Monday, February 2, 2015

KUHUSU SERIKALI ZA MITAA




























Utawala wa Kijiji ni miongoni mwa tawala katika serikali za mitaa za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni utawala wa chini kabisa kimuundo ukitanguliwa na utawala wa Kitongoji. Kuwa utawala wa chini haimaanishi kuwa na umuhimu mdogo, isipokuwa ni kupitia utawala huu ndiko ambako mambo mengi yanayoamuriwa au kupangwa na tawala za juu kama serikali, hutekelezwa. Utawala wa kijiji huelekeza wananchi katika kutumia madaraka yao ya kidemokrasia kuamua juu ya mambo yanayowahusu kama wanakijiji moja kwa moja bila kupitia mlolongo au urasimu mrefu. Mambo yanayohusiana na tawala za serikali za mitaa yanaratibiwa  na Ofisi ya Waziri Mkuu.

Mkutano Mkuu wa Kijiji ni chombo cha utawala kinachoundwa na wajumbe wafuatao:
·        Wakazi wote wa Kijiji wenye umri usiopungua miaka 18 na wenye akili timamu.
·        Mwenyekiti wa Kijiji.
·        Wenyeviti wa Vitongoji vyote kijijini.
·        Wajumbe wa Halmashauri ya Kijiji ambao ni kati ya 15 na 25.
·        Afsa Mtendaji wa Kijiji – Katibu.

Kwa mujibu wa kifungu cha 103 (2) cha sheria namba 7 ya mwaka 1982. Mkutano Mkuu wa Kijiji huitishwa mara mmoja kila baada ya miezi mitatu.
Kwa mujibu wa kifungu cha 141 cha sheria namba 7 ya mwaka 1982, Mkutano Mkuu ndiyo Mamlaka yenye madaraka ya juu kabisa kuhusu maamuzi yote ya sera na maendeleo kijijini na ndiyo yenye wajibu wa kuwachagua na kuwaondoa madarakani wajumbe wa Halmashauri ya Kijiji ikiwa ni pamoja na kutekeleza majukumu mbalimbali iliyopewa kwa mujibu wa sheria hii na nyingine.

Kila baada ya miaka mitano kinakuwa na Mkutano Mkuu Maalum wa uchaguzi wa Mwenyekiti na wajumbe wa halmshauri ya Kijiji. Mkazi wa kijiji anayegombea nafasi ya uongozi kwenye halmashauri ya kijiji au uenyekiti wa kijiji lazima awe na umri usiopungua miaka 21. Mwenyekiti wa Mkutano Mkuu ni Mwenyekiti wa kijiji akisaidiwa na Afisa Mtendaji wa Kijiji(VEO). Mwenyekiti na Afisa Mtendaji wa Kijiji (VEO) hupanga ratiba za vikao, kuandaa na kuitisha vikao vya Mkutano Mkuu wa Kijiji.
Muundo wa Halmashauri ya Kijiji
Halmshauri ya kijiji ni chombo kikuu cha utendaji katika utawala wa kijiji. Hukutana mara moja kila mwezi, mikutano ya dharura inaweza kuitishwa. Akidi (qorum) ya vikao vya halmshauri ya kijiji ni nusu ya wajumbe wote wa halmashauri ya kijiji. Wakati Mkutano Mkuu ni kama Bunge, halmshauri ya kijiji ni kama serikali. Huchaguliwa na Mkutano Mkuu wa Kijiji. Uchaguzi wa halmashauri wa kijiji husimamiwa na Mkurugenzi wa halmshauri ya Wilaya. Mkazi wa kijiji mwenye umri usiopungua miaka 21 ana sifa za kuchaguliwa kwenye halmshauri ya kijiji. Wajumbe wa halmashauri ya kijiji wanatakiwa wasizidi 25 na wasiopungua 15. Mkutano Mkuu kwa kushirikiana na Msimamizi wa uchaguzi idadi ya wajumbe wanayotaka kutokana na mazingira yao kutegemea na wingi wa wakazi na ukubwa wa eneo lao (idadi ya vitongoji). Wajumbe wa halmashauri ya kijiji ni Mwenyekiti wa kijiji, wenyeviti wa vitongoji, wanawake ambao watakuwa theluthi moja ya wajumbe wote na wajumbe wengine. Mwenyekiti wa kijiji ni mwenyekiti wa halmshauri ya kijiji na mwenyekiti wa Mkutano Mkuu. Wenyeviti wa vitongoji huchaguliwa na wakazi wa vitongoji huingia kwenye halmashauri ya kijiji kwa mujibu wa nyadhifa zao.

Wajibu na Majukumu ya Mkutano Mkuu wa Kijiji
·        Kupokea na kujadili taarifa za utekelezaji wa shughuli mbalimbali.
·        Kupokea na kujadili mapato na matumizi ya fedha.
·        Kupokea na kujadili taarifa za makusanyo ya fedha yakiwamo ya ushuru, ada na mapato
 mengine yanayopaswa kukusanywa ndani ya kijiji kwa mujibu wa sheria

·        Kupokea na kujadili taarifa za watu walioomba kupewa ardhi.
·        Kupokea na kujadili mapendekezo yatakayotolewa na Halmashauri ya Kijiji au Kitongoji.
·        Kupokea maagizo (kama yapo) kutoka ngazi za juu za Serikali na kuweka mkakati wa utekelezaji.
·        Kufanya maamuzi yanayozingatia demokrasia.
·        Kuchagua Mwenyekiti na Wajumbe wa Halmashauri ya Kijiji.
·        Kujadili na kupitisha bajeti na mipango ya maendeleo ya Kijiji.
·        Kuidhinisha utungwaji wa sheria ndogo kabla ya kupelekwa kwenye                  Halmashauri ya wilaya kwa ajili ya kupitishwa kwa manufaa ya kijiji.
·        Kufanya maamuzi yanayozingatia demokrasia.
·        Kujadili na kupitisha bajeti na mipango ya maendeleo ya Kijiji.
·        Kupitisha azimio la kukaripia rasmi mjumbe yoyote wa halmashauri au halmashauri kwa ujumla kwa utendaji mbovu

Kazi za Mwenyekiti wa Kitongoji
·        Kutunza rejesta ya wakazi wa kitongoji na nyaraka nyingine muhimu zinazohusu maendeleo ya kitongoji kwa jumla ikiwa ni pamoja na kumbukumbu za vizazi na vifo.
·        Kusimamia shughuli za ulinzi na usalama wa watu na mali zao waishio katika eneo lote la kitongoji.
·        Kuhamasisha ulipaji wa kodi na ushuru mbalimbali, kama utakavyoamuliwa na kuwekwa mara kwa mara na Halmashauri ya Kijiji na Wilaya. Jukumu hilo pia linatekelezwa na Mwenyekiti wa kitongoji kilicho kwenye eneo la Mji, Manispaa au Jiji.
·        Kusimamia katika eneo lake suala zima la Hifadhi ya mazingira hususan vyanzo vya maji n.k.
·        Kusimamia suala la afya katika eneo lake ikiwa ni pamoja na utekelezaji wa kampeni za afya za Kitaifa, Kimkoa au Kiwilaya dhidi ya magonjwa ya kuambukiza, na hasa, vita dhidi ya UKIMWI.
·        Kufuatilia hali ya lishe na uchumi wa wakazi wa kitongoji.
·        Kufuatilia na kuhakikisha kuwa kila mtoto mwenye umri wa kwenda shule anapatiwa nafasi na kushirikiana na viongozi wa shule katika udhbiti utoro shuleni.
·        Kuhamasisha elimu ya watu wazima.
·        Kusimamia na kuwahamasisha wakazi wa kitongoji katika kutekeleza shughuli za kujitegemea.
·        Kusuluhisha migogoro midogo midogo isiyostahili kushughulikiwa na Mabaraza ya Kata au Mahakama.
·        Kuwakilisha kitongoji katika Serikali ya Kijiji.
·        Kuwaongoza na kuwahamasisha wakazi wa kitongoji washiriki katika sherehe za Taifa na mikutano ya hadhara itakayoandaliwa na kuitwa na Serikali au Halmashauri.
·        Kutekeleza kazi nyingine atakazopangiwa na Halmashauri ya Kijiji na Wilaya. Jukumu hili pia linatekelezwa kwa vitongoji vilivyo kwenye Halmashauri za Miji, Manispaa au Jiji
·        Kufanya maamuzi yanayozingatia demokrasia.
·        Kuchagua Mwenyekiti na Wajumbe wa Halmashauri ya Kijiji.
·        Kujadili na kupitisha bajeti na mipango ya maendeleo ya Kijiji.
·        Kuidhinisha utungwaji wa sheria ndogo kabla ya kupelekwa kwenye Halmashauri ya wilaya kwa ajili ya kupitishwa kwa manufaa ya kijiji.


Mamlaka na Majukumu ya Halmashauri ya Kijiji
  • Kutafakari maamuzi, mapendekezo na maazimio ya mkutano Mkuu wa kijiji na kubuni mbinu na njia za kutekeleza.
  • Wajumbe wa halmshauri wenyewe wakiwa hawaridhiki kabisa na utendaji wa Mwenyekiti wa kijiji wana haki ya kumwondoa kwa kura theluthi mbili ya wajumbe wote na kuitisha Mkutano Mkuu wa kijiji ili kuchagua mwenyekiti mwingine.
  • Kupokea taarifa za mikutano ya vitongoji na kamati zake kufanyia kazi na kupeleka Mkutano Mkuu wa kijiji.
  • Kupokea, kutafakari na kufanyia kazi maagizo na mapendekezo kutoka kamati ya maendeleo ya kata (WDC) na halmshari ya wilaya.
  • Kubuni na kuendekeza sera na mwelekeo wa kijiji kwa mkutano mkuu wa kijiji.
  • Kuandaa na kupendekeza mipango ya maendeleo ya muda mrefu kwa Mkutano Mkuu wa kijiji.
  • Kutunga sheria ndogondogo kwa kushauriana na Mkutano Mkuu wa kijiji.
  • Kuwaalika wataalamu panapokuwa na haja ya kufanya hivyo ila hawatakuwa na haki ya kupiga kura.
  • Kupokea, kutafakari na kupendekeza kwa Mkutano Mkuu wa kijiji maombi ya ugawaji wa ardhi zaidi ya ekari 100 hadi 500 rasilimali zingine kwa maamuzi.
  • Kupokea, kutafakari na kuamua ugawaji wa ardhi chini ya ekari 100.
  • Kutoa taarifa za utendaji kwa Mkutano Mkuu wa Kijiji.
  • Kumiliki mali na kuingia mikataba kwa niaba ya kijiji.

Ushiriki wa wananchi ni jambo la msingi sana katika kujiletea maendeleo yao katika vijiji na mitaa. Mahali ambapo wananchi hawashiri wala hawashirikishwi kunakuwa na lawamana mizozo mingi kwa viongozi hasa pale ambapo maamuzi yaliyopitishwa yanawaumiza wananchi. Hapa ndipo wengi huona umuhimu wa kushiriki unapojitokeza zaidi.

http://sw.wikipedia.org/wiki/Utawala_wa_Kijiji_-_Tanzania


No comments:

Post a Comment

Previous Page Next Page Home