Tuesday, April 5, 2016

WATU NINAOJIVUNIA KATIKA TASNIA YA SANAA KWIMBA KWETU(SEHEMU YA 1)


BY NGUDU NYUMBANI BLOG
05/04/2016.
(SEHEMU YA KWANZA)

KATIKA maisha, hali ya kujiamini juu ya kile unachokifanya na kukifanya kwa utashi na utulivu mkubwa ndiyo silaha muhimu kuelekea mafanikio. Licha ya kujiamini ni lazima kukubaliana na matokeo kwa kukubali changamoto zinazokukabili na kujua namna bora ya kuzikabili ili usonge mbele.

Leo nimeamua kuwakumbuka baadhi ya ndugu zangu hasa kwenye tasnia ya sanaa kwa ujumla wake. Nimejaribu kuwazungumzia vijana baadhi waliojihusisha na sanaa hasa ‘wasanii’ kipindi cha nyuma.  Ambapo wengi wao walifanya kama hobby(kwa kipindi hicho baadae wakaachana nayo) na wengine waliwekeza muda mwingi kuhakikisha wanaendelea na utaratibu huo na leo tunawatambua kama wasanii.

Nakumbuka kipindi hicho, vijana wengi walikuwa wanapenda hasa kuimba. Jamaa zangu,  Omary Kigoda na Juma Damas( mwenyezi amlaze mahala pema)  walikuwa ni watu wa kuandika mashairi mara kadhaa ila changamoto ilikuwa namna ya kupata au kuvifikia vyombo vya kurekodia mashairi hayo, kipindi hicho hapakuwa/hawakuwa na simu za kurekodi japo sauti kama ilivyo leo. Mbali na kuimba bwana omary alipenda kuigiza pia.

Kwa sasa Omary licha ya kuwa mtumishi wa serikali lakini anajihusisha na sanaa pia(kuigiza na kuandaa filamu), ambapo amehusika kwenye baadhi ya filamu  ikiwemo ‘MADNESS’  iliyopo sokoni kwa sasa unaweza kuitafuta na kuitazama. Mdogo wake pia msharo (Shaban) ni msanii anayewakilisha kundi la THE WINNERS ambapo naye amepata kufanya kazi kadhaa ikiwemo ‘Bolingo nangaye’ akimshirikisha  Man M the winner. Video yao na video nyingine unaweza kuzipitia HAPA

Kipindi hicho  wasanii wakubwa  walikuja kutoa burudani wilayani katika kumbi tofauti enzi hizo ‘Safari club’ na KWIDECO ndio zilitumika zaidi. Wasanii kama Inspecta haroun(Babu), Bwana misosi,  Mzee wa ‘mashikolo mageni(jina nimesahau)’ na wengine wengi walitumbuiza. Sikupata kuwapo katika show ya Inspecta Haroun ambapo ilitokea vurumai kubwa ikisemekana kwamba hakuwa yeye bali ni jamaa tu aliyekuwa akicheza ‘Track’ na kufatiliza na sio kuimba Live kama wanavyofanya wengi kwa kuwekewa mdundo tu.

Ni kipindi ambacho watu kama Cosmas Kulwa(CK) na wenzie kipindi wapo Ngudu sekondari  walionekana kufanya mziki na kukubalika na wengi. Sina kumbukumbu nzuri kama Dickson Philipo na sullu cosmas nao walihusika pamoja na CK wakati huo. CK aliendelea na kujihusisha na mziki ila wenzie walijihusisha kwa muda na kuacha pengine sababu ya majukumu mengine waliyokuwa nayo.

Ni kipindi hicho ambapo Storyteller Rhymes au ‘Aron Deus’, au  ‘Mboni’ na wengine tulipenda kumwita ‘Mwibonya’. Enzi izo akiwa Ngudu sec kwenye sherehe kama Graduation na nyinginezo alipata kuonesha uwezo wa kuFlow kwa aina yake, mziki wa hip hop. Alikuwa na uwezo wa kuandika mashairi yenye vina na kuyaimba kwa namna iliyowavutia wengi. Sina hakika kama anaendelea na kufanya mziki licha ya kuwa na kipaji cha kucheza mpira wa miguu pia. Nilipata kusikiliza wimbo wake mmoja, japo sina hakika na pengine kumbukumbu sahihi  ya nyimbo alizowahi kurekodi na kama anaendelea kujihusisha nao mpaka leo.

Kuna vijana wengine wengi pia walikuwa wakiimba kipindi hicho, PUNGU na wadogo zake ni mfano mzuri kwa wanaolifahau jina hili. Pia Igo Lyric Re-chird au ‘Richard’, akiwakiwakilisha vizuri kutoka pande za Welamasonga . Japo hata sasa bwana Igo lyric anaonekana kama kujihusisha na mziki licha ya kuwa mwanafunzi wa chuo.

Ni kipindi hicho ambapo ‘Dj Jigga’ akifanya vizuri zaidi kutoa burudani murua pande za Kwideco(akishirikiana vizuri na jamaa zake Masuka na Edo).  kulikuwepo na ma DJ wengi kipindi hicho pengine nisiweze kuwakumbuka wote. Baadae akaja DJ Kisandu  kabla ya kuachana na kazi hiyo na kujihusisha na kazi nyingine. Vijana kadhaa walipata kuvutiwa na kazi hii wakiwemo DJ SOLEJI, DVJ COLINE na wengine wengi ambao wengi wao wanaendelea na kazi hiyo hadi leo.

Raymond akiwakilisha toka pande za kwa ‘madiba’ au Ngudulugulu kama inavyofahamika kwa wengi. Huyu nae alikuwa anapenda kuimba tangu yupo shuleni. Japo maisha yanaenda kwa kasi sina hakika kama bado anaendelea nao au ilikuwa ni uchakaramu  wa shuleni tu enzi hizo. Mtu kama FREDRICK MASHUDA katika ubora wake wa kutangaza na sauti yake nzito ile kipindi hicho ilikuwa burudani ya aina yake.

Bwana mdogo ‘Physical GoldChain’ au kwa jina jingine Danny Sayi, nae hakuwa nyuma kipindi hicho kwenye kuimba. Pengine

Ukiachana na waliokuwa wakiimba, kuna waliokuwa wanacheza hasa mziki wa Dancehall, kundi hili lilikuwa na vijana wengi baadhi yao ni Shirugu, Tunda(kulwa & dotto), Dome, na wengineo ambapo kuna kipindi walivuma sana kiasi cha kuvutia vijana wengi kupenda kucheza pia. Ndio kipindi hicho sherehe za kuzaliwa(birthday) zikifanyika kwa wingi sana ama ukumbi ukiwa nyumbani kwa mwenye sherehe au mara kadhaa ukumbi wa ‘Chuo cha afya’, KWIDECO au Safari Club na kwingineko.

HALI ILIVYO KWA SASA.
Maisha yanaenda kasi sana kiasi cha umri kwenda na kila mmoja kuwa na majukumu yake.  Kuna ambao wanatambulika kama wasanii kwa sasa na wengine walikomea enzi hizo na kwa sasa kila mmoja ana ‘mishe’ zake. Baadhi ya wanaotambulika na kujulikana kwa wengi;

LEDDY CHOMBO(RED MAN)
Wengi wetu tunamfahamu huyu jamaa na amewahi fanya nyimbo nyingi. Sina kumbukumbu vizuri lakini nakumbuka aliwahi kutoa Album na kuizindua pale KWIDECO miaka ya 2007 au 2008 hivi. Mpaka sasa anafanya mziki japo kwa upande wangu naona sio kwa kasi kama aliyokuwa nayo kipindi kile cha  nyuma. Mwezi wa pili mwaka huu alitoa wimbo ‘Happy Birthday’ bila shaka wengi wetu mliusikia. Pia kwa kiasi Fulani anajihusisha katika kutayarisha muziki pia.

STAR JAY
Huyu pia ni zao la Kwimba ila kwa kiasi kikubwa kazi zake za muziki anazifanyia Dar es salaam. Naambiwa pia licha ya kuimba, anaweza kutengeneza beat(producer). Mzee wa zidisha makopa na Good time. Nilikuwa namsikia mara kadhaa ila nilimsikia katika ubora wake kwenye uzinduzi wa album ya Leddy Chombo ambapo alikuwa akimpa support. Unaweza kusaka nyimbo zake zipo mtandaoni kwa wale wasiomjua.

CK
Huyu brother licha ya kufanya shughuli nyingine zinazomwingizia kipato pia anaendelea kufanya mziki. Nimepata kuongea nae mara kadhaa changamoto yake kubwa ikiwa ni namna ya kurekodi mziki wake na kuusambaza uufikie umma kwa haraka na urahisi. Kipindi ambacho leddy anafanya vizuri na kusikika kwa kasi ndipo hata CK nae alikuwa ‘hot’ vile vile.
JOE  DASUKUMA
Kwa wale waliopo kwenye groups za facebook bila shaka wamewahi kuona akijinasibu mara kadhaa. Kuna wimbo wa ‘ONE DAY’ amepata kufanya. Simfahamu vizuri lakini inatosha kwa namna ambavyo anavyotoa updates za kazi zake anazofanya. Anaweza kama akiwepa muda wakusikilizwa na kupata support inayostahili, bila shaka nyota yake itang’aa zaidi.

DOGO SILVER
Kama yeye jinsi anavyojiita au unaweza mwita MABEYO, uchakaramu wake ulianza kuonekana tangu yupo shuleni hasa pale NGUDU sekondari. Katika harakati za kutaka kutoka na kufanya anachoamini kinaweza kumtoa. Amefanikiwa kutoa nyimbo kadhaa mojawapo akimshirikisha  PNC(shino) kwenye wimbo unaoitwa ‘Ukweli wa mambo’(unaweza kuutafuta mtandaoni ukaupa nafasi kwenye masikio yako).
 Aliwahi kuwa na mpango wa kufanya Track na Ommy dimpoz kipindi cha nyuma lakini sijui nini kilimkwamisha pengine. Kwa sasa naambiwa analitumikia jeshi la wananchi hivyo nafasi yake kujihusisha na masuala ya muziki ni ndogo sana.

WENGINEO MBALI NA KUIMBA.

LUCY CHARLES
Huyu ni mwana mitindo mzawa wa Kwimba, ni binti mrembo na msomi pia. Amewahi kushinda mataji kadhaa huko nyuma kama MISS MWANZA na MISS LAKE ZONE. Kwa sasa anajishughulisha zaidi na masuala ya mitindo pamoja na shughuli nyingine.
 Kupitia huyu vijana wengi(wakike) wanaweza kuvutiwa na kuwa inspired na kile anachokifanya endapo tu watautambua mchango wake na msaada wake katika kuwasaidia njia kwa wale wenye lengo la kuwa kama yeye na zaidi. Binafsi siwezi kuelezea mchango wake, zaidi ya kujivunia  kuwa na mtu kama yeye kwenye jamii yetu.
Blogu yetu kupitia HAPA ilipata kuweka picha zake kama kutambua anachokifanya pia. Unaweza kufungua link hiyo kuziona hasa kwa wasiomjua.

KING SUKA.
Huyu kaka mkubwa yupo kwenye tasnia ya filamu kama mwigizaji na muongozaji  ambapo amehusika kwenye filamu kadhaa. Pia ni mmiliki wa blogu ya kijamii KING OF NEWS
Kupitia yeye , anaweza saidia vijana wengi nyuma yake njia sahihi za kufuata na hatimaye kutoka kupitia tasnia hiyo ya filamu na uigizaji. Na imani analijua hilo na analifanya kwa ustadi mkubwa kusaidia wengine katika sanaa.

Hawa ni baadhi ya ninaowafahamu na kuwasikia wakifanya mambo yao kwenye tasnia ya sanaa kwa ujumla. Pengine wapo wengine wengi ambao siwajui lakini mmojawapo miongoni mwetu akawa anawajua na taarifa zao anaweza kutujuza pia.
Kila mmojawetu ana jukumu kubwa la ku-support hawa watu na wengine kwenye tasnia ya sanaa  ili kuwafanya waendelee kufanya vizuri.

Pia wao nao kila mmoja wao kwa nafasi yake anapaswa kujua jamii iliyomzunguka inataka nini kwake. Pia tunategemea mchango wao  mkubwa kwenye ujenzi wa jamii  yetu pia.
Ningependa kuweka sawa kitu kimoja kwamba, kwa asilimia kubwa hao niliowazungumzia wanatokea kata ya NGUDU, japo kama wilaya tuna kata 30 hivyo naamini watakuwepo wengine wengi.

Itaendelea sehemu ya pili siku nyingine kulingana na mahitaji na mapendekezo ya wadau….

Tafakari!
KWIMBA TUITAKAYO
nguduone@gmail.com





No comments:

Post a Comment

Previous Page Next Page Home