Wednesday, November 25, 2015

ILIKUWA NI LAZIMA MH MANSOOR ASHINDE UBUNGE JIMBO LA KWIMBA 2015


KOMANYA, BONIPHACE, mwandishi wa makala na mmiliki wa blogu
BY NGUDU NYUMBANI BLOG

Ni ukweli usiopingika kuwa, jimbo la Kwimba tangu mfumo wa vyama vingi kuasisiwa mwaka 1992,  na uchaguzi wa kwanza ukihusisha mfumo huo limeongozwa na chama tawala(CCM) kuanzia ngazi za serikali za mitaa, wawakilishi kama madiwani, mbunge, pia halmashauli kuwa chini ya usimamizi wa Ccm. Hali hiyo imeendelea kuonekana katika chaguzi zote zilizofuata nikimaanisha 2000,2005,2010 na 2015.
Japo kwenye uchaguzi wa wawakilishi serikali za mtaa mwishoni mwa mwaka jana wapinzani walipata uwakilishi kwenye baadhi ya vijiji na vitongoji japo haikubadili upepo kisiasa katika jimbo hili.

Kuna baadhi ya mambo au sababu zinazonipelekea kusema ndugu Mansoor alikuwa na nafasi kubwa kushinda ubunge jimbo la kwimba. Machache kati ya mengi ni kama ifuatavyo..

Moja, kukubalika sana maeneo mengi hasa vijijini. Hii ni kete kubwa kwa mgombea yeyote kuweka mazingira ya kushinda uchaguzi hasa ukizingatia vijijini ndio kuna mwitikio mkubwa wa wapiga kura. Imani hiyo kaijenga tangu agombee awamu iliyopita. Pia wananchi wengi walipata kumwamini katika miaka mitano iliyopita, kwa maana hiyo imani yao kubwa ilimjenga na kumpa imani kubwa ya kushinda awamu nyingine. Hapa namaanisha muitikio wao hasa kwenye kampeni zake.

Pili, nguvu ya pesa aliyonayo. Pia katika hili mgombea huyu alikuwa vizuri ukilinganisha na wapinzani wake. Katumia njia hii kucheza na akili za wananchi kwa kugawa kiasi cha fedha, nguo na vifaa vya chama. Pia katika hatua nyingine kupitia wapambe wake amegawa majembe baadhi ya vijiji kuhamasisha maendeleo. Njia hii imeongeza imani kwa wana ccm na wananchi wasio na vyama hata baadhi ya wapinzani wasio na msimamo kuwa na matumaini nae. Japo uhalisia ni kwamba inakosekana elimu ya uraia kwa wananchi kujua zawadi hizi kipindi cha kampeni hazina manufaa ya kudumu katika maisha yao ya kila siku ukizingatia hutolewa mara moja kila baada ya miaka mitano.

Tatu, kukosekana kwa upinzani imara wenye kuweza kujenga hoja na kuja na sera za kuweza kuwashawishi wananchi wawachague. Katika hili pia UKAWA kushindwa kufikia makubaliano ya kusimamisha mgombea mmoja na badala yake kusimamisha wawili ndugu Mh shilogela(CDM) na Mh Ntiga Otto(CUF) kulisaidia kwa kiasi kikubwa kugawana kura za upinzani na kumpa nafasi Mh mansoor kuwaacha kwa mbali kwenye mchuano.

Nne, kuwaaminisha wananchi baadhi ya mambo kama kayafanikisha. Kati hili ndugu Mansoor aliweza kuanisha mafanikio katika awamu iliyopita kama kuwaletea wananchi maji kutoka ziwa Victoria, umeme, kuwezesha ujengwaji wa  zahanati/vituo vya afya kadhaa. Kuweka mambo sawa ni kuwa kazi ya mbunge kwa mujibu wa katiba ni kuwakilisha wananchi, kutunga sheria na kusimamia serikali katika masuala ya maendeleo kama kusimamia miradi. Ila sio kweli kwamba kawaletea wananchi maji wala umeme, bali ni kupitia kuishauri na kuikumbusha serikali kufanya hayo na mengine jimboni kwake ila hana uwezo wa kutoa hela yake kufanikisha hayo. Katika hili la maji limekuwa likipigiwa kelele tangu kale na limekuwa likihubiliwa kwenye ilani ya ccm kila uchaguzi na limekuja kufanikishwa kwa kucheleweshwa kwenye uongozi wa JK japo lilikuwepo tangu enzi za Mkapa. Hapa naweza kuwapongeza Mh mansoor na Mh Leticia Nyerere ambao walipata kuliulizia utekelezaji wake kila walipopata nafasi kwenye bunge kuuliza swali au kujenga hoja kila mmoja katika nafasi yake. Katika hayo alifanikiwa kujipatia kura za kutosha.

Tano, jimbo bado ni ngome kuu(stronghood) ya chama tawala. Hili pia linachangia kwa asilimia kubwa kama sehemu ni ngome ya chama fulani miaka nenda rudi ni rahisi kwa chama husika kushinda japo kuna baadhi ya maeneo hali ilibadilika na ambaye hakutarajiwa kushinda.
Jimbo la Kwimba lipo chini ya Ccm kabla ya mfumo wa vyama vingi, baada ya kuanzishwa mfumo wa vyama vingi hadi leo huku wakijikusanyia madiwani wengi na kuweza kuisimamia halmashauri. Kwahiyo upinzani walipaswa kutumia nguvu zaidi na njia mbadala za kuwawezesha kushinda.

MAONI YANGU
Nilipata kufatilia uchaguzi kwa kuwasikiliza wagombea kama Mh Mansoor, Mh shilogela na Ndugu Ntiga kusikiliza sera zao na hoja zao juu ya uwakilishi wa jimbo letu.
 Kiukweli nilimwelewa sana ndugu Ntiga Otto jinsi alivyokuwa akiwasilisha Mipango na mikakati yake juu ya kuiongoza Kwimba, japo ni hali isiyofichika kwamba ndiye alikuwa na wasikilizaji/wananchi wachache zaidi ukilinganisha na hao wenzake wawili waliokuwa na watu wengi.
 Hawa Iswalala(UDP) na mch. Yohana(ACT) sikupata kuwasikia ama kuhudhulia kampeni zao. Bila shaka kilichomwangusha huyu kijana aliyejimbanua(Otto) ni kutokukubaliana kwenye umoja wao. Pia ‘mind set’ za wananchi wengi ambao hawako tayari kusikiliza sera na kubakia kushabikia vyama zaidi.
Salamu zangu hizi zimfikie popote alipo na asikate tama ajipange kwa awamu ijayo.
Uchaguzi umeisha, mbunge na madiwani wamepatikana, cha msingi ni kuwapa support tuweze kufikia lengo la kupiga hatua ya maendeleo jimbo na wilaya yetu kwa ujumla.
 Malalamiko ya kwamba huyu mhindi, sijui sio mzawa hayatosaidia kitu zaidi ya kushirikiana na kiongozi aliyeshinda kusukuma gurudumu la maendeleo. Pia ideology ya kuwa mbunge ndio mtu sahihi wa kuleta maendeleo jimboni, ni ya kupuuzwa tu. kila mmoja wetu anayo nafasi ya kuleta maendeleo kwenye jamii yake na sio kusubiri fulani akuletee maendeleo mlangoni.
tunawa support viongozi wa ngazi zote tukiweka itikadi za vyama vyetu pembeni. Sote ni wamoja ubaguzi ni kuonesha udhaifu.

kutokana na machache niliyoyagusia hapo juu, nashawishika kusema kwamba Ilikuwa ni lazima kwa mh. Mansoor kushinda ubunge kwenye jimbo la Kwimba mwaka 2015.

KWIMBA TUITAKAYO
nguduone@gmail.com




No comments:

Post a Comment

Previous Page Next Page Home