Wednesday, February 10, 2016

SHIKOME, KWIWODE, NADSO NA NGO’s NYINGINEZO KWIMBA RIPOTI ZA MAENDELEO YAO ZIPO VIPI?


BY NGUDU NYUMBANI BLOG

Japo kwa ufupi tupate kujua maelezo machache juu ya taasisi hizi zisizo za kiserikali kwa faida ya wasiojua, kisha kama kuna wahusika au wadau wa maendeleo wanaojua kinachoendelea ndani ya taasisi hizi waujuze umma wa wana Kwimba maendeleo yake yako vipi japo kwa muhtasari kufikia mwezi huu.

 Nikimaanisha miradi ya maendeleo kupitia taasisi hizo, mwitiko wa watu kushirikiana na taasisi na mchango wa serikali pamoja na wafadhili kutoka ndani na nje umewezesha kwa kiasi gani kuikuza taasisi husika na hatimaye kufikia malengo yake. Na kama kuna utaratibu maalumu wa kupata taarifa husika hizo pia ni vema ikajulikana wenye nia ya kujua wakafuata..



1. SHIKOME ORGANISATION GROUP

Ni taasisi isiyo ya kiserikali inayojihusisha  na masuala ya maendeleo kwenye jamii na demokrasia, ambapo imejikita hasa kusaidia makundi ya watu kwenye jamii kama watoto, vijana, wanawake na masuala ya kijinsia kwenye jamii.

Imeanzishwa mwaka 2007 na wamepata kuanzisha na kusimamia baadhi ya miradi ikiwemo SHIKOME  ORGANISATION TAILORING CENTER hapo Ngudu chini ya ufadhili wa shirika moja la nje Vraag en Aanbod International.

Katika moja ya report zao wameweza kuelezea baadhi ya mambo ya uanzishwaji wa mradi, malengo, wanufaika, kazi zitakazofanyika kwenye mradi huo na mengineyo. Coordinator wa mradi huo alikuwa ndugu MADELEKE SULEIMAN

Pia kuna katiba ya taasisi hii ambayo imejaribu kuelezea utaratibu mzima juu ya uendeshaji wa taasisi, masuala ya uanachama na mengine yote yahusuyo umoja huo. Pia kuna cheti cha usajiri kinachothibitisha kuwa taasisi hiyo imesajiliwa kihalali kwa mujibu wa sheria.

Kwa sasa hakuna report zao zinazoonesha mwendelezo wa miradi wanayoisimamia na hatua walizofikia kwenye miradi hiyo. Kwa msaada ya anayejua ama mhusika ama mdau wa maendeleo anayejua juu ya taasisi hii ni vyema na busara akaujuza umma hatua waliyopo kwa sasa…….

2. KWIMBA WOMEN DEVELOPMENT (KWIWODE)


Taasisi hii imeanzishwa mnamo mwaka 2004 na kikundi cha wanawake wajasiliamali wa Kwimba kusaidia kutetea haki za mwanamke na kuleta usawa wa kijinsia kwa maana ya fursa sawa kwa jinsia zote.

Kazi kubwa ya kikundi hiki ni kulinda haki za mwanamke, kumpa mafunzo mbalimbali ya ujasiliamali ya kumwezesha kujikwamua na hali ngumu ya maisha na mambo mengine yanayoihusu jamii.

Moja ya miradi yao ni ule wa mwaka 2010 uliojulikana kama REHABILITATION AND SANITATION FACILITIES FOR NYAMILAMA PRIMARY SCHOOL PROJECT  chini ya support nzuri kutoka kwa Tanzania development trust na coordinator wa mradi alikuwa ni  Edina Ihonde


3. NEEDFUL ACTION FOR DEVELOPMENT SEARCH ORGANISATION(NADSO)
Ni taasisi inayohusisha umoja wa wanafunzi waliosoma Ngudu sekondari au na kuishi wilaya ya Kwimba kwa ujumla. Lengo kubwa la taasisi hii ni kusaidia jamii za watanzania kwenye Nyanja za maendeleo hususani wilaya yetu ya Kwimba hasa katika elimu, ujasiliamali,na shughuli za maendeleo kwa ujumla. Ambapo itafanya kazi na wadau wote wa maendeleo nchi nzima lakini kwa kuelekeza zaidi wilaya ya Kwimba.

Katika  moja ya mafanikio ya taasisi ni pamoja na kutembea shule ya sekondari Ngudu Msafara uliofanikisha Ununuzi wa vitabu na pia kuwapo kwa documentary juu ya kilichojiri kwenye safari hiyo kwa ujumla safari hii ilifanyika mwezi wa 5 mwaka huu.

Kwa anayetaka kujiunga na taasisi hii kuna utaratibu ulitolewa hapo kabla ambapo kuna katiba ya taasisi ambayo imeongelea mambo yote kwa undani kabla ya kutaka kuwa mwanachama.

MWISHO.
Lengo la kuelezea yote haya ni kutambua uwepo wa taasisi, kuonesha kujali na kuzitakia taasisi hizi mafanikio ambapo ni maendeleo ya wilaya yetu pia.
 Pengine zikawepo nyingine tofauti na hizi nilizozitaja ambapo lengo lao pia ni kusaidia maendeleo ya wilaya yetu pia. Ushauri kwa vijana na wadau wote wa Kwimba kujiunga katika vikundi mbalimbali vya kimaendeleo mkianza kujisimamia wenyewe kwa mtaji mdogo mlionao, ambapo mkionesha nia ya dhati juu ya mnachokifanya bila shaka support itapatikana tu.

KWIMBA TUITAKAYO.
nguduone@gmail.com .



No comments:

Post a Comment

Previous Page Next Page Home