Sunday, December 7, 2014

MASWALI YA MBUNGE WETU MANSOOR SHANIF HIRAN BUNGENI.

HAYA NDO MASWALI ALIYOULIZA BUNGENI MBUNGE WANGU Shanif Mansoor Hiran TANGU NIMCHAGUE KUNIWAKILISHA., Je nimpe kura mwaka 2015? Anafaa kuniongoza?


 1. REGIONAL ADMINISTRATION AND LOCAL GOVERNMENT 4 July 2011 Mji mdogo wa Ngudu ambao ndio Makao Makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba, una wakazi wengi na taasisi mbalimbali zinazotoa huduma za kijamii na kiuchumi lakini una matatizo makubwa ya maji ambayo hutokana na uchakavu wa pampu mbili za kuvuna maji na pump moja ya kusukuma na kusambaza maji kutoka kwenye vyanzo vya maji vilivyo eneo la Kilyaboya. Gharama za pump hizo kwa pamoja hazizidi shilingi milioni hamsini za Kitanzania. Je, Serikali inajipanga vipi kuhakikisha tatizo hili la maji linamalizika kwa wakati ili kuondoa kero hiyo iliyopo kwa muda mrefu sasa?


 2. WIZARA YA AFYA 30 October 2013 SWALI HILI INAWEZEKANA MH WANGU HAKUWEPO BUNGENI AKAMUAGIZA JIRANI YAKE AULIZE KWA NIABA YAKE, (MHE RICHARD M. NDASSA) Hivi sasa kuna mkanganyiko juu ya dawa gani inayoweza kutibu malaria:- Je, ni dawa gani sahihi inayotibu malaria?


 3. Transport/Road 10 August 2011 Rais wa Jamhuri ya Muungano wakati wa ziara yake ya Kampeni Wilayani Kwimba tarehe 25/10/2010 aliahidi kuboresha barabara za Wilaya hiyo kwa kiwango cha lami:- Je, Serikali inasema nini juu ya utekelezaji wa ahadi hiyo kwa kuboresha barabara kwa kiwango cha lami kutoka Magu Mjini kupitia Ngudu hadi Hungumalwa?

 4. WIZARA YA NISHATI NA MADINI 13 April 2012 Ni muda mrefu sana Serikali imekuwa ikiahidi kuupatia Mji wa Ng’hungumalwa umeme wa Gridi ya Taifa:- Je, ni lini Serikali itakamilisha mpango wa kupeleka umeme katika Mji wa Ng’hungumalwa na Vitongoji vya Sangu, Mwaluja na Tarafa za Mwamashimba, Nyamilama na Kata zingine ambapo pana shughuli za kiuchumi kama vile Cotton Ginneries na mashine za kusaga/kukoboa nafaka?

mwandishi:  luteja abel.

No comments:

Post a Comment

Previous Page Next Page Home