Monday, June 8, 2015

MULONGO AZINDUA MASHINDANO YA U13 TAIFA JIJINI MWANZA


Mkuu  wa mkoa wa Mwanza Mh. Magessa Mulongo jana kwenye uwanja wa CCM Kirumba akifungua mashindano ya Taifa ya vijana umri chini ya miaka 13

Akifungu mashindano hayo Mh Mulongo amewataka vijana hao kujituma katika michezo na masomo kwa kuwa vyote vinakwenda sambamba

Amesisitiza shirikisho la mpira Tanzania TFF kuongeza juhudi katika kuendeleza soka la vijana

Katika salamu zake za utangulizi Rais wa TFF Jamal Malinzi ameeleza kuwa lengo la mashindano hayo ni kuibua timu ya vijana wenye umri wa miaka 13 ambao watahamishiwa kwenye shule ya Alliance, watakuwa hapo kusoma na kufundishwa mpira.


Mpango wa TFF ni kuwa hadi kufikia mwaka 2019 timu hii itakuwa imara kuiwakilisha Tanzania katika mashindanoya fainali za Afrika umri chini ya miaka 17, fainali ambazo zitafanyika Tanzania

Mikoa yote 25 ya Tanzania bara inashiriki mashindano haya na mkoa wa Dar es salaam umewakilishwa na timu tatu Kinindoni, Ilala na Temeke.
TFF inashukuru Symbion power kwa ushirikiano wa kuendeleza mpira wa vijana


IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA(TFF)



No comments:

Post a Comment

Previous Page Next Page Home