Tuesday, March 22, 2016

MABADILIKO YA WAJUMBE KWENYE KAMATI ZA BUNGE


TAARIFA KWA UMMA

Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai (Mb) amefanya mabadiliko ya baadhi ya Wajumbe wa Kamati za Kudumu za Bunge ili kuzingatia mahitaji mapya na changamoto zilizojitokeza baada ya kuunda Kamati hizo mwezi Januari 2016. Mabadiliko hayo, yamefanywa chini ya Kanuni ya 116(3) ya Kanuni za Kudumu za Bunge inayompa Mamlaka ya kuteua Wabunge kuunda Kamati Mbalimbali za Bunge.
Aidha kufuatia mabadiliko hayo ambayo baadhi yake yamehusu Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti au wote wawili, Kamati za Kudumu za Bunge zilizoathirika na mabadiliko haya zitawajibika kufanya Uchaguzi wa viongozi kwa mujibu wa kanuni ya 116 (10) kama ifuatavyo:

 1. Kamati ya Ardhi, Maliasili na Utalii itahitaji kupata Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wapya.
 2. Kamati ya Nishati na Madini itahitaji kupata Mwenyekiti mpya.
 3. Kamati ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma itahitaji kupata Mwenyekiti mpya.
 4. Kamati ya LAAC itahitaji kupata Makamu Mwenyekiti mpya.
 5. Kamati ya Huduma na Maendeleo ya Jamii itahitaji kupata Makamu Mwenyekiti mpya.
 Mabadiliko haya kwenye kamati zote yanaanza mara moja ambapo orodha ya wajumbe waliobadilishwa imeambatishwa.

Imetolewa na:
Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano
Ofisi ya Bunge DAR ES SALAAM

22 Machi, 2016.

Taarifa kamili pamoja na list ya waheshimiwa wabunge kwenye kamati za kudumu za bunge  soma HAPA

Sunday, March 13, 2016

UNA MCHANGO GANI KWENYE SHULE ULIYOPATA KUSOMA NA KUKUFIKISHA HAPO ULIPO LEO?


BY NGUDU NYUMBANI BLOG
13/03/2016

NYASECO ALUMINAE, hili ni kundi la wadau waliopata kusoma shule ya sekondari  Nyamilama iliyopo talafa ya Nyamilama, kata ya Nyamilama wilaya ya KWIMBA.

Wadau hawa licha ya uchache wao lakini walipata kujipanga na kwenda kuitembelea shule waliyopata kusoma miaka kadhaa iliyopita. Lengo ni kujua maendeleo ya shule yao hiyo, changamoto zinazoikabili shule hiyo na mambo yote yanayoihusu shule kwa ujumla.

Sijabahatika kupata taarifa zao zaidi, japo kwa “Video clip” ya dakika chache inatosha kuonesha  malengo na Mipango waliyokuwa nayo kutaka  kuitembelea shule yao. Shauku yao kubwa ilikuwa ni kuona mabadiliko ya shule hiyo kipindi wanasoma na hali ilivyo kwa kipindi wameitembelea. 
Previous Page Next Page Home