Thursday, February 18, 2016

MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE(CSEE) 2015- WILAYA YA KWIMBA


Baraza la Mitihani (NECTA) leo Februari 18, 2016 limetoa Matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Nne uliofanyika mwishoni mwa mwaka 2015.

Akitangaza Matokeo hayo katibu Mtendaji wa Baraza hilo Dkt Charles Msone amesema jumla watahiniwa 272,947 sawa na 67.53% ya watahiniwa waliofanya mtihani wa kidato cha nne 2015 wamefaulu tofauti na mwaka 2014 ambapo ufaulu ulikuwa 68.33%.

Upande wa watahiniwa wa shule, waliofaulu ni 240,996 sawa na asilimia 67.91 ya waliofanya mtihani, wasichana wakiwa 11,125 (64.84) na wavulana wakiwa 124,871 (71.09). 


Upande wa watahiniwa wa shule, ufaulu umeshuka kwa asilimia 1.85 ikilinganishwa na mwaka 2014.

Kwa upande wa watahiniwa wa kujitegemea, watahiniwa 31,951 sawa na asilimia 64.80 wamefaulu ikilinganishwa na watahiniwa 29,162 (61.12) waliofaulu mwaka 2014.

Kwa upande wa ubora wa ufaulu kwa kuangalia madaraja waliyopata watahiniwa wa shule, amesema waliopata daraja la Kwanza ni 9,816 sawa na asilimia 2.77, daraja la pili ni 31,986 sawa na asilimia 9.01, daraja la tatu ni 48,127 sawa na asilimia 13.56.

Waliopata daraja la nne ni 240,996 sawa na asilimia 67.91 na waliopata daraja la sifuri (waliofeli) ni 113,489. Watahiniwa waliopata ufaulu mzuri wa kati ya daraja la kwanza hadi la tatu ni 94,941 sawa na asilimia 24.73 wavulana wakiwa 56,603 sawa na 29.99 na wavulana 38,338 sawa na asilimia 19.63.



Amezitaja shule 10 zenye watahiniwa zaidi ya 40 zilizofanya vizuri zaidi kuwa ni Kaizerege ya mkoani Kagera, Alliance Girls ya Mwanza, St. Francis Girls ya Mbeya, Canossa ya Dar es salaam, Marian Boys ya Pwani, Alliance Rock Army ya Mwanza, Feza Girls Dar es salaam, Feza Boys ya Dar es salaam na Uru Seminary ya Kilimanjaro.


Shule 10 zilizofanya vibaya zaidi kwa watainiwa zaidi ya 40 ni pamoja na Pande ya mkoani Lindi, Igawa ya Morogoro, Korona ya Arusha, Sofi ya Morogoro, Kurui ya mkoani Pwani, Patema ya Tanga, Saviak ya Dar es salaam, Gubali ya Dodoma, Kichangani ya Morogoro na Malinyi ya Morogoro.

Kwa upande wa watahiniwa, Dkt Msonde amesema kati ya watahiniwa 10 waliofanya vizuri zaidi, wanne ni  wasichana na sita ni wavulana.

Mwanafunzi aliyeongoza ni msichana Butogwa Charles Shija wa Canossa, akifuatiwa na msichana mwingine Congcong Wang wa Feza Girls na wa tatu ni mvulana Innocent Lawrence wa Feza Boys.

Wengine ni Dominick Marco Aidano wa Msolwa, Sang'udi E Sang'udi wa Ilboru, Asteria Herbert Chilambo wa Canossa, Belinda Jackson Magere wa Canossa, Humfrey Martine Kimanya wa Msolwa, Bright B Mwang'onda wa Marian Boys na wa 10 ni Erick R Mwang'ingo wa Marian Boys.

Matokeo hayo yamepangwa katika mfumo wa madaraja (Division) badala ya ule wa wasatani wa alama (GPA) kama ambavyo iliagizwa na Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi hivi karibuni.

MATOKEO  YA SHULE ZILIZOPO WILAYA YA KWIMBA.

Matokeo haya yamewekwa kwa mtririko wa  shule na kiungo(link) ya matokeo ya shule husika. Hii itarahisisha kwenda moja kwa moja kwenye shule unayotaka kuona matokeo yake..

































MWANDU

MWANKULWE

MATOKEO YA TANZANIA NZIMA UNAYAPATA>>>>>>MATOKEO YOTE HAPA

No comments:

Post a Comment

Previous Page Next Page Home