Thursday, January 21, 2016

RIPOTI YA MWAKA 2015 JUU YA MAMBO YALIYOJIRI KWA HISANI YA NGUDU NYUMBANI BLOG


RIPOTI YA MWAKA JUU YA MAMBO YALIYOJIRI KWA HISANI YA NGUDU NYUMBANI BLOG

Hii ni ripoti iliyojumuisha mambo mbalimbali ambayo blogu ya Ngudu nyumbani (www.ngudukwimba.blogspot.com) ilipata kuyakusanya kwa mwaka huu kutoka vyanzo mbalimbali vya habari na watu binafsi. Hivyo imepata kuyapanga mambo kwenye makundi kama yalivyoainishwa hapo chini. Twende pamoja…

ULINZI NA USALAMA
Katika hili mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wa wilaya ambaye ni mkuu wa wilaya ambapo chombo cha ulinzi na usalama ndio washauri wake hivyo yeye ndiye mwenye jukumu kubwa la kuhakikisha anafuatilia kwa ukaribu zaidi usalama wa raia wake. Ndani ya mwaka huu kumepata kutokea matukio baadhi ambayo kwa namna moja au nyingine hayakuleta picha nzuri kwenye jamii yetu.

1. Tukio la mkazi mmoja wa ngudu kukutwa amefariki alipokuwa kwenye magereza kitu ambacho kilivuta hisia za watu wengi ambapo kuna mambo kadhaa yaliendelea hapo baada ya kuzuka sintofahamu juu ya kifo chake.

2.Pia tukio jingine ni lile la mtoto mwenye ulemavu wa ngozi(Pendo Emanuel) kijiji cha ndamhi  kata ya fukalo alipopotea kwenye mazingira ya kutatanisha na kupelekea jeshi la polisi kuingilia kati kwa kufanya upelelzi na msako mkali juu ya kupotea kwa mtoto huyo. Tukio hili lilitokea kati mwishoni mwa mwaka jana na mwanzoni mwa mwaka huu.

ELIMU (MATOKEO)
MSINGI-DARASA LA SABA
Upande wa elimu naweza kujikita zaidi katika matokeo ya shule zilizoongoza kiwilaya na zilizoshika nafasi ya mwisho pia. Kwa upande wa shule za msingi
Kimiza primary school inayopatikana kata ya lyoma iliongoza kati ya shule 151 katika wilaya, huku ikiwa ya 30 kimkoa kati ya shule 900 na ya 126 kitaifa kati ya 16096. Ikumbukwe kimiza primary ndiyo iliongoza hata kwenye matokeo ya mwaka jana

MATOKEO KIDATO CHA 4
Mfumo mpya wa upangaji wa matokeo kulingana na grade ulihusika mwaka huu. Baadhi ya matokeo ya shule zilizojitahidi katika ufaulu yapo kama ifuatavyo;
Ngudu sec
Distinction=2, merit=8, credit=18, pass=39, fail=18
Bujiku sec
distinction=2, merit=12, credit=21, pass=38, fail=22
Nyamilama sec
distinction=2, merit=7, credit=17, pass=44, fail=34
**matokeo ya form 2 pia yalihusisha mfumo mpya wa upangaji matokeo kwa grade

MATOKEO YA KUJIUNGA NA KIDATO CHA 5
TAMISEMI; matokeo ya kujiunga na kidato cha 5 yaliyotoka mwaka huu yakihusisha wanafunzi waliohitimu kidato cha nne mwaka 2014 ambapo wilaya ya Kwimba ina jumla ya shule za sekondari 28, ambapo 27 ni za serikali na 1 ya binafsi.

Sumve girls sec school(private)
waliochaguliwa jumla=56
wavualana=0, wasichana=56

Kwa shule za serikali, Bujiku sakila sekondari ndiyo iliongoza kupeleka idadi kubwa(25) ya wanafunzi kidato cha 5, naya mwisho ni Bupamwa sekondari iliyopeleka wanafunzi wawili na Mhande sec akipeleka wanafunzi watatu tu..

Bupamwa sec school
waliochaguliwa 2
wavulana =2, wasichana=0

Bujiku sakila sec school
Waliochaguliwa jumla=25
wavulana=16, wasichana=9

Shule nyingine zilizofatia kwa kupeleka wanafunzi wengi ni Ngudu sec na Nyamilama ambapo zilizopeleka wanafunzi 22 kila moja.

Pia katika hatua nyingine NACTE katika hotuba yao juu ya kuvifuta usajili na kuvishusha hadhi baadhi ya vyuo nchini, chuo cha afya, Ngudu School of Environmental Health Sciences – Kwimba ni moja ya Taasisi  na Vyuo vilivyoshushwa hadhi baada ya kutotimiza masharti ya Ithibati   ambapo (hadhi kabla ya notisi)-Ithibati ya Awali, na (hadhi baada ya notisi)-Usajili wa Muda

TAKWIMU MBALIMBALI

1. MAENEO YA UTAWALA KATIKA MAMLAKA ZA SERIKALI ZA MITAA (MAMLAKA ZA WILAYA MWAKA 2015 GN. 221 LA TAREHE 5/6/2015 )
Kupitia TAMISEMI ilitolewa takwimu ya orodha ya mamlaka za wilaya zote nchini ambapo katika wilaya ya Kwimba takwimu zilikuwa kama ifuatavyo;
Kata=30, vijiji=119, vitongoji=870

2. Makadilio ya idadi ya wapiga Kura wilaya ya kwimba (national bureau of statistics)
Jimbo la kwimba
Makadirio ya idadi ya watu kwa mwaka 2015= 235,818.
Makadirio ya watu wenye miaka 18 na zaidi= 102,763
Jimbo la sumve
makadirio ya idadi ya watu kwa mwaka 2015= 203,166
Makadirio ya watu wenye miaka 18 na zaidi= 87,993 

UKUAJI WA TEKNOLOJIA
Katika secta hii mitandao ya kijamii na vyombo vya upashaji habari ndio vinahusika. Ambapo kuna baadhi ya blogu za kijamii zimepata kuanzishwa ndani ya mwaka huu

Ngudu nyumbani blog
Jumla ya machapicho(post) kwa mwaka huu ni 41
Jumla ya watembeleaji kwenye blogu mpaka sasa=8085
Ngudu nyumbani (facebook page)= like 251
Tatizo kubwa linakuja pale ambayo wilaya inapokuwa haina Tovuti ya habari wala angalau blogu ambayo inakuwa chini ya halimashauri ambapo taarifa za muhimu kama miradi ya maendeleo, matangazo, maagizo, maazimio ya baraza la madiwani na mambo mengine yangepatwa kuwekwa kule ili kuwapa uwezo wananchi kujua yanayoendelea kwenye wilaya. 

Katika hili NGUDU NYUMBANI BLOG ilipata kushauri wazo hili ambapo mmiliki wa blogu alionana na uongozi wa halmashauri(DED) na kumwelezea, wazo likapokelewa na kufikishwa kitengo cha Tehama na kushauri mhusika aandae pendekezo(proposal) juu ya uendeshaji wa blogu hiyo.
 Zoezi lilifanyika pendekezo likaandaliwa na jinsi ambavyo mambo yatakuwa(kuanzisha blogu na baadae kuwa na tovuti maalumu) lakini cha ajabu tangu kutumwa kwa mapendekezo hayo(kwa barua pepe) mapema mwezi May mwaka huu hadi leo hakuna majibu yoyote na hakuna jitihada zozote juu ya uanzishwaji wa tovuti wala nini,  pengine ni kweli wazo halikuwa zuri kwao basi jitihada za kulifikisha wazo hili na kufanyiwa kazi zilikomea hapo.
 Ukiachana na hilo kwenye tovuti ya mkoa(www.mwanza.go.tz) kuna kiungo(link) ya Kwimbadc ambayo kwa mwaka sasa ipo kwenye majaribio kitu cha ajabu sana hiki. Kwa wataalamu wa IT wanajua tovuti inachukua siku 3 kukamilika(kuwa na domain name na kuwa hosted) kwa blogu ni masaa kadhaa tu inakua hewani(blogu ni bure katika kuifungua) lakini hili kwa wilaya yetu limekuwa janga. 
Wadau wa maendeleo wenye kujua umuhimu wa tovuti hizi wanaweza kusaidia kushauri pia kuanzia mwakani tuanze na mambo mapya kwasababu najua kitengo cha Tehama kipo na kitengo cha habari pia kipo wasisite kufanikisha hili(kumewahi kuwepo blogu ya wilaya miaka ya 2012), na panapotokea kuhitaji msaada NGUDU NYUMBANI BLOG  ipo kuwasaidia.

Katika upande wa blogs pia kuna baadhi ya blogu zimeanzishwa mwaka huu lengo kuu ni kuhamasisha maendeleo na kutoa taarifa husika.

1. KWIMBA KWETU (www.kwimbanyumbani.blogspot.com) hii inajihusisha na miradi ya kimaendeleo hasa masuala ya elimu kwenye shule zilizoko vijijini

2. NGUDU SCHOOL OF ENVIRONMENTAL HEALTH SERVICE(www.nguduschool.blogspot.com) hii blogu ikiwa maalumu kwa chuo cha afya japo bado haijawa na muonekano mzuri mhusika anaweza wasiliana na ngudu nyumbani blog wakasaidiana katika hilo.

UCHAGUZI MKUU

Katika uchaguzi mkuu uliofanyika mapema mwezi octoba 25 mwaka huu

UBUNGE NA UDIWANI JIMBO LA KWIMBA
Katika jimbo la kwimba nafasi ya ubunge kulikuwa na washiriki wa5 kutoka vyama mbalimbali ambapo ndugu Mansoor Shanif Hiran(CCM) alishinda na kutangazwa kuwa mbunge halali wa jimbo hii ni mara ya pili mfululizo ambapo mwaka 2010 pia alishinda kiti hicho,  akiwashinda wapinzani wake ndugu Shilogela(CDM) na Otto(CUF). 
Na kitu cha ajabu kidogo ni kuwa mgombea wa  UDP ndugu Aloyce Iswalala Isanzu hakupata hata kura 1 kwa jimbo zima
Kwenye nafasi ya udiwani, jimbo la Kwimba lina kata 15 ambapo kata 14 walishinda CCM na kata 1(Ng’wangalanga) ikichukuliwa na CDM

UBUNGE NA UDIWANI JIMBO LA SUMVE
Nafasi ya ubunge ilikuwa na wagombea wa4, ambapo ndugu Ndassa Richard Mganga(CCM) alishinda na kutangazwa kuwa mshindi katika uchaguzi huo huku akipata upinzani mkali kutoka kwa ndugu Mchele(CUF) na Ng’holo(CDM)
Kwenye uchaguzi wa madiwani ambapo jimbo la Sumve lina kata 15,  CCM alishinda kata 11, CDM kata 3 na CUF kata 1

UCHAGUZI VIONGOZI HALMASHAURI YA WILAYA (M/KITI NA MSAIDIZI)
Katika baraza la wawakilishi(madiwani) kulifanyika pia uchaguzi wa mwenyekiti wa halimashauri ambapo baraza lilihusisha wajumbe 42.
 Ambapo mchanganuo wake upo hivi; CCM wajumbe 36(madiwani 14 kwimba, madiwani 11 sumve, wabunge 2, viti maalumu 9) CDM ina wajumbe 4 + 1 viti maalumu jumla 5 na CUF ina mjumbe mmoja. 
Katika uchaguzi huo Ccm iliweza kuongoza na hivyo kuendelea kuiongoza halimashauri ya wilaya ya Kwimba kwa awamu ya 5 mfululizo tangu kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi

MENGINEYO
1. Kulifanyika uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura zoezi lililohusisha mikoa na wilaya zote nchini
2. Taasisi ya kifedha ya bayport financial service inayojihusisha na mambo ya mikopo kufungua tawi kwimba mkoa wa mwanza

MWISHO
Ningependa kusikia maoni, ushauri, marekebisho na kitu chochote juu ya report hii na blogu ya Ngudu nyumbani kwa ujumla + page ya facebook(ngudu nyumbani) ili tuanze mwaka mpya na mambo mapya.

Asanteni sana.
NGUDU NYUMBANI
nguduone@gmail.com

No comments:

Post a Comment

Previous Page Next Page Home