Sunday, May 24, 2015

Ajira Mpya Kwa Walimu 2015........Haya Ni Majina Ya Awamu Ya Pili Pamoja Na Mabadiliko Ya Vituo Vya Kazi


Tarehe 27  na 30  Aprili, 2015,  Ofisi ya Waziri Mkuu  -  TAMISEMI ilitangaza ajira ya wahitimu wa mafunzo ya ualimu na mafundi sanifu  wa maabara  kwa  kuweka  orodha kwenye tovuti ya    www.pmoralg.go.tz.  Iliagizwa kuwa  waajiriwa    wapya walipaswa kuripoti katika Mamlaka za Serikali za Mitaa kuanzia tarehe 01 hadi 09 Mei, 2015.

Napenda  kuchukua nafasi hii kuutaarifu umma  kuwa ofisi yangu  ilipokea  na kuchambua  maombi ya  walimu ambao hawakuajiriwa awali;  na walioomba kubadilishiwa vituo kutokana na    matatizo mbalimbali.

 Vilevile ofisi  imezingatia kuwapanga tena  walimu ambao kwa sababu  za msingi  walishindwa kuripoti kufikia tarehe 09 Mei, 2015.  

Walimu wote waliopo katika orodha ya awamu ya pili wanapaswa kuripoti kuanzia tarehe  01 hadi 05 Juni, 2015  kwenye ofisi za Wakurugenzi wa Halmashauri kwa ajili ya kuajiriwa na kupangiwa vituo vya kazi.

Orodha ya walimu  hao watakaoajiriwa katika halmashauri husika  imegawanywa katika makundi yafuatayo:-

i.  walimu wa cheti (Daraja IIIA) waliokosa ajira kwa awamu ya kwanza;

ii.  walimu wa cheti (Daraja IIIA) waliobadilishiwa vituo;
iii.  walimu  wa  masomo ya sanaa  kwa ajili ya shule za sekondari  ambao hawakupangiwa vituo; 

iv.  walimu waliobadilishiwa vituo wa masomo ya sanaa  kwa ajili ya shule za sekondari; 

v.  walimu wa masomo ya sayansi na hisabati kwa ajili ya shule za sekondari ambao hawakupangiwa vituo; na

vi.  walimu  waliobadilishiwa vituo wa masomo ya sayansi na hisabati kwa ajili ya
shule za sekondari.

Utaratibu wa Ajira ya Walimu Awamu ya Pili
Kila mwajiriwa mpya anatakiwa kuzingatia yafuatayo:-i.  kuwasilisha vyeti halisi vya taaluma ya kuhitimu mafunzo  ya ualimu, elimu ya sekondari, cheti cha kuzaliwa pamoja na nakala zake; na

ii.  atalipwa  posho ya kujikimu kwa muda wa siku saba (7) na nauli ya usafiri wa magari (ground travel), malipo hayo yatatolewa na halmashauri husika.

Angalizo
i.  Walimu ambao wamekwisharipoti na mchakato wao wa ajira umeanza katika  Mamlaka za Serikali za Mitaa hawatahusika na mabadiliko  haya  hivyo waendelee kufanya kazi katika halmashauri husika na hawahusiki na upangaji wa awamu hii.

ii.  Walimu ambao walichelewa kuripoti tarehe 9 Mei, 2015 na majina yao hayajaonekana katika mabadiliko haya wanatakiwa waende kuajiriwa katika halmashauri walizopangwa awali (kwa kuzingatia orodha iliyotolewa kwenye tovuti tarehe 30/4/2015).  Aidha, walimu wa masomo ya sanaa ambao hawakuripoti katika Halmashauri za Wilaya za Meru na Arusha wamebadilishwa vituo.

iii.  Walimu waliopangwa ni wale wa masomo  ya sanaa/biashara na cheti waliohitimu mafunzo kwa mwaka wa masomo 2013/14 na wahitimu  wa miaka ya nyuma wa masomo ya sayansi na hisabati kwa ajili ya kufundisha katika shule za sekondari.

iv.  Kituo cha kazi cha mwalimu ni shule na sio Makao Makuu ya Halmashauri, posho italipwa baada ya mwalimu kuripoti na kuandika  barua kupitia kwa
Mkuu wa Shule.

v.  Mwalimu hatapokelewa na kuaajiriwa kama ikitokea yupo katika orodha na amehitimu shahada au stashahada zisizo za ualimu na wenye shahada za ualimu zisizo na somo au masomo ya kufundishia katika shule za sekondari.

vi.  Ikibainika kuna mwalimu atakayekwenda kuripoti na kuchukua posho na kuondoka, atachukuliwa hatua kwa mujibu wa Sheria.

Ni muhimu kuzingatia maelekezo haya, ikiwa ni pamoja na muda uliowekwa kuripoti kuepuka usumbufu unaoweza kujitokeza.

Limetolewa na
Ndg. Jumanne A. Sagini
KATIBU MKUU
OFISI YA WAZIRI MKUU-TAMISEMI 
______________










No comments:

Post a Comment

Previous Page Next Page Home