi 25,259 wakiwemo wasichana 11,853 nawavulana 13,406 sawa na asilimia 45.92 wamechaguliwa kusoma masomoya Sanaa na Biashara.
Friday, June 26, 2015
HOTUBA YA KAIMU KATIBU MTENDAJI WA BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI (NACTE) KUHUSU TAMKO LA BARAZA LA KUVIFUTIA USAJILI BAADHI YA VYUO NA KUVISHUSHA HADHI VINGINE
Ndugu waandishi wa
habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari, ninayo furaha kubwa kuwakaribisha
katika ofisi za Baraza. Lengo la kuwaita hapa leo ni kuwapa taarifa juu ya
maamuzi yaliyofikiwa na Baraza ikiwa ni katika jitihada za kuinua ubora wa
elimu ya ufundi nchini.
Ndugu Waandishi wa
Habari
Baraza la Taifa la Elimu
ya Ufundi ni chombo kilichoanzishwa kwa Sheria ya Bunge Sura ya 129, kwa lengo
la kusimamia na kuratibu taaluma zinazotolewa na taasisi na vyuo vva elimu ya
ufundi nchini, ambavyo siyo vyuo vikuu au vyuo vikuu vishiriki. Jukumu kubwa la
Baraza ni kuendeleza na kuinua ubora wa elimu ya ufundi nchini kwa kusimamia
kikamilifu shughuli za kuendesha mafunzo ili tuzo zinazotolewa na taasisi na
vyuo ziwe na ubora unaokubalika kitaifa na kimataifa.
Kwa kutumia Sheria na
Kanuni za Baraza za Usajili (2001) na zile za Ithibati na Utambuzi (2001),
mnamo tarehe 20 Februari 2015, Baraza lilitoa notisi ya siku 30 kwa taasisi na
vyuo vilivyokiuka taratibu na vyenye mapungufu makubwa ya Usajili na Ithibati kupitia
taarifa yake kwa Umma. Notisi hii ililenga kuzipa taasisi na vyuo nafasi ya
kujirekebisha.
Baraza linakiri kuwa
taasisi na vyuo vingi kama vilivyoorodheshwa kwenye Jedwali Na. 1, Jedwali Na.
3, na baadhi kwenye Jedwali Na. 5 vimechukua hatua mbalimbali za kurekebisha
mapungufu yaliyojitokeza. Hata hivyo, hadi kufikia leo tarehe 24 Juni 2015
yaani siku 124 baada ya Notisi ya Baraza, kuna vyuo ambavyo havijachukua hatua
yoyote ya kurekebisha mapungufu yake kama inavyooneshwa kwenye Jedwali Na. 2 na
Jedwali Na. 4.
Tamko la Baraza
Kutokana na mapungufu
hayo Baraza limeamua kuchukua hatua kwa mujibu wa Sheria na Kanuni zake kwa
taasisi na vyuo vyote vilivyoorodheshwa katika Jedwali Na. 2 na Jedwali Na. 4
kwa makosa yafuatayo:
a) Ama
kumalizika kwa muda wa Usajili wa Awali (Preparatory Registration) na
Usajili wa Muda (Provisional Registration); au
b)
Kutoanza mchakato wa kupata Ithibati baada ya kupata Usajili Kamili; au
c)
Kumalizika kwa muda wa Ithibati na kutochukua hatua ya kuomba upya Ithibati
(re-affirmation); na
d) Taasisi
na Vyuo kuamua vyenyewe kusitisha kutoa mafunzo kwa sababu mbalimbali.
Tuesday, June 16, 2015
MAENEO YA UTAWALA KATIKA MAMLAKA ZA SERIKALI ZA MITAA (MAMLAKA ZA WILAYA) MWAKA 2015 GN. 221 LA TAREHE 5/6/2015
Orodha kamili inayojumuisha Wilaya zote, Kata zake, vijiji na Vitongoji kwa ujumla unaweza kuipakua kupitia kiungo(link) hapo chini
PAKUA HAPA ORODHA KAMILI
Friday, June 12, 2015
Makadirio ya Idadi ya Wapiga Kura kwa Wilaya ya Kwimba Mwaka 2015
Makadirio ya idadi ya watu wenye umri wa
kupiga kura katika mkoa
wa Mwanza ni (1,403,743). Haya ni makadirio ya idadi ya watu ambao
watakuwa na umri wa miaka 18 na zaidi hadi kufikia uchaguzi wa
mwaka 2015.
wa Mwanza ni (1,403,743). Haya ni makadirio ya idadi ya watu ambao
watakuwa na umri wa miaka 18 na zaidi hadi kufikia uchaguzi wa
mwaka 2015.
Mkoa wa Mwanza una majimbo 9 ya uchaguzi. Jimbo la Buchosa
linaongoza kwa kuwa na idadi kubwa zaidi ya watu wenye umri wa
kupiga kura (217,733) likifuatiwa na Jimbo la Nyamagana (210,220).
Jimbo lenye idadi ndogo zaidi ya watu wenye umri wa kupiga kura
ni Sumve ambalo lina watu 87,993.
Hapa chini imewekwa orodha ya majimbo ya
wilaya ya kwimba, kata zake, makadirio ya idadi ya watu mwaka 2015 na makadirio
ya idadi ya watu wenye umri wa miaka 18 na zaidi
Kusoma idadi kamili ya Makadirio ya Idadi ya Wapiga Kura kwa Mkoa, Mwaka
2015
SOMA
HAPA=>>>>>> FUNGUA HAPA
Soma Bajeti ya Mwaka 2015/ 2016 Iliyowasilishwa na Waziri Wa Fedha Jana Bungeni
Waziri wa Fedha, Mhe. Saada Salum Mkuya (MB) akiwasilisha bungeni Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2015/16, Mjini Dodoma jana.
SOMA BAJETI YA MWAKA 2015/16 HAPA===>>>BAJETI YA MWAKA 2015/16
Monday, June 8, 2015
MULONGO AZINDUA MASHINDANO YA U13 TAIFA JIJINI MWANZA
Mkuu
wa mkoa wa Mwanza Mh. Magessa Mulongo
jana kwenye uwanja wa CCM Kirumba akifungua mashindano ya Taifa ya vijana umri
chini ya miaka 13
Akifungu mashindano hayo Mh Mulongo amewataka vijana
hao kujituma katika michezo na masomo kwa kuwa vyote vinakwenda sambamba
Amesisitiza shirikisho la mpira Tanzania TFF
kuongeza juhudi katika kuendeleza soka la vijana
Katika salamu zake za utangulizi Rais wa TFF Jamal
Malinzi ameeleza kuwa lengo la mashindano hayo ni kuibua timu ya vijana wenye
umri wa miaka 13 ambao watahamishiwa kwenye shule ya Alliance, watakuwa hapo
kusoma na kufundishwa mpira.
Mpango wa TFF ni kuwa hadi kufikia mwaka 2019 timu
hii itakuwa imara kuiwakilisha Tanzania katika mashindanoya fainali za Afrika
umri chini ya miaka 17, fainali ambazo zitafanyika Tanzania
Mikoa yote 25 ya Tanzania bara inashiriki mashindano
haya na mkoa wa Dar es salaam umewakilishwa na timu tatu Kinindoni, Ilala na
Temeke.
TFF inashukuru Symbion power kwa ushirikiano wa
kuendeleza mpira wa vijana
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA(TFF)
MWANZA : Takukuru yawaburuza kortini vigogo watatu wa Serikali
TAASISI ya Kupambana na Kudhibiti Rushwa nchini (TAKUKURU)
imewaburuza mahakamani vigogo watatu wa Serikali kwa makosa mawili
ya matumizi mabaya ya madaraka na kutumia nyaraka mbalimbali
kumtapeli mwajiri wao.
Vigogo hao ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Msalala
Mkoa wa Shinyanga, Patrick Karangwa (45), Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya
ya Magu Mkoa wa Mwanza, Ntinika Paul (51) na Mhasibu Mkuu wa Wilaya ya Magu,
Mathayo Masuka.
Walifikishwa wiki iliyopita katika Mahakama ya Wilaya ya
Nyamagana Mkoa wa Mwanza, mbele ya Hakimu Mkuu Mfawidhi wa Mahakama hiyo,
Janeth Masesa.
Ilidaiwa kuwa watuhumiwa hao walitenda makosa hayo mwaka 2009
wakati wakiwa wafanyakazi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza.
Ilielezwa kuwa wakati wakitenda makosa hayo, Karangwa alikuwa
Mchumi Mkuu Jiji la Mwanza, Paul alikuwa mweka hazina mkuu wa
jiji hilo wakati Masuka alikuwa mkaguzi wa ndani wa jiji la Mwanza.
Watuhumiwa hao walikana mashtaka hayo na wapo nje kwa dhamana na
kesi hiyo inatarajiwa kutajwa tena Juni 11 mwaka huu.
Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Mwanza, Kasomambuto Mbengwa,
alithibitisha taasisi hiyo kuwakifikisha vigogo hao mahakamni.
Wednesday, June 3, 2015
Sunday, May 24, 2015
Ajira Mpya Kwa Walimu 2015........Haya Ni Majina Ya Awamu Ya Pili Pamoja Na Mabadiliko Ya Vituo Vya Kazi
Tarehe 27 na 30 Aprili, 2015, Ofisi ya Waziri
Mkuu - TAMISEMI ilitangaza ajira ya wahitimu wa mafunzo ya ualimu
na mafundi sanifu wa maabara kwa kuweka orodha kwenye
tovuti ya www.pmoralg.go.tz. Iliagizwa kuwa
waajiriwa wapya walipaswa kuripoti katika Mamlaka za Serikali
za Mitaa kuanzia tarehe 01 hadi 09 Mei, 2015.
Napenda kuchukua nafasi hii kuutaarifu umma kuwa
ofisi yangu ilipokea na kuchambua maombi ya walimu
ambao hawakuajiriwa awali; na walioomba kubadilishiwa vituo kutokana
na matatizo mbalimbali.
Vilevile ofisi imezingatia kuwapanga tena
walimu ambao kwa sababu za msingi walishindwa kuripoti kufikia
tarehe 09 Mei, 2015.
Walimu wote waliopo katika orodha ya awamu ya pili wanapaswa
kuripoti kuanzia tarehe 01 hadi 05 Juni, 2015 kwenye ofisi za
Wakurugenzi wa Halmashauri kwa ajili ya kuajiriwa na kupangiwa vituo vya kazi.
Orodha ya walimu hao watakaoajiriwa katika halmashauri
husika imegawanywa katika makundi yafuatayo:-
i. walimu wa cheti (Daraja IIIA) waliokosa ajira kwa awamu
ya kwanza;
ii. walimu wa cheti (Daraja IIIA) waliobadilishiwa vituo;
iii. walimu wa masomo ya sanaa kwa ajili
ya shule za sekondari ambao hawakupangiwa vituo;
iv. walimu waliobadilishiwa vituo wa masomo ya sanaa
kwa ajili ya shule za sekondari;
v. walimu wa masomo ya sayansi na hisabati kwa ajili ya
shule za sekondari ambao hawakupangiwa vituo; na
vi. walimu waliobadilishiwa vituo wa masomo ya
sayansi na hisabati kwa ajili ya
shule za sekondari.
Utaratibu wa Ajira ya Walimu Awamu ya Pili
Kila mwajiriwa mpya anatakiwa kuzingatia yafuatayo:-i.
kuwasilisha vyeti halisi vya taaluma ya kuhitimu mafunzo ya ualimu, elimu
ya sekondari, cheti cha kuzaliwa pamoja na nakala zake; na
ii. atalipwa posho ya kujikimu kwa muda wa siku saba
(7) na nauli ya usafiri wa magari (ground travel), malipo hayo yatatolewa na
halmashauri husika.
Angalizo
i. Walimu ambao wamekwisharipoti na mchakato wao wa ajira
umeanza katika Mamlaka za Serikali za Mitaa hawatahusika na
mabadiliko haya hivyo waendelee kufanya kazi katika halmashauri
husika na hawahusiki na upangaji wa awamu hii.
ii. Walimu ambao walichelewa kuripoti tarehe 9 Mei, 2015
na majina yao hayajaonekana katika mabadiliko haya wanatakiwa waende kuajiriwa
katika halmashauri walizopangwa awali (kwa kuzingatia orodha iliyotolewa kwenye
tovuti tarehe 30/4/2015). Aidha, walimu wa masomo ya sanaa ambao
hawakuripoti katika Halmashauri za Wilaya za Meru na Arusha wamebadilishwa
vituo.
iii. Walimu waliopangwa ni wale wa masomo ya
sanaa/biashara na cheti waliohitimu mafunzo kwa mwaka wa masomo 2013/14 na
wahitimu wa miaka ya nyuma wa masomo ya sayansi na hisabati kwa ajili ya
kufundisha katika shule za sekondari.
iv. Kituo cha kazi cha mwalimu ni shule na sio Makao Makuu
ya Halmashauri, posho italipwa baada ya mwalimu kuripoti na kuandika
barua kupitia kwa
Mkuu wa Shule.
v. Mwalimu hatapokelewa na kuaajiriwa kama ikitokea yupo
katika orodha na amehitimu shahada au stashahada zisizo za ualimu na wenye
shahada za ualimu zisizo na somo au masomo ya kufundishia katika shule za
sekondari.
vi. Ikibainika kuna mwalimu atakayekwenda kuripoti na kuchukua
posho na kuondoka, atachukuliwa hatua kwa mujibu wa Sheria.
Ni muhimu kuzingatia maelekezo haya, ikiwa ni pamoja na muda
uliowekwa kuripoti kuepuka usumbufu unaoweza kujitokeza.
Limetolewa na
Ndg. Jumanne A. Sagini
KATIBU MKUU
OFISI YA WAZIRI MKUU-TAMISEMI
______________
5.Orodha ya Walimu wa Sanaa(Shahada/Stashahada) Awamu ya Pili Waliopangiwa Vituo Vipya - 23 Mei 2015
Thursday, May 21, 2015
ZIARA YA MBUNGE WA JIMBO LA KWIMBA KWA WANANCHI WAKE
Mbunge wa Kwimba Mansoor amepata mapokezi makubwa jimboni kwake. |
Akiwa ameambatana na Katibu wa mkoa wa Mwanza Bw. Miraji Mtaturu, Mbunge huyo amekabidhi kadi 1600, mifuko ya saruji 600 yenye thamani ya shilingi milioni 12 na kuviwezesha vikundi mbalimbali zaidi ya shilingi milioni 5.
wanachama wapya |
MBUNGE MANSOOR, JIMBO LA KWIMBA LIMEBADILIKA
NA KUPIGA HATUA YA
MAENDELEO KWA VITENDO.
MBUNGE wa Jimbo la Kwimba, Shanif Mansoor,ametamba kuwa wananchi wa
jimboni humo wajivune kwa kushirikiana nae kuleta maendeleo kwa vitendo na
kulibadilisha badala ya kusikiliza uzushi wa baadhi ya wapinzani wake kisiasa
wanaoendekeza ukabila.
Pia amekuwa akichangia miradi ya maendeleo ambapo metoa kiasi cha shilingi milioni 17 za kutekeleza ahadi zake za maendeleo na Ilani ya Uchaguzi ya CCM kwa vitendo katika Jimbo lake.
Mansoor alikabidhi saruji mifuko 600 katika Kata za Mhande, Fukalo, Ngudu na Bupamwa kwa ajili ya kusaidia ujenzi kwenye shule za msingi, zahanati na sekondari pamoja na kuchangia fedha na vifaa vya Kompyuta kwenye baadhi ya sekondari na Chuo cha Afya cha Ngudu mjini.
Mbunge Mansoor akizungumza na mamia ya wananchi waliofurika kwenye mkutano wa hadhara juzi uliofanyika katika viwanja vya stendi mjini Ngudu, alisema kwamba saruji hiyo aliyoitoa katika Kata ya Bupamwa kwenye vijiji vya Dodoma, Kiliwi na itegamatwi kwa ujenzi wa vyumba vya madarasa shule za msingi.
Katika Kata ya Fukalo alitoa saruji katika vijiji vya Sanga, Msongwa, Chibuji kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule za msingi, Kata ya Mhande ni kijiji cha Gurumwa kwa ajili ya kusaidia pia ujenzi wa shule ya msingi na milioni tatu kwa maabara ya sekondari na Kata ya Ngudu mjini alitoa fedha kiasi cha shilingi milioni mbili sekondari ya Bujiku Sakila na shilingi milioni moja Ngudu mjini.
Maeneo mengine aliyochangia ni Chuo cha Afya Ngudu mjini shilingi milioni 2 kwa ajili ya ujenzi wa choo na kutoa Komputa tatu(sh. 1.8 mil), kuchangia saruji mifuko 50 kanisa la Romani (RC) na mifuko 50 kanisa la Afrika Iniland Charch Tanzania (AICT) katika kijiji cha Kilyaboya na kikundi cha ujasilimali Ngudu mjini kilipata shilingi laki tano.
Mansoor aliwaeleza wananchi kuwa katika fedha hizo za kuchangia maendeleo hazihusiani na Mfuko wa Jimbo la Kwimba bali kutokana na nguvu yake kwa lengo la kuwasaidia wananchi ili kupiga hatua ya maendeleo, ambapo al katika Kata ya Ngudu mjini alichangia saruji pia vijiji vya Gudula (shule) na Chamela (jengo la Kiliniki).
“Thamani ya saruji ambayo leo nimeitoa kusaidia wananchi katika vijiji hivyo ni shilingi milioni 12 na jumla ya fedha zilizokabidhiwa ni shilingi milioni tano tasilimu hivyo hapa misaada yote imegharimu kiasi shilingi milioni 17 jambo ambalo ni la kujivunia kwa wananchi kwa kuwa na Mbunge anayetambua maendeleo,”alisema.
Mansoor alitamba kuwa kwa kipindi chake cha uwakilishi kwa wananchi amefanya mambo makubwa kusimamia ikiwemo, usambazaji umeme vijijini katika Kata, kupigania maji safi kutoka chanzo cha Ziwa Victoria cha Ihelele, Shinyanga- Kahama ambayo huduma imefika na barabara ya Hungumalwa, Ngudu-Magu kwa kiwango cha lami ambayo tayari upembuzi yakinifu utaanza hivi karibuni.
Mbunge huyo alitoa wito kwa wananchi wa Jimbo la Kwimba kumpatia ushirikiano kutekeleza yale aliyoahidi kwao na kutekeleza Ilani ya CCM kwa vitendo na kuwapuuza baadhi ya wanasiasa wachache walioanza kupitapita huku wakimchafua na kuanza kuhamasisha ukabila jambo ambalo alisema wananchi wanapashwa kutafakari na kuwataka wapinzani wake waeleze sela na hoja zitakazowashawishi kuwachagua.
chanzo: gsengo blog.
Subscribe to:
Posts (Atom)