Thursday, January 21, 2016

MATOKEO YA KIDATO CHA PILI

MATOKEO YA KIDATO CHA PILI

Jumla ya wanafunzi 324,068 wa kidato cha pili sawa na asilimia 89.12 ya wanafunzi  363,666 waliofanya mtihani  wamefaulu kuendelea na kidato cha 3 mwaka 2016.

Jumla ya watahiniwa 164,547 sawa na asilimia 89.00 ya watahiniwa wote wa kike waliofanya mtihani huo wamefaulu.  Kwa upande wa watahiniwa wa kiume, 

watahiniwa 159,521 sawa na asilimia 89.24 ya watahiniwa wote wamefaulu mtihani.
 Huku wanafunzi 39,567 sawa na asilimia 10.88 wameshindwa kukidhi viwango vya kuwaruhusu kuendelea na kidato cha 3

Ufaulu umeshuka kwa baadhi ya masomo kama Uraia, Historia, Jiografia, Kingereza, Fizikia, Biolojia, Hisabati na Book keeping ukilinganisha na mwaka jana
Mikoa ya Mwanza, Dar es salaam, Mbeya na Iringa ndiyo imetoa shulle 10 bora, huku shule 10 zilizofanya vibaya zikitoka katika mikoa ya Tanga, Mtwara, Lindi na Dar es salaam.

MATOKEO YA NGUDU SEC NA BUJIKU SAKILA SEC

NGUDU SECONDARY SCHOOL

Shule ilikuwa na watahiniwa 103 ambao walitakiwa kufanya mtihani wa kidato cha pili ambapo mpangilio wa madaraja (class) upo kama ifuatavyo;
Distinction-4
Merit-12
Credit-18
Pass-53
Absent-6 (hawakufanya mtihani)
Referred-10 (waliorudia mwaka wa masomo)
-------------------------------------------------------------------------------------------------------
Repeater-7 (hawa ni wale waliokuwa wamerudia mwaka)
WALIOONGOZA
-         JONIA JULIAS WANJARA. Ana GPA ya 3.3, Class ni MERIT (Upande wa wasichana)
-         ABDALLAH HEMED NG'OE. Ana GPA ya 5.0  Class ni DISTINCTION (Upande wa wavulana)

BUJIKU SEC SCHOOL

Shule ilikuwa na watahiniwa 143 ambao walitakiwa kufanya mtihani wa kidato cha pili ambapo mpangilio wa madaraja(class) upo kama ifuatavyo;
Distinction-16
Merit-17
Credit-30
Pass-69
Absent-8
Referred-4
--------------------------------------------------------------------------------------------
Repeaters-25
WALIOONGOZA
-         DEVOTHA JERAD LUCAS. Ana GPA ya 4.4, Class ni Distinction
-         HASSANI RAJABU HASSAN. Ana GPA ya 4.7, Class ni DISTINCTION
-         PETER LAMECK YUMBU. Ana GPA ya  4.7, Class ni DISTINCTION

Matokeo yote ya kidato cha pili unaweza kuyapata kupitia link hii http://necta.go.tz/matokeo/ftna2015/html/index.htm au tembelea tovuti ya NECTA kwa maelezo zaidi.

Ukijaribu kulinganisha matokeo ya shule hizi mbili utaona Bujiku Sakila wamefanya vizuri kuliko Ngudu sec. Hali hii imekuwa ikijitokeza hata kwenye matokeo ya kidato cha 4, kwamba Bujiku wanaendelea kuwazidi Ngudu sec katika ufaulu.

Ukichunguza zaidi unashindwa kujua sababu za kwanini shule kongwe kama Ngudu inakuwa na muendelezo wa matokeo mabaya kuanzia form 2 na form 4 ukilinganisha na shule nyingine ambazo bado hazijawa na miundombinu na rasilimali nyingi kama ilivyo kwa shule hii kongwe

Bado shule nyingi zimekuwa na changamoto nyingi hasa za mazingira mazuri ya kusomea, walimu wa kutosha, upatikanaji wa huduma za kijamii n.k. Mwishoni mwa mwaka jana tumeshuhudia walimu takribani 300(wa msingi na sekondari) wakipanga kugoma kufundisha kama madai yao hayajashughulikiwa.

Wanafunzi waliopata Merit, Credit  na Pass wana kazi kubwa ya kufanya ili kuhakikisha wanafanya vizuri kidato cha nne vinginevyo ndiyo tutaendelea kuzalisha vijana wengi wasio na cha kufanya maeneo mengi ya wilaya yetu hasa ya stend almaarufu kama SOKO MJINGA, kusinda wakitabiri matokeo(BETTING) ili siku ziende. Na pengine wahusika wa elimu hawaoni kama kuna tatizo lolote katika mfululizo wa matokeo mabovu haya,.

Mwaka huu tunaanza sera ya ELIMU BURE kuanzia darasa la kwanza hadi kidato cha nne, japo sidhani kama inaweza kuwa bora kama kwanza changamoto za miaka mingi zinazoikumba sekta hii hazijapatiwa ufumbuzi wa kudumu.
NGUDU NYUMBANI

@2016

No comments:

Post a Comment

Previous Page Next Page Home