Saturday, January 24, 2015

RAIS KIKWETE KAFANYA MABADILIKO KWENYE BARAZA LA MAWAZIRI



Katibu mkuu kiongozi, Balozi Ombeni sefue akizungumza na vyombo vya habari jioni hii wakati akitangaza mabadiliko madogo ya baraza la mawazili, Ikulu jijini Dar es salaam
Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania, Dkt Jakaya Mrisho Kikwete leo amefanya mabadiliko madogo katika Baraza lake la mawaziri, ambalo Ameliapisha jioni hii Ikulu jijini Dar es salaam
Hayo yamefanyika ikiwa ni baada ya aliyekuwa waziri wa Nishati na Madini kujiuzulu wadhifa wake

Hawa ndiyo Mawaziri 8 walioteuliwa na rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete leo
 
1.George Simbachawene- Waziri wa Nishati na Madini
2.Mary Nagu -Waziri wa nchi Mahusiano na Uratibu
3.Harrison Mwakyembe - Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki. 
4.Wiliam Lukuvi - Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi
5.Steven Wassira - Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika
6.Samwel Sitta - Waziri wa Uchukuzi
7.Jenista Mhagama - Waziri wa Sera na Uratibu wa Bunge 

8.Christopher Chiza- Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji na Uwezeshaji 



Manaibu Waziri  5 walioteuliwa
1.Steven Masele - Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano
2.Angellah Kairuki - Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Makazi
3.Ummy Mwalimu- Naibu Waziri wa Katiba na Sheria
4.Anna Kilango- Naibu waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi
5.Charles Mwijage - Naibu Waziri wa Nishati na Madini

Saturday, January 17, 2015

MATOKEO YA KIDATO CHA PILI


Baraza la mithani nchini limetangaza matokeo ya kidato  cha pili yaliyofanyika mwaka 2014 huku idadi kubwa ya  wanafunzi wakiwa wamefaulu na kujiunga na kidato cha  tatu, ikiongezeka kwa asilimia 92.66 ikilinganishwa na  mwaka 2013 ambapo idadi ya wanafunzi waliofaulu  ilikuwa asilimia 89.34 matokeo hayo yametangazwa leo jijini Dar es salaam na  katibu Mkuu wa Baraza la Mitihani nchini NECTA Dr  Charles E Msonde wakati wa mkutano na waandishi wa habari ambapo alisema watahiniwa waliofanya mtihani huo uliofanyika novemba mwaka jana ilikuwa 405,204 sawa na asilimia 89.40. Kati ya hao wasichana walikuwa 233.834 sawa na asilimia 51.60 na wavulana walikuwa 219.357 sawa na asilimia 48.40

Dkt Msonde alisema kati ya watahiniwa hao waliofaulu na kupata alama za kuweza kuendelea na kidato cha tatu walikuwa 375,434 sawa na asilimia 92.6 ya watahiniwa wote waliofanya mtihani huo ambapo wasichana walikuwa 195,328 sawa na asilimia 92.8 na wavulana 180106 sawa na asilimia 92.69

Aidha Dokta Msonde aliwataja watahiniwa ambao wamepata alama ambazo hawawezi kuendelea na kidato cha tatu na itawalazimu kurudia kidato cha pili ambapo wapo 29770 sawana asilimia 7.34

Vilevile ameyataja masomo waliyofanya vizuri watahiniwa hao ni uraia, historia, kiswahili, kingereza na jeografia. Pia kwa masomo walifanya vibaya ni Hisabati, Kemia, kilimo, somo la biashara pamoja, fizikia pamoja na jeografia.

Kwa upande wa shule za wilaya yangu, hasa za mjini hapo ambazo ni pamoja na NGUDU SECONDARY SCHOOL na BUJIKU SAKILA kuna baadhi ya matokeo ya wanafunzi waliofanya vizuri  zaidi kama inavyooneshwa hapo chini kwenye majedwali  

Wednesday, January 7, 2015

Mkuu wa mkoa wa Mwanza atoa siku tano kwa wanakijiji kwimba kuhakikisha wanampata mtoto Albino Aliyetekwa tangu Disemba 27, 2014


Mkuu wa mkoa wa Mwanza Magesa Mulongo ametoa muda wa siku tano kwa wakazi wa kijiji cha Ndami na jeshi la jadi Sungusungu wilayani kwimba, kuhakikisha wanampata mtoto mwenye ulemavu wa ngozi – Alibinism, Pendo Emanuel akiwa hai au amekufa ikiwa ni pamoja na wahusika wa tukio hilo kukamatwa na kufikishwa katika vyombo vya dola.

Agizo hili la mkuu wa mkoa wa Mwanza Magesa Mulongo, linakuja kufuatia watu wasiojulikana kumuiba mtoto Pendo Emanuel mwenye ulemavu wa ngozi majira ya saa 4 usiku Desemba 27 mwaka jana nyumbani kwao katika kijiji cha Ndami na kutoweka naye kusikojulikana, mkasa ambao umeilazimu kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wa Mwanza kuapa kuwa serikali haitalala usingizi mpaka mtoto huy mwenye umri wa miaka minne apatikane.
 
Mwenyekiti wa chama cha watu wenye ulemavu wa ngozi mkoa wa Mwanza Alfred Kapole amesema kuwa miongoni mwa kesi 72 zilizokuwa mahakamani zikihusu mauaji ya walemavu wa ngozi, ni kesi tatu ndizo zilizotolewa hukumu mpaka sasa, huku akiilaumu ofisi ya mkemia mkuu wa serikali pamoja na mahakama kwa kuchelewesha kesi hizo.
 
Mama mzazi wa mtoto Pendo, Bi. Sophia Juma pamoja na mkurugenzi wa shirika lisilokuwa la kiserikali la Chiriko Bi. Specioza Kasoli wamesema kila mtu ana haki ya kuishi na kulindwa na kuongeza kwamba mtoto huyo ni kati ya watu 74 wenye ulemavu wa ngozi wilayani kwimba na alikuwa ni mtu wa 9 kwa kupatiwa ulinzi.
 
Kamanda wa Polisi mkoani Mwanza Valentino Mlowola amesema tayari askari polisi wamepiga kambi katika kijiji hicho kwa kazi moja tu ya kuhakikisha mtoto huyo anapatikana, lakini pia watuhumiwa wanasakwa kwa udi na uvumba ili wafikishwe mahakamani kwa kosa la jinai.

Tuesday, January 6, 2015

ZIFAHAMU SIFA, MAJUKUMU YA DIWANI WAKO, KISHA JITOKEZE KULETA MABADILIKO KWENYE JAMII YAKO.

Diwani ni mwakilishi aliyechaguliwa kusimamia utekelezaji wa majukumu ya Serikali za Mitaa.  Madiwani ndio wanaounda Halmashauri za Serikali za Mitaa na ndio wenye mamlaka ya kutekeleza majukumu ya Serikali za Mitaa.  Sheria za Serikali za Mitaa zimeainisha majukumu ya kutekelezwa na Mamlaka hizi kuwa ni ya kuwaletea wananchi maendeleo kwa kuwapatia huduma bora na kwa gharama nafuu. Majukumu hayo ya Serikali za Mitaa ni haya yafuatayo:
             i.                Kulinda na kutunza utulivu na amani na kusimamia Utawala Bora;

      ii.           Kuendeleza ustawi wa jamii na kuinua uchumi wa wananchi wake ikiwemo kuimarisha afya, elimu, utamaduni, burudani na ustawi wa wananchi wake;

           iii.                Kuhakikisha maendeleo ya kiuchumi na kijamii yanapatikana kwa mujibu wa Sera za Taifa za Maendeleo Mijini na Maendeleo Vijijini;

           iv.                Kuhakikisha na kuchukua hatua zozote zinazofaa katika kuzuia au kuondoa uhalifu na kulinda watu pamoja na mali zao;

            v.                Kuimarisha na kuendeleza kilimo, viwanda na biashara;

           vi.                Kuuondoa umaskini na kero nyingine katika jamii hususan kwa kuzingatia makundi ya vijana, wazee na walemavu wa aina mbalimbali na wale wasiojiweza;

         vii.                Kuhimiza dhana ya ushirikishwaji wa wananchi, vyama vya hiari na visivyo vya hiari katika kujiletea maendeleo;

        viii.                Kubuni vyanzo mbalimbali vya mapato vya kuwezesha Halmashauri kutekeleza majukumu yake niliyoyataja hivi punde.


Hayo ndiyo majukumu ya Serikali za Mitaa ambayo msimamizi mkuu katika halmashauri ni Diwani.

ZIFAHAMU KATA, VIJIJI NA VITONGOJI VYA WILAYA YAKO


MAENEO YA UTAWALA KATIKA MAMLAKA ZA SERIKALI ZA MITAA (MAMLAKA ZA WILAYA) MWAKA 2014
Kwa mujibu wa takwimu zilivyo kwenye tovuti ya ofisi ya waziri mkuu, wilaya ya kwimba ina kata, vijiji na vitongoji kama ifutavyo
1.  NYAMBITI
-vijiji (Nyambiti, kinoja, solwe, ibindo, mwankuba)
-Na vitongoji 33 jumla

 2. MWANDU
-Vijiji (Goloma, Isabilo, Mwandu, Shushi)
Vitongoji jumla 30

3.  MALYA
-Vijiji (Malya, Mwahembo, Talaga, Mwitambu,Kitunga)
-Vitongoji jumla 31

4.  MWAGI
-Vijiji (Ligembe, Kishili, Mwamajila, Mwabilanda)
-Vitongoji jumla 26

5.  NKALALO
-Vijiji (Nkalalo, Manawa, Mwaging’hi,)
-Vitongoji jumla 16

Thursday, January 1, 2015

MSANII BOB HAISA KUTOA BURUDANI YA NGUVU UKUMBI WA KWIDECO NGUDU MJINI LEO TAR 1/1/2015


TAARIFA KUHUSIANA NA MTOTO MWENYE ULEMAVU WA NGOZI ALIYETEKWA HUKO TARAFA YA MWAMASHIMBA WILAYANI KWIMBA.


Jeshi la polisi mkoani mwanza linawashikilia watu wanne, akiwemo baba mzazi, Emmanuel shirinde(28) wa mtoto mwenye ulemavu wa ngozi, pendo emmanuel ambaye aliporwa na watu wasiojulikana waliovamia nyumbani kwao

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza, Valentino Mlowola, tukio la uporwaji wa mtoto huyo lilitokea Desemba 27, mwaka huu saa 4.30 usiku katika kijiji cha Ndami tarafa ya Mwamashimba wilayani Kwimba mkoani hapa.

Akifafanua, Kamanda Mlowola alisema siku ya tukio saa 4.30 usiku Shirinde akiwa amelala nyumbani kwake na familia yake, akiwemo Pendo, walivamiwa na watu wawili wasiojulikana.
 

SALAMU ZA MWAKA MPYA ZA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHESHIMIWA DKT. JAKAYA MRISHO KIKWETE KWA WATANZANIA, TAREHE 31 DESEMBA, 2014


Utangulizi
Ndugu zangu;
Watanzania Wenzangu;
Kama ilivyo ada imefikia siku ya kuuaga mwaka mmoja na kuukaribisha mwaka mwingine. Leo tunauaga mwaka 2014 na kuukaribisha mwaka mpya wa 2015. Tunamshukuru Muumba wetu mwingi wa rehema kwa kutujaalia uzima na kutuwezesha kuifikia siku ya leo. Kwa ndugu na jamaa zetu ambao hawakujaliwa kuiona siku ya leo tuzidi kuwaombea mapumziko mema.  Nasi tumuombe Mwenyezi Mungu, mwingi wa rehema atujaalie umri mrefu, afya njema na mafanikio tele kwa kila tuliombalo katika mwaka 2015 na miaka ijayo.
Ndugu wananchi;
          Hizi ni salamu zangu za mwisho za mwaka mpya kutoa nikiwa Rais wa nchi yetu. Mwakani salamu kama hizi zitatolewa na Rais wetu mpya.  Mimi wakati huo nitakuwa raia wa kawaida kijijini kwangu Msoga nikifuatilia kwenye TV na radio hotuba ya Rais wa Awamu ya Tano ya uongozi wa nchi yetu akitoa salamu zake za kwanza za  mwaka mpya, itakuwa siku ya furaha na faraja kubwa kwangu.
Previous Page Next Page Home