Tuesday, December 23, 2014

MATOKEO YA DARASA LA SABA WILAYA YA KWIMBA

Matokeo ya darasa la saba yalitangazwa hivi majuzi na kutolewa tathmini ya ufaulu wa wanafunzi waliofanya mtihani huo, ikionesha ufaulu umeongezeka ni katika utekelezaji wa sera ya MATOKEO MAKUBWA SASA(BIG RESULT NOW).

Nimejaribu kupitia tovuti ya baraza la mitihani ili kupata matokeo kamili ya wilaya ya kwimba, kwa kuangalia shule zilizoongoza na zilizoshika mkia katika wilaya kwa ujumla ambapo jumla ya shule ni 151 kama ifuatavyo.

SHULE KUMI ZILIZOONGOZA KWENYE UFAULU:

  1. KIMIZA
  2. MWABARATULU
  3. KADASHI
  4. ICHEJA
  5. BUDUSHI
  6. MWAGI
  7. NYAMBITI
  8. GULUNG'WA
  9. MALYA
  10. NYAMILAMA
SHULE TANO ZILIZOBURUZA MKIA

147.NG'HULIKU
148. MWANG'HALANGA
149.KILIGU
150.SANGA

BAADHI YA WASHINDI WA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MTAA NA MAENEO YAO


















Katika uchaguzi wa serikali za mtaa zilizofanyika nchini kote tar 14 dec 2014, wilaya yetu ya kwimba baadhi ya maeneo yaliyokuwa yakishikiliwa na CCM yamekuwa ngome mpya ya wapinzani(CHADEMA). Kwenye picha hapo juu ni mwenyekiti mpya wa NGUDU MJINI ndugu casmiry. Baadhi ya maeneo ni kama ifuatavyo

HOTUBA YA MHESHIMIWA RAIS NA WAZEE WA DAR ES SALAAM


Kikwete:   Naendelea kuimarika kila siku japo sipo fit kabisa. Leo nazungumzia uchaguzi wa serikali za mitaa, umeenda vizuri ukiacha maeneo machache. Ni uthibibitisho wa kuendelea na kukomaa kwa demokrasia na natoa pongezi kwa walioshinda na wakae chini kupanga mikakati ya kuongoza maeneo yao. Katika taarifa ya waziri Ghasia alielezea kasoro zilizojitokeza na aliahidi kuchukua hatua. Nieleze furaha yangu kwa Hawa Ghasia juu ya hatua alizochukua na mimi nikaweka ridhaa yangu, lazima watumishi wajue kuna adhabu ya makosa wanayoyafanya, kuwawajibisha itakua fundisho kwao na kwa wengine wawe makini kwenye uchaguzi wa 2015.

WATU WANAOJULIKANA NGUDU KWA NAMNA MOJA AMA NYINGINE




Tuesday, December 9, 2014

ZIFAHAMU KATA ZA WILAYA YA KWIMBA

Wilaya ya Kwimba ni moja kati ya wilaya saba zinazounda mkoa wa Mwanza.Upande wa magharibi imepakana na wilaya ya Misungwi, wilaya ya Magu kwa upande wa kusini.Kwenye sensa iliyofanyika mwaka 2002 ilikuwa na wakazi wapatao 316,180(takwimu za 2012 sikubahatika kuzipata). Makao makuu ya wilaya yapo Ngudu

Wilaya ya kwimba ina jumla ya kata 25, na vijiji 111, kama ifuatavyo;

Mbunge wa viti maalumu(kwimba), Leticia Nyerere, alipokuwa akiongelea swala la uraia pacha


Mbunge wa viti maalum Mh. Leticia Nyerere amewatoa mashaka waTanzania wote waliokua njee ya nchi juu ya swala zima la kuwa raia wa nchi mbili
Amesema kinachoendelea hivi sasa juu ya maoni ya kuanzishwa kwa katiba mpya tume itatumia busara zake ili kuingiza kipengele cha uraia wa nchi mbili katika katiba hiyo mpya kwani itawezesha raia wa Tanzania walioko nje ili kusaidia kujenga taifa la Tanzania katika kuwekeza mitaji yao na miradi mbali mbali ya kukuza uchumi.

Mhe. Leticia Nyerere ameyasema hayo wakati alipoongea na baadhi ya waTanzania waishio DMV Nchini Marekani.  

unaweza kumsikiliza hapa
https://soundcloud.com/mswahiliflani/maoni-ya-raia-wa-nchi-mbili-na

Mwandishi: Nguduone.

Sunday, December 7, 2014

JUKWAA LA KWIDEKO LAEZULIWA NA UPEPO

Baada ya paa la jukwaa kupeeruswa na upepo wa mvua hapo jana...1958 hadi 2014


Mwandishi : Michael Nkiya Mageni.




MAWAZO HURU JUU YA MAENDELEO YETU

MAWAZO YANGU.
Wilaya yetu ni moja kati ya wilaya kongwe mkoa wa MWANZA, japo nadhani ndio inaongoza kwa umaskini.Nilifikili nikadhani kuna baadhi ya mambo yanayotufanya tubaki hapa tulipo, machache kati ya mengi

1. Aina ya uongozi mbovu wa serikali uliopo katika wilaya yetu kwa ujumla, kuanzia ngazi ya kijiji hadi ile ya juu kabisa kwenye halmashauri ya wilaya.
hatutaki mabadiliko ya uongozi

MAWAZO YA WAZAWA JUU YA MAENDELEO YA WILAYA YETU


NILIKUWA NAPITA PITA NIKAKUTANA NA HII MTANDAONI,
NAVYOAMINI MWENGE WA UHURU WETU HUU HAUNA FAIDA KIVILE ZAIDI YA KUPOTEZA FEDHA ZA WANANCHI, KITU AMBACHO KINGEWEZA KUZINDULIWA NA WAWAKILISHI WA RAISI NGAZI YA WILAYA, AMBAPO HZO GHARAMA ZA HUO MSAFARA WANGEWEKEZA KWENYE MAENDELEO YA WILAYA YETU

MASWALI YA MBUNGE WETU MANSOOR SHANIF HIRAN BUNGENI.

HAYA NDO MASWALI ALIYOULIZA BUNGENI MBUNGE WANGU Shanif Mansoor Hiran TANGU NIMCHAGUE KUNIWAKILISHA., Je nimpe kura mwaka 2015? Anafaa kuniongoza?


 1. REGIONAL ADMINISTRATION AND LOCAL GOVERNMENT 4 July 2011 Mji mdogo wa Ngudu ambao ndio Makao Makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba, una wakazi wengi na taasisi mbalimbali zinazotoa huduma za kijamii na kiuchumi lakini una matatizo makubwa ya maji ambayo hutokana na uchakavu wa pampu mbili za kuvuna maji na pump moja ya kusukuma na kusambaza maji kutoka kwenye vyanzo vya maji vilivyo eneo la Kilyaboya. Gharama za pump hizo kwa pamoja hazizidi shilingi milioni hamsini za Kitanzania. Je, Serikali inajipanga vipi kuhakikisha tatizo hili la maji linamalizika kwa wakati ili kuondoa kero hiyo iliyopo kwa muda mrefu sasa?

MWANA MITINDO MZAWA WA KWIMBA























Wanangudu jamani naomba tumuunge mkono dada yetu mpendwa Lucy Charles anaeiwakilisha ngudu kwimba vizuri katika tasnia ya mitindo.........MAFANIKIO 
YAKE NI MAFANIKIO YETU PIA.

Previous Page Next Page Home