Friday, November 13, 2015

TUME YATOA MAELEZO NA IDADI YA MADIWANI VITI MAALUM


JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
UTEUZI WA MADIWANI WANAWAKE WA VITI MAALUM

Kwa mujibu wa Kifungu cha 86 A (8) cha Sheria ya Uchaguzi Serikali za Mitaa Sura ya 292, (Uchaguzi wa Madiwani) kikisomwa kwa pamoja na Vifungu vya 35 (1) (c) na 19 (1) (c) vya Sheria za Serikali za Mitaa (Tawala za Wilaya) na Na. 7 ya mwaka 1982 na Serikali za Mitaa (Tawala za Miji) Na. 8 ya mwaka 1982, Tume ya Taifa ya Uchaguzi imepewa mamlaka ya kushughulikia na kutangaza Viti Maalum vya Madiwani Wanawake visivyopungua 1/3 ya Madiwani wa kuchaguliwa katika kila Halmashauri. Kwa kuwa Kata 3,957 zilifanya Uchaguzi Mkuu 2015 hivyo 1/3 yaViti Maalum vya Madiwani Wanawake ni 1,406. Hata hivyo, Tume haikuweza kugawa Viti vyote katika Halmashauri kutokana na kuahirishwa kwa Uchaguzi wa baadhi ya Kata katika baadhi ya Halmashauri nchini. Mgawanyo wa viti vilivyobaki utafanyika mara baada ya chaguzi zilizoahirishwa kufanyika.
Vyama vya Siasa vilivyoshiriki Uchaguzi Mkuu kwa upande wa Madiwani na kukidhi vigezo vya kisheria vya kupata Viti Maalum ni kama ifuatavyo:-


Jumla ya Viti vilivyogawanywa ni 1,392.
 Viti 14 vilivyosalia vitagawanywa mara baada ya Kata zilizoahirishiwa Uchaguzi kukamilisha zoezi la kupiga Kura
Majina ya Madiwani Wanawake wa Viti Maalum kwa kila Halmashauri walioteuliwa yataweza kupatikana kutoka Vyama na kwenye Halmashauri husika. Aidha tarehe 14/11/2015, Tume ya Taifa ya Uchaguzi itatangaza majina ya Madiwani wa Viti Maalum walioteuliwa. Ikumbukwe kuwa Tume imefanya uteuzi kwa kuzingatia Orodha iliyowasilishwa Tume na kila Chama kwa kuzingatia vipaumbele vya Chama husika.

Imetolewa na:
Jaji (Mst.) Damian Z. Lubuva
MWENYEKITI TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI

12/11/2015

No comments:

Post a Comment

Previous Page Next Page Home