Friday, February 12, 2016

WILAYA MBILI AU HALMASHAURI MBILI NDANI YA WILAYA MOJA?


BY NGUDU NYUMBANI BLOG
12/02/2016

WILAYA ya KWIMBA ni moja kati ya wilaya 7 zinazounda mkoa wa MWANZA. Katika sensa ya mwaka 2012, idadi ya wakazi wa wilaya ya KWIMBA ilihesabiwa kuwa 406,509. Pia makadirio ya idadi ya watu kwa mwaka 2015 takwimu zinaonesha majimbo mawili yanayopatikana wilaya ya KWIMBA  yana jumla ya wakazi 438,984 ambapo jimbo la Kwimba ni 235,818 na Sumve ni 203,166.

Nimejaribu kuandaa majedwali yanayohusisha sensa ya mwaka 2012, pia makadirio ya idadi ya watu mwaka 2015 kwa majimbo ya KWIMBA na SUMVE kama ifuatavyo;



WILAYA
JIMBO
KATA
SENSA YA MWAKA  2012
MAKADIRIO YA IDADI YA WATU 2015
KWIMBA
KWIMBA
MWANG’HALANGA
11, 099
11,986


NYAMILAMA
7, 611
8,219


MWAKLYAMBITI
16, 079
17,364


HUNGUMALWA
16, 508
17, 827


MWAMALA
10, 582
11,427


KIKUBIJI
 22, 032
23,792


MHANDE
19, 629
21, 197


BUPAMWA
17,366
18,753


FUKALO
17,534
18,935


NG’HUNDI
9,255
9,994


IGONGWA
11,705
12, 640


NGUDU
27,630
29,837


MWANKULWE
9,495
10,254


ILULA
11,966
12, 922


SHILEMBO
9,882
10, 671




WILAYA
JIMBO
KATA
SENSA YA MWAKA  2012
MAKADIRIO YA IDADI YA WATU 2015
KWIMBA
SUMVE
WALLA
17,190
18,563


BUNGULWA
10,361
11,189


SUMVE
16,436
17,749


NGULLA
12,692
13,706


MWABOMBA
10,096
10,903


MWAGI
11,325
12,230


ISENI
10,349
11,176


NYAMBITI
13,731
14,828


MALIGISU
20,788
22,449


MWANDU
11,132
12,021


MALYA
15,437
16,570


LYOMA
12, 561
13,564


BUGANDO
7,173
7,746


NKALALO
7,266
7, 846


MANTARE
11, 599
12, 526



wilaya ya KWIMBA ina Ukubwa wa eneo la nchi kavu 3903km ambapo Asilimia za eneo kwenye mkoa ni 15.5
Wilaya ya Kwimba inaundwa na tarafa tano ambazo ni Ngudu, Nyamilama, Mwamashimba, Ibindo na Ngulla. Tarafa 2 zikiwa jimbo la Sumve na 3 jimbo la KWIMBA.

Wilaya pia ina kata 30, vijiji 119 na vitongoji 870. Hii ni kulingana na takwimu za TAMISEMI  mwaka 2015.

UZALISHAJI NA MAPATO

Makusanyo ya mamlaka za serikali za mitaa kwa wilaya ya Kwimba kuanzia mwaka 2005 mpaka june 2015 kuna ongezeko la asilimia 128, ambapo kupitia ongezeko hilo la ukusanyaji wa mapato ndipo kunakuwa na ongezeko la wigo wa utoaji huduma kwa wananchi.

Katika hili wataalamu wa uchumi wanaweza kutusaidia kueleza kama mapato haya yanatumika ipasavyo kuongeza utoaji bora wa huduma kwenye wilaya yetu.

Kweny upande wa kilimo, uzalishaji wa zao la pamba umeshuka kutokana na ukame  na kusababisha mapato yatokanayo na ushuru wa pamba kupungua. Ukiacha suala la ukame pia soko zuri kwa wakulima wa pamba bado ni tatizo na changamoto kubwa kwa wakulima wa zao hilo. Pia uzingatiaji wa kilimo bora na cha kisasa kinachohusisha utumiaji wa mbolea na madawa ya kuzuia wadudu waharibifu wa mimea bado ni tatizo. Mbolea za ruzuku bado hazifanyiwi mzunguko unaostahili mpaka kumfikia mkulima.

katika kuimarisha huduma za ugani shirikishi(ushauri kwa wakulima), Mkoa wa MWANZA umetumia mbinu shirikishi katika kuibua miradi ya ASDP na kuanzisha mashamba darasa.
Katika sekta ya uzalishaji mali, wilaya ya KWIMBA ndiyo yenye idadi kubwa ya mashamba darasa(113) ukilinganisha na wilaya nyingine mkoa wa MWANZA.  ASDP huu ni mpango wa maendeleo ya sekta ya kilimo.

Idadi ya zana za kilimo wilaya ya KWIMBA kufikia 2015, matrekta makubwa ni 57, matrekta madogo(power tillers) yapo 45, majembe ya kukokotwa na ng'ombe(plau) jumla yapo 9,933. 

Katika uhamasishaji wa ujenzi wa maghala bora ya kuhifadhia mazao, wilaya ya KWIMBA ina maghala manne ya kuhifadhia chakula hasa baada ya mavuno. Japo tatizo la njaa hasa wilaya hii bado ni changamoto kubwa ambayo inapaswa mikakati katika kupata utatuzi na ufumbuzi wa kudumu.
Itakumbukwa gazeti la Habari Leo liliwahi kuandika habari juu ya mbunge wa jimbo la Sumve  kuomba msaada serikalini kuletewa chakula cha msaada jimboni. Mbunge aliyasema hayo kwa kile alichoikiita kukauka kwa mazao kutokana na ukosefu wa mvua. Hii ilikuwa mwaka jana 2015

TAASISI ZA ELIMU.

Wilaya ya KWIMBA ina shule za awali 148(zote serikali), na shule za awali 151. ikiwa ni wilaya pekee kwa mkoa isiyokuwa na shule za binafsi upande wa awali na msingi mpaka kufikia mwaka 2015.

W ilaya pia ina  Shule za sekondari 31, ikiwa ni wilaya ya pili yenye idadi kubwa ya shule za sekondari baada ya wilaya ya Sengerema yenye shule 48. Japo inahitajika ongezeko la shule za kidato cha tano na sita, ambapo mpaka sasa katika kata zote 30 za wilaya kuna shule 3 tu.
Wilaya ya KWIMBA ina vyuo vitatu vinavyotoa elimu na mafunzo kwa ngazi ya astashahada na stashahada.

1. MALYA COLLEGE OF SPORTS DEVELOPMENT. Ni moja ya vyuo vikubwa vya michezo kipo kata ya Malya. Inasemekana ndicho chuo pekee cha kuzalisha wataalamu na walimu wa michezo Tanzania.
Makala inayochambua mafanikio na mwenendo wa chuo hiki unaweza kuisoma HAPA

2. NGUDU SCHOOL OF ENVIRONMENTAL HEALTH SCIENCES. Kilichopo tarafa ya NGUDU na kata ya NGUDU jirani kabisa na hospital ya wilaya.

3. SUMVE SCHOOL OF NURSING-KWIMBA. Hiki kinapatikana ilipo hospital ya rufaa ya SUMVE  kata ya Sumve

UWEZESHAJI.

Katika kuhamasisha uimarishaji wa mifuko ya wanawake iliyopo katika halmashauri, ili wanawake wengi zaidi waweze kupata mikopo na kunufaika. Wilaya ya Kwimba ina jumla ya vikundi 13 hadi kufikia 2015.

Naweza kusema kuwa idadi hii ni ndogo sana ukilinganisha na uhitaji wa huduma hii. ambapo tunatarajia vikundi vingi zaidi vikiandikishwa na kuwezeshwa ili kumkwamua mwanamke ambapo viongozi wenye dhamana wana wajibika katika hili.

WILAYA MBILI AU HALMASHAURI MBILI?

Baada ya kuona takwimu na maelezo mengine baadhi yanayohusu wilaya ya KWIMBA, turudi kwenye mada kuu inayolenga kujua kama kutatakiwa mgawanyo kwenye wilaya ulenge haswa wapi.
Mwaka jana(2015) mwezi June Mbunge wa Jimbo la Sumve alipata kunukuliwa akimwomba katibu mkuu wa chama tawala ndugu Abdulrahman Kinana kupitia moja ya mikutano ya siasa jimboni kwake kwamba wilaya igawanywe ziwe wilaya mbili(KWIMBA na SUMVE).

“Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara mjini Sumve, mbunge huyo alisema wilaya hiyo ina watu wapatao 400,000 ambao ni wengi kiasi cha kuhitaji kugawanywa.”. Hata hivyo, Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana alishauri waanzie kuomba halmashauri badala ya mgawanyo wa wilaya.

 Alisema halmashauri ndiyo inapata fedha za maendeleo kwa maana kwamba, wakiwa na halmashauri mbili, kila moja itapata fedha zake.

Nadhani pia angeshauriana na mbunge mwenzie wa jimbo la Kwimba kisha wakawa na msimamo wa pamoja. Baadae wangeandaa hoja binafsi kwenye bunge(endapo kama hoja hiyo ni mahsusi kwa bunge) juu ya agenda hiyo wakiwa tayari wamefanya upembuzi yakinifu juu ya watakachoenda kukiwasilisha.

Kila mmoja anaweza kuwaza kwa namna yake ya kipekee kwamba kilingana na vigezo vya uanzishaji wa mamlaka mpya ya serikali za mtaa, wilaya yetu inakidhi vigezo vipi kati ya kugawanywa na kuwa wilaya mbili au kuwa na halmashauri mbili ambazo zote zitakuwa chini ya wilaya moja?

Katika msingi wa majadiliano yetu, tunaweza kushauri kulingana na taratibu na kanuni zinazoongoza ugawanywaji au uundwaji wa mamlaka mpya chini ya serikali za mitaa. Pia umuhimu wa kugawanya mamlaka ni upi na pengina kama kutakuwa na athari pia ni vyema zikabainishwa.

VIGEZO NA TARATIBU ZA KUANZISHA/KUPANDISHA HADHI MAMLAKA ZA
SERIKALI ZA MITAA
Mamlaka za Serikali za Mitaa huanzishwa kwa kuzingatia Ibara 145 na 146 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Ibara hizi zinaelekeza kuanzishwa kwa vyombo vya Serikali za Mitaa katika eneo la Mikoa, Wilaya, Mji na Kijiji. Ili kutekeleza matakwa haya,
Sheria za Serikali za Mitaa zimeweka masharti, misingi na taratibu za kufuatwa katika kuanzisha  Mamlaka za Serikali za Mitaa.
Utaratibu wa kuanzisha Mamlaka za Serikali za Mitaa ni mapendekezo au maombi ya kuanzisha Mamlaka hizo kupata ridhaa ya wananchi kupitia vikao vilivyowekwa Kisheria katika ngazi husika.
Katika makala hii inayohusisha wilaya na halmashauri, ngazi ya halmashauri ni kupitia Baraza la madiwani. Na upande wa wilaya suala hili linakuwa chini ya “KAMATI YA USHAURI YA WILAYA-DDC”

VIGEZO VYA KUANZISHA HALMASHAURI ZA WILAYA:
 i. Kuwepo na idadi ya Kaya zinazotakiwa kwa eneo kuwa Halmashauri ya Wilaya;
ii. Kuwepo kwa idadi ya watu wanaotakiwa kwa eneo kuweza kutambuliwa kuwa Halmashauri ya Wilaya;
iii. Kuwa na eneo la ardhi ya kutosha kuendeleza shughuli za kiuchumi, kijamii na kimaendeleo katika Halmashauri ya Wilaya kiwango;
 iv. Kuwepo na mapato yanayotarajiwa kukusanywa kama kodi au tozo nyingine zenye kutosheleza utoaji wa huduma muhimu pamoja na uendeshaji wa shughuli za Serikali katika eneo zima la Halmashauri ya Wilaya;
v. Kuwepo kwa huduma za kijamii na kiuchumi, kama vile shule, vituo vya afya, zahanati, maji, barabara kwa kuzingatia viwango vilivyowekwa kitaifa kwa kila sekta husika.

Vigezo vya kuanzisha Halmashauri ya Mji (Town Council)
 i. Kuwe na watu wasiopunga 30,000.
ii. Mji uwe na uwezo wa kujiendesha angalau kwa asilimia 50% ya bajeti yake.
iii. Mji uwe na kiwango cha juu cha utoaji huduma ya hospitali, kuwe na shule ya Sekondari, kuwe na angalau maduka ya rejareja yenye leseni yasiyopungua 50, Kituo cha Polisi na pawe na Makao makuu ya Tarafa..
Kwa hayo machache unaweza ukawa ni mwanzo mzuri wa wasomaji wa makala hii kujenga hoja juu ya kipi ni bora na halali kwa mazingira ya sasa ya wilaya yetu.

Ni nafasi nzuri pia kwa wataalamu wa masuala ya sheria kuweza kutuchambulia kanuni na taratibu zinasemaje juu ya uanzishwaji wa mamlaka mpya ya serikali za mitaa, Lengo ni kuona wilaya inasonga mbele kimaendeleo kutoka hatua hii tuliyopo.

 Pia kwa wataalamu wa kada nyinginezo zote kuweza kuchangia katika hili, ili mwisho wa siku tuwe na mawazo ya wengi yanayoweza kukubalika na umma wa wana KWIMBA wote.

Nitoe  RAI yangu kwa wasomaji wote wa makala haya kwamba, wapitie vizuri kisha wachangie kulingana na kilichoongelewa. Ni imani yangu kwamba wilaya hii kongwe ina wasomi wengi katika ngazi mbalimbali hivyo kwa watakaopata wasaa wa kupitia hapa wanaweza kusaidia sana kuchangia kwa weledi na ustadi mkubwa.
Je inatakiwa wilaya mbili au inatakiwa tuwe na halmashauri mbili ndani ya wilaya yetu?



Tafakari.

NGUDU NYUMBANI BLOG
nguduone@gmail.com



No comments:

Post a Comment

Previous Page Next Page Home